6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 3,653
- 8,000
Niaje waungwana.
Kama kawaida, leo nimekuja kutoa somo kamili kwa wale wayahudi uchwara wa Tandale kwa Mtogole, wasiojua nguvu halisi ya Iran katika miaka iliyopita, iliyopo na ijayo.
Bila kuongelea kuhusu dola la Iran (Persia Empire) ambayo ilitawala eneo zima la Mashariki ya kati kabla hata ya kuzaliwa Uyahudi, Israel, Firauni, Ibrahim, Yesu nk.
Leo napenda kuongelea Iran ya leo ambayo imeweza kushinda vita vya maneno na vitendo, dhidi ya maadui zake wakubwa duniani, ambao ni Marekani, Israel na kwa mbali nchi za Ulaya Magharibi.
Baada ya Marekani, Israel na washirika wao kushindwa kuidhibiti Iran kwa njia ya vita baridi, waliamua kuwatumia waarab njaa kama vile Saudi Arabia, Jordan, Iraq nk kuitenga nchi hiyo kupitia mgongo wa utofauti wa kiimani kama vile ushia na usunni. Vita hii ilileta mgawanyiko mkubwa, haswa ukizingatia waarab wengi hawana elimu yoyote ya kuweza kutambua kile kinachopandikizwa juu yao na jirani yao.
Baada ya kufanikiwa kupandikiza chuki hizo, wakaangalia nchi 1 wapo ambayo wakiipa silaha za kutosha itaweza kuingia vitani na Iran, kupambana na Iran, kuishinda Iran, kuuangusha utawala wa Iran na hatimae kuweka kibaraka wao ambae atakuwa tayari kufata yale yanayotakiwa na nchi hizo zilizotoa msaada wa kivita.
Basi bwana baada ya kukaa chini kutafakari, wakaona Iraq ndio nchi pekee itakayoweza kukamilisha mission kutokana na Jiografia, aina ya kiongozi (Sadam) plus propaganda za ki ushia na ki usunni. Bila kuchelewesha muda, Sadam akawezeshwa akaingia mzigoni kwa kushtukiza huku Iran Lisa haijajipanga, haina backup, Plus vikwazo vikali vya kiuchumi na silaha. Vita ile ilienda miaka 8, from 1980 hadi 1988, huku Iraq ikipewa kila aina ya silaha na Marekani ili iweze kushinda vita hiyo. Pamoja na Iran kukosa backup na vikwazo juu lkn iliweza kulinda mipaka yake na uongozi wake hadi kupelekea Sadam mwenyewe na maboss zake kunyoosha mikono ya kuomba poo ili vita iishe.
Baada ya vita kuisha bila Marekani na washirika wake kupata walichokitaka, walichukia na kuanza kuonesha chuki za wazi kwa Sadam baada ya kuwaingiza hasara ya silaha Kwa muda wa miaka 8, bila ushindi wowote. Chuki hii dhidi ya Sadam iliendelea, huku Sadam nae akipanga kuzitumia silaha zilizobaki kuishambulia Israel ambayo nayo ilikuwa kwenye mission ya kuitumia Iraq kama daraja la kuuangusha utawala wa Ayatollah na serikali yake.
Baada ya mbinu zile za ushia, sunni na vita kupitia Iraq kukwama, wakaja na mbinu za kutengeneza makundi ya mujahidina ili wayatumie kuyumbisha usalama wa eneo zima linaloizunguka Iran, Na baadae wayatumie kuingia Iran kufanya ugaidi na hatimae waanzishe vita dhidi ya serikali ya Iran. Iran ililiona hilo na kuamua kutengeneza na yenyewe makundi ya wapiganaji katika eneo linaloizunguka Israel na washirika wao wa Middle East. Ili wao wakimwaga ugali na yeye amwage mboga.
Lakini kama hiyo haitoshi Iran ikaendelea kujiimarisha Kwa teknolojia yake mwenyewe, silaha zao wenyewe nk.
Baada ya mbinu zote kukwama topeni, Marekani akaamua kumtumia mshirika wake alie karibu na eneo hilo (Israel) kufanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya viongozi wa jeshi, serikali na miundombinu ya ulinzi, kwa lengo la kuuangusha utawala walioushindwa kuuangusha miaka mingi iliyopita, huku Marekani ikiahidi kutoa support yoyote pale itapohitajika kufanya hivyo.
Intelejensia yao (US na Israel) zilijua kwamba baada ya ambush kufanyika, hakutakuwa na mwanajeshi hata 1 atakae kuwa na uwezo wa kushika hata kisu kuilinda nchi yake. Waliamini mbinu iliyotumika kuuangusha utawala wa Sadam na Ghadafi ingeweza tena kutumika kuuangusha utawala wa Jemedari Ayatollah. Wakasahau kwamba wale kina Sadam na Ghadafi walikuwa ni Waarab ambao nchi zao hazina historia sawa hata kidogo na Iran ambao ni waajemi, watu wenye akili na uwezo wa kuweza kupigana vita yoyote ile, tangu miaka na miaka.
Baada ya maandalizi ya kutosha Israel imapiga ambush. Lakini kilichotokea masaa kadhaa tu baadae kiliiwacha mdomo wazi Dunia. Kwani Pamoja na maadui kutangaza kufunga anga, na kuweka maelfu ya mifumo ya kuzuia na kulinda anga kuanzia Saudi Arabia, Jordan na Israel kwenyewe, lkn bado mifumo hiyo iliendelea kufanywa chujio la nazi baada ya makombora hatari ya Iran kupenya mifumo hiyo bila kikwazo chochote, saa yoyote na eneo lolote.
Baada ya vita vya siku 12 huku Israel ikipokea kila aina ya silaha kutoka Marekani, UK, Ujerumani, Ufaransa, Italy, Belgium, Uholanzi nk. Netanyahu mwenyewe aliamua kuomba poo, baada ya maelfu ya waisrael wakiwemo mkewe na ndugu zake kukimbilia Poland katika nchi ya asili ya Benjamin Netanyahu.
Sasa vita iliisha huku waliovizia wakiwa hoi. Leo hii wanajipanga tena kwenda kupima upepo ambao bila shaka utageuka kimbunga chenye kusomba miti, nyumba, ndege, meli na magari.
Wakati Venezuela walienda kumchukua mtu bila kutumia risasi hata 1. Huku wanakwenda kushuhudia jinsi meli zao za kijeshi zinavyokwenda kuzamishwa majini kama karatasi bila huku mifumo yao ya kuzuia makombora ikiishia kuzuia nzi na vipepeo tu kama ilivyokuwa Israel siku ile.
Ogopa nchi ambayo pamoja na vikwazo vya miaka zaidi ya 50, lkn bado ni tishio kubwa kwa nchi zote zenye nguvu duniani kama vile Marekani, Israel, UK, Ufaransa nk.
Nchi ambayo, raisi wa Marekani (taifa lenye nguvu) fedha, teknolojia na intelejensia kubwa duniani (Trump) anaogopa itamuua.
Trump hakuwahi kuihofia Venezuela na nchi yoyote yenye uadui nao. Lakini kwa Iran ameonesha wasi wasi mkubwa juu ya maisha yake dhidi ya nchi hiyo.
So bila shaka Trump anasubiri ramadhani ndio aanze kuishambulia Iran, lkn nawahakikishia kuwa baada ya majibu ya Iran kuleta uharibifu mkubwa kwa jeshi, na vifaa vya Marekani. Trump ndo atakuwa mtu kwanza kuomba Iran ije mezani kufanya mazungumzo ya kusitisha vita kwa story ya kwamba Iran imekubaliana na baadhi ya masharti yake ili iondolewe vikwazo.
Mlale usingizi mnono.