Iran Inatisha Mpeni Pole Israel

Iran Inatisha Mpeni Pole Israel

Adiosamigo

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
10,614
Reaction score
13,997
Iran wamekuja na technology mpya ya Missiles hukioni kichwa we utaishia kudaka target sio orignal hio hio Missile moja inaonyesha kama ina vichwa vingi hivyo Air defense zitakuwa zinafata hizo fake target kumbe kichwa orignal kina kwenda kwenye target



View: https://youtube.com/shorts/r1STIIPZgGg?si=GNVle_PDTZsm8iHI

View: https://youtube.com/shorts/Z-DahHbxau4?si=PKNkFUKvi3Zc_2qC



View: https://youtu.be/cGFRcM_T-bI?si=co1-KRx_92TXAULd

Kheee kwamba ili ni jambo geni!??
😆😆😆😆
Wafuga majini wa mtogole mna chekesha sana
 
Kheee kwamba ili ni jambo geni!??
😆😆😆😆
Wafuga majini wa mtogole mna chekesha sana
We baki na ujinga wako hio Missile moja itameza. abda defense.missiles karibu 50 na hipati target yenyewe inapenya kwa kutumia joto baridi mpaa kwenye target, nyie mtakuwa mnalenga joto la moto.
 
Sema haya maisha bana.Huwezi amini kabla ya Ayatolah hajafanya mapinduzi Iran in 1970's.Israel ma Iran walikua marafiki wakubwa, Israel alikua anansaidia Iran kutengeneza na kumuuzia makombora, na hapo tu Israel alikua anamsaidia Iran kutengeneza mitambo ya nuclear kwa ajili ya matumizi ya kiraia, yaani walikua mtu na mtu wake.
Islamic Revulution 1979 ikaleta watu matatizo leo hii ni maadui wa kufa mtu..
 
Maneno hayabadilishi uhalisia.

Hapo zamani tuliambiwa, kamwe Israel haiwezi kuishambulia Iran, na kwamba ikithubutu kuishambulia, ndiyo utakuwa mwisho wa Israel. Kinyume chake, Israel ikaishambulia Iran, ikapiga kila ilipotaka. Aliyetajwa kuwa ni mbabe, Iran, ikaishia kurusha makombora hovyo, yakawaua waisrael 28, wote wakiwa raia, isipokuwa askari mmoja aliyekuwa likizo. Lakini mbabe huyo fake Iran, ikapoteza watu 1,190, na majeruhi 4,475 huku vifo karibia 600, vikiwa ni makamanda wa jeshi na wanasayansi wa nuclear.

Mwisho wa yote Iran akaamua kuwabembeleza wakuu wa Ulaya, waongee na Trump, ili vita ikome. Mbabe bandia Iran, akasema kutokana na vita hiyo, amesitisha ushirikiano na tume ya UN ya nuclear, lakini tishio dogo tu toka Israel kuwa kama Iran itarudi kurutubisha nuclear energy, kwa vile hakuna watazamaji, yenyewe itaitwanga tena Iran, mbabe fake amesalimu amri na kuahidi kutoa ushirikiano kwa tume ya UN ya nuclear.

Waarabu, kama maneno yao yangekuwa ndiyo vitendo, basi Israel isingekuwepo Duniani.
 
Back
Top Bottom