Iran kununua ndege 100 kutoka Boeing

Iran kununua ndege 100 kutoka Boeing

thesym

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
3,864
Reaction score
4,847
140512180614_iran_air_640x360_airteamimages_nocredit.jpg

Mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Iran imetangaza kuwa itanunua ndege 100 kutoka kampuni ya uundaji ndege ya Boeing, nchini Marekani.

Mwezi Februari, Marekani iliipa idhini kampuni ya Boeing kuanzisha mazungumzo ya kibiasahara na Tehran, kufuatia kuondolewa japo kwa kiasi kidogo vikwazo vya kiuchumi, baada ya makubaliano ya kupunguza mpango wake wa kinuklia.

Iran inajikakamua kununua ndege mpya za kibiashara, kuchukua mahala pa ndege zake nzee ili kupanua sekta yake ya uchukuzi wa angani.

Mwezi Januari, Iran iliafikia makubaliano na Marekani kununua zaidi ya ndege 100 kutoka katika kampuni ya uundaji wa ndege barani Ulaya, ya Airbus.

Siku ya Alhamisi, mamlaka barani Ulaya iliamua kuondoa marufuku katika orodha yake ya uchukuzi wa angani ndege za Iran Air, iliyokuwa imewekwa hapo awali kwa sababu za kiusalama.

Note. Hawa jamaa wameamua wakati TZ miezi miwili imeshapita kukiwa hakuna ndege iliyowasili Kama ilivyoahidiwa.
 
Matusi yote kwa makafir wa Ulaya na Marekani leo wanarudi huko huko kununua bidhaa zao! Ama kweli unafiq ni zaidi ya uchawi. Na vibaraka wao humu jf sikiliza watakavyobadili kauli ili kuendana na mtazamo wa mabwana zao.

Aha ha ha! Halafu sikilizia Ayatullah na ujumbe/wasaidizi wake watakavyokuwa wamestarehe ndani ya Boeing ikiwapeleka hijja huku "matusi" yakimtoka (na juzuu zake mkononi) dhidi ya Marekani na Mazayuni bila kujali ndio watengenezaji wa mbawa za chombo kilichowabeba.

Kwa unafiq atajifanya kuifagilia Uchina bila kujua China ndio mzalishaji mkuu wa kiti moto duniani kwa zaidi ya 70%. Bila kujali China ndio mzalishaji mkuu wa "mvinyo" duniani kwa zaidi ya 65%.

Ukisikia baniani mbaya ila kiatu chake dawa ndio mambo kama haya. Hii dunia haiishi vituko hii.
 
afu tanzania inaenda kununua zile ndege mbovu za urusi wakati wairan maswahiba wakubwa wa urusi wanazikataa na kwenda kununua za mbaya wa urusi!
 
Tatizo lenu wengi wenu hamuijui Iran. Inanunua ndege hizo ili kuiba technologia hiyo ili nao waweze kutengeneza zao za aina hiyo
thubutuuu,walianza nunua china na wananunua mpk keshokutwa
 
MLETA MADA KUMBE WEWE NI 'KILAZA',MPANGO WA SERIKALI WA KUNUNUA NDEGE UKO KATIKA UTEKELEAJI UNAOANZA NA MWAKA MPYA WA FEDHA WA KISERIKALI,SO BAJETI ILIANISHA AINA YA NDEGE ZITAKAZO NUNULIWA ILI MWAKA WA FEDHGA UTAKAPOANZA KUTEKELEZWA ITENGWE PESA HIYO KWA AJILI YA KUNUNUA NDEGE,HILO MOJA.

lA PILI NI JUU YA HAO IRAN KUNUNUA NDEGE ZA ULAYA NA MAREKANI,JUA HAO NDIO WALIOIWEKEA IRANI VIKWAZO VYA KUCHUMI NA HAI NDIO WALIOLEGEZA VIKWAZO HIVYO KWA SABABU WALIZOAAINISHA,NA NINAUHAKIKA KUWA KUNA MASHARTI YA KIBIASHARA AMBAYO PANDE HIZO TATU WATAKUWA WAMEWEKEANA HASWA KATIKA KUZINUFAISHA PANDE MBILI KIUCHUMI ZAIDI YANI ULAYA NA MAREKANI NA KUNUNUA NDEGE NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI TU WA HUO MKATABA
 
Matusi yote kwa makafir wa Ulaya na Marekani leo wanarudi huko huko kununua bidhaa zao! Ama kweli unafiq ni zaidi ya uchawi. Na vibaraka wao humu jf sikiliza watakavyobadili kauli ili kuendana na mtazamo wa mabwana zao.

Aha ha ha! Halafu sikilizia Ayatullah na ujumbe/wasaidizi wake watakavyokuwa wamestarehe ndani ya Boeing ikiwapeleka hijja huku "matusi" yakimtoka (na juzuu zake mkononi) dhidi ya Marekani na Mazayuni bila kujali ndio watengenezaji wa mbawa za chombo kilichowabeba.

Kwa unafiq atajifanya kuifagilia Uchina bila kujua China ndio mzalishaji mkuu wa kiti moto duniani kwa zaidi ya 70%. Bila kujali China ndio mzalishaji mkuu wa "mvinyo" duniani kwa zaidi ya 65%.

Ukisikia baniani mbaya ila kiatu chake dawa ndio mambo kama haya. Hii dunia haiishi vituko hii.
Hao wanaonuzwa wanawatumikia wenye pesa,mwnye pesa(bwana),kanunua kwa mhudumu wake(mfanyakazi).Duniani kuna mwenye nazo na mwenye kutumwa na aliye nazo.
 
Tatizo lenu wengi wenu hamuijui Iran. Inanunua ndege hizo ili kuiba technologia hiyo ili nao waweze kutengeneza zao za aina hiyo
hahahaaa.....60+ years to come labda...mchina mwenyewe bado anajaribu kuiba tech za boeing ili nae aunde yake,kwani alishindwa kununua ili akaibe?..we unafkir blueprint za ndege zao un aweza kuzipata kirahisi ivo?
 
Matusi yote kwa makafir wa Ulaya na Marekani leo wanarudi huko huko kununua bidhaa zao! Ama kweli unafiq ni zaidi ya uchawi. Na vibaraka wao humu jf sikiliza watakavyobadili kauli ili kuendana na mtazamo wa mabwana zao.

Aha ha ha! Halafu sikilizia Ayatullah na ujumbe/wasaidizi wake watakavyokuwa wamestarehe ndani ya Boeing ikiwapeleka hijja huku "matusi" yakimtoka (na juzuu zake mkononi) dhidi ya Marekani na Mazayuni bila kujali ndio watengenezaji wa mbawa za chombo kilichowabeba.

Kwa unafiq atajifanya kuifagilia Uchina bila kujua China ndio mzalishaji mkuu wa kiti moto duniani kwa zaidi ya 70%. Bila kujali China ndio mzalishaji mkuu wa "mvinyo" duniani kwa zaidi ya 65%.

Ukisikia baniani mbaya ila kiatu chake dawa ndio mambo kama haya. Hii dunia haiishi vituko hii.
wewe ndio huelewi, jamaa wameondolewa vikwazo, sasa wananunua ndege kutoka marekani, hawakuwa wamekataa ila walikuwa na vikwazo vya uchumi, fatilia mgogora wa Iran na Marekani tangu enzi za Reagan au baada ya kupinduliwa Shah.
 
Sawa ila kwa matusi yale usingetegemea wangekaa wanunue bidhaa za west. Nakumbuka hata hapa wajinga fulani waliwaunga mkono eti nao wanasusia vitu vya Marekani. Kuna kipindi fulani waliandamana pale Biafra na maazimio yao eti ni kususia CocaCola na Colgate eti ni za kimarekani. Waliishia kunuka midomo tu wapuuzi wale.
 
ile scraper ya mrusi ilikuwa inasifiwa humu na mabongo lala iliishia wapi? iran kaikataa anachukua vyuma cha uhakika
 
Back
Top Bottom