Iran: ‘Kisasi cha Mungu’ kitakumba Saudia

Iran: ‘Kisasi cha Mungu’ kitakumba Saudia

Status
Not open for further replies.
Mfumo kristo kumbe una nguvu sana, unawagombanisha hadi makazeni wa Mwamedi?
 
Tatizo lao ni maslahi ya uchumi. Wafalme wa saudia sio maimamu wala masheikh.wala si. Wahubiri msikitini.wao ni viongozi wa kisiasa na serikali.
Saudi ni taifa la massuni wengi na wanafata sharia.
Maimamu wao hawana maamuzi yoyote kwa serikaliya saudia.mfumo wa dini unajiendesha wenyewe kupitia shura zao .

Iran ni taifa la kishia. Wao kiongozi wao mkuu ni Ayatolllah, kunakua na serikali yakuchaguliwa lakini maamuzi ya mwisho anayo Ayatollah ambaye ndie kiongozi wa majeshi

Hio ndio tofauti ya hawa.
Sera ya khomein ni kueneza ushia sehemu za massuni....sio kuuneza uislam ambako hakuna waislam. Sera hii ni ya uchokozi.
Sera ya pili ni kuanzisha wanamgambo wa kijeshi sehemu za masuni . Walifanikiwa kuanzisha Hizbollah ambayo inajidai ni chama cha siasa lakini ikaanzisha jeshi nje ya mfumo wa nchi ya Lebanon. Hawa wamekua wakifata kila kitu wanachoambiwa na iran.
Wamesababisha lebanon kushambuliwa na Israel mara kadhaa.
Wameingilia siasa za Syria.
Mfano wa hizbollah ndio sera ya Khomeni ndani ya nchi za kisuni..hivyo chokochoko hizi zipo Bahrain, pakistan , afganistan, na Walitaka kuijaribu Saudia.
Kule pemba waliwahi kutimuliwa baada kukaribishwa kusaidia. Wameingilia sana masikini kule Tandika kwa kuwashawishi kwa fedha waislam wa kissuni... Ni wachokozi..na ukiwachia ndo ujue watakuletea Hizbollah ndani ya nchi yako na kuleta fitina kama Hizboolah walivo muua Rafik Hariri..waziri mkuu wa Lebanon...
Walianza kumtumia puppet Nimr kuleta fitina , ni uhaini raia kuwa jasusi wa nchi nyengine....na nchi nyingi adhabu yake ni kifo....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom