BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,334
- 8,813
Watumishi wa Obama wamepatiamo sababu ya kuziponda Airbus na ndege za urussi..hahaa
Wabongo bana mwisho wa maneno aisee
Wabongo bana mwisho wa maneno aisee
Watumishi wa Obama wamepatiamo sababu ya kuziponda Airbus na ndege za urussi..hahaa
Wabongo bana mwisho wa maneno aisee
Naona mtumishi wa putin umeamua kuitaja airbus ili kuzipromote ndege za urusi!! airbus ziko vizuri ww. hapa duniani ni boeing na airbus, hizo za urusi hazisogelei hata bombardier za mcanada na comac za mchina
Lkn mtumishi wa obama kubali tu Airbus ni zaidi ya Boeing au sio?
Tatizo lenu wengi wenu hamuijui Iran. Inanunua ndege hizo ili kuiba technologia hiyo ili nao waweze kutengeneza zao za aina hiyo
Ha ha aliyekwambia ulaya hawaishi waislamu nani? Naona kama umpaniki brother hao waulaya wangekuwa na akili kama zako wasingeweza kutengeneza ndege na kuwauzia wairan.Matusi yote kwa makafir wa Ulaya na Marekani leo wanarudi huko huko kununua bidhaa zao! Ama kweli unafiq ni zaidi ya uchawi. Na vibaraka wao humu jf sikiliza watakavyobadili kauli ili kuendana na mtazamo wa mabwana zao.
Aha ha ha! Halafu sikilizia Ayatullah na ujumbe/wasaidizi wake watakavyokuwa wamestarehe ndani ya Boeing ikiwapeleka hijja huku "matusi" yakimtoka (na juzuu zake mkononi) dhidi ya Marekani na Mazayuni bila kujali ndio watengenezaji wa mbawa za chombo kilichowabeba.
Kwa unafiq atajifanya kuifagilia Uchina bila kujua China ndio mzalishaji mkuu wa kiti moto duniani kwa zaidi ya 70%. Bila kujali China ndio mzalishaji mkuu wa "mvinyo" duniani kwa zaidi ya 65%.
Ukisikia baniani mbaya ila kiatu chake dawa ndio mambo kama haya. Hii dunia haiishi vituko hii.
iran kagombana na utawala wa marekani,hajagombana na hizo ndege,Kuna jamaa wanajifanya hawajaiona hii thread! FaizaFoxy Ritz kahtaan Kansigo Lizaboni Simiyu Yetu THE BIG SHOW maatope et. al.
ulishasikia wairan wanasafiri kwa ungo hata siku moja?.Mbona hajaiba na kutengeneza ndege Mpya kwa zile za zamani alizonazo?hizo za zamani vipuri tuu vilimshinda kufanya reverse engineering mpaka akawa ananunua vipuri kwa kutumia makampuni fake ya Ulaya baada ya yale makampuni nayo kula vikwazo vya Marekani akaamu kuziweka chini ndege zake kwa sababu ya usalama wa Abiria.
Ha ha ha! Yale yale niliyotahadharisha! Vikaragosi watajitoa ufahamu in favour of their master's decision. Ila brother hii ya kwako kali - "wamegombana na Marekali ila sio na ndege za kimarekani ...". Sawa, ila unayakumbuka yale matusi ya Iran dhidi ya Marekani na Mazayuni? Iran anajua partly Boeing zinatengenezwa Israel? Au saa hizi anajifanya hamanzo ...iran kagombana na utawala wa marekani,hajagombana na hizo ndege,
...
russia alikua hajaamua tu kutengeza ndege za abiria,cheki kama ile Antonov ya mizigo unadhani marekani anaweza kutengeza kitu kama kile.?wewe kijakazi wa putin iwe airbus bora ama boeing ni sawa tu make zote zimetengenezwa na mataifa rafiki na yenye teknolojia ya juu. ila ile scraper ya boss wako putin hamna kitu
we husomi vyanzo vya habari vya iran nini.?Ha ha ha! Yale yale niliyotahadharisha! Vikaragosi watajitoa ufahamu in favour of their master's decision. Ila brother hii ya kwako kali - "wamegombana na Marekali ila sio na ndege za kimarekani ...". Sawa, ila unayakumbuka yale matusi ya Iran dhidi ya Marekani na Mazayuni? Iran anajua partly Boeing zinatengenezwa Israel? Au saa hizi anajifanya hamanzo ...
russia alikua hajaamua tu kutengeza ndege za abiria,cheki kama ile Antonov ya mizigo unadhani marekani anaweza kutengeza kitu kama kile.?
Cheki hata helcopter zao ni heavy duty,nimewai kuona helcopter ya mrusi ikiwa imebeba helcopter ya marekani chinook kama imebeba kikaratasi tu,wakati hiyo chinook kwa marekani ndo transport helcopter.
Wamarekani wakitaka heavy lifting wanachukua Antonov,sasa hapa huwezi kusema eti kwakua marekani hapatani na mrusi basi wasitumie bidhaa za mrusi
we husomi vyanzo vya habari vya iran nini.?
Matusi yako palepale,na pia matusi ya marekani kwa iran yako palepale,kuna vitu humu duniani vinafanyika kama akili yako nyepesi utabaki kushangaa tu.
Katika operation opera,wajua kuwa wairan waliwasaidia waisrael kuvishambulia vinu vya kinyuklia vya iraq miaka ya 80?
Unajua nini kuhusu iran-contra scandal?
Wamarekani walikuwa wakiwauzia iran silaha,
wamarekani bado wanatumia roketi za mrusi kwenda angani licha ya ugomvi wao na mrusi.
So kama unaakili sio nyingi unaweza baki unashaangaa tu.
Hizo tenda boeing na airbus walikuwa wanapigana vikumbo wazipate
Kabla ya mapinduzi ya Iran,IranAir ndiyo ilikuwa the fatest growing airline in the world.Baada ya vikwazo ,wameendelea kutumia ndege zilezile kwa muda wote huu thats why wanasema ndege zao sio salama lkn zimeanguka ngapi ? vikwazo vimeisha sasa ndo unaona jeuri yao tena ya kuagiza ndege 100 tena kubwa.Ktk bunge la bajeti mwaka jana , Waziri wa uchukuzi alitangaza kamba serikali itanunua Dash 8-Q400 mbili kwa ajili ya ATCL.Mpaka leo bado siku 8 kuisha mwaka wa fedha hakuna ndege ila manyoya tu.Na sasa tunaambiwa tena kwamba tunaagiza Dash 8-Q400 mbili na CS-300 moja lkn nina shaka manake orders za ndege duniani ni jambo la wazi kama tunavyoona la IranAir na hakuna lolote lililotangwa kuhusiana na ATCL ku peleka order.Kama tujuavyo order za ndege sio kama za magunia ya mchele.Ndege zinachukua muda kutengenezwa na ndo maana ukiagiza ndege leo waweza ipata 2018.
Namalizia kwa kusema warusi wame advance kwa sasa katika dunia ya passenge aircraft na mfano unaonekana kwa superjet 100 au Mc21
Mkuu nilishangaa juzi Waziri alipo sema tena kwamba wana mpango wa kununua Dash 8-Q400 - nikawa najiuliza maswali mengi:hivi huu mpango wa kununua jetliners kutoka Urusi ambazo ni roomy,more comfortable na kubeba abiria wengi mpango huo umekwama wapi tena? Mwishowe nikafikiri si ajabu alioata shinikizo kutoka kwa viongozi wenzake wenye colonial hangover kwamba ndege za Urusi si salama - of course huo ni uongo wa mchana - sasa Waziri mwenyewe kasoma Urusi na alikuwa ana safiri na ndege za Urusi za shirika la Aeroflot ambalo miaka ya nyuma lilikuwa linaongoza kuwa na ndege nyingi za abiria Duniani ni mara chache ndege hizo zilikuwa zinapata ajali ukilinganisha na Mataifa ya magharibi - je hilo Waziri kalisahau - kwa nini awaelimishi ma doubting Thomasis'.
Fedha za kununua ndege kutoka Canada tungenunua ngapi aina ya MC-21 kutoka Urusi, ndege nyingine ya kisasa kutoka Urusi ni Sukhoi Superjet 100 zinenunuliwa na nchi nyingi Duniani si hilo tu ndege yenyewe imehundwa kwa ushirikiano na nchi ya Italy.
Aeroflot wana maboeing na maAirbus ya kumwaga, hawaamizi ndege za nyumbani
Mkuu take your time kudigest kilicho andikwa nimesema hivi "MIAKA YA NYUMA URUSI NDIYO ILIKUWA INAONGOZA DUNIANI KUWA NA NDEGE NYINGI ZA ABIRIA ZILIZO HUNDWA NCHINI MWAO" kuna member mwingine kakumbusha kwamba siyo kwamba Warusi hawana uwezo/ujuzi wa kuhunda ndege za kubeba abaria, kilicho tokea ni kwamba Taifa hilo liliyumba kidogo baada ya Rais Gorbachev kufanya mahamuzi ya kijinga kwa kukubali USSR iwe in a loose ushirikiano baina ya former states specifically Baltic States, Ukraine na Georgia nia yake ilikuwa nzuri tu lakini mwisho wake ulikuwa kivingine kabisa, maadui wa Urusi wakatumia mwanya huo kurubuni viongozi wa nchi hizo kusambaratisha ushirikiano mdogo ulikuwa umebaki - hicho ndicho kilichotokea, kitendo hicho hakikuathili sana viwanda vya kuhunda ndege wala wataalamu na wahandisi wa kuhunda ndege wote hao bado wapo na viwanda vipo hisipokuwa vya Ukraine ambavyo vilikuwa vinahunda injini za helicopter - sasa baada ya Russian Federation kijipanga upya matokeo yake ndiyo haya hivi sasa wanakuja juu katika soko la ndege za abiria.
maneno mengii! kwa mantiki yako hata tanzania tunakuja juu make tayari tushatengeneza ya kwetu
Umeona eeeh anawatafutia BAN hao watuDuh unatafuta umaarafu kupitia migongo ya watu.