Iran kumbe ni moto wa kuotea mbali!

Iran kumbe ni moto wa kuotea mbali!

Risen man

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
20,005
Reaction score
54,085
IAEA yathibitisha mpango wa Iran wa kuzalisha uranium Shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limethibitisha mpango wa Iran wa kuzalisha uranium.

Mwakilishi wa nchi hiyo katika IAEA ameeleza kwamba mpango huo unalenga kuzalisha fueli ya aina mpya kwa ajili ya kinu cha nyuklia cha Tehran, na Iran imeripoti hatua zote husika kwa IAEA huku maofisa wa shirika hilo wametembelea kinu cha kuzalisha uranium mwezi huu.

Taarifa moja iliyotolewa na IAEA imesema Iran imeliarifu kuwa kazi yake ya utafiti wa nyuklia haitazuiliwa na kanuni yoyote.

Baada ya kupunguza ahadi kwenye makubaliano juu ya suala la nyuklia la Iran mwezi Januari mwaka jana, Iran ilitangaza kuwa utafiti wa nyuklia hautazuiliwa na utafanyika kwa mujibu wa mahitaji ya nchi hiyo.

Na habari nyingine zimesema hivi karibuni Kikosi cha wanajeshi wa baharini cha Iran kimefanya mazoezi ya kijeshi na kuonyesha meli mbili mpya za kivita.

Moja inayoitwa Makran yenye urefu wa mita 228 inaweza kubeba helikopta 5 na vifaa vya tani 82,000 na kuendeshwa kwa siku 1000 bila ya kutia nanga.

Na meli nyingine ya kivita ambayo ilionekana katika mazoezi hayo ni Zereh, yenye urefu wa mita 47, inaweza kurusha makombora kutoka kwenye meli yenye masafa ya kilomita 300.

FB_IMG_16107282120028325.jpg
 
Iran inachekesha inaunda meli wakati wanawake wao hawana taulo za kike pedi kujisitiri
Kwani hata huko Marekani na Ulaya wanatengeneza hayo mazaga yao kwani watu wasio na makazi hawapo? Wananchi wao wote wanajiweza wanapata kila kitu?
 
Iran iko vizuri lakini haijafikia level ya kupambana na Marekani kama ilivyo Korea Kaskazini
 
Iran iko vizuri lakini haijafikia level ya kupambana na Marekani kama ilivyo Korea Kaskazini
Hhhhhhhhh: kama hujui mkosoaji mkubwa wa Marekani ni Irani na ndio tishio dunia nzima ndio sababu ya kumbana bana iri asizidi kuwa tishio .pale wananyenyekea wamarekani ya VIKWAZO vyote walivyo weka imekua kazi bure hhhhhhh WAAJEMI NDIO WAKALE NA WALIWATANGULIA KUONA JUA: HAWA WALIKUA HATARI SANA FUATILIA HISTORIA YA AJEMII ATA KWA BIBLIA UTAWAKUTA MZEEE
 
Iran inachekesha inaunda meli wakati wanawake wao hawana taulo za kike pedi kujisitiri
Kwa hii habari yako unajiona uko sawa kweli?
Ulishawahi kusikia Iran anaomba msaada zaidi ya kutoa msaada?

Achana na habari za mrengo wa kushoto za mabeberu brother
 
Back
Top Bottom