Iran: Hatuna Chaguo ila Kutumia Silaha za Nyuklia

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Iran imesema haitakuwa na njia nyingine ila kutumia silaha za nyuklia endapo itashambuliwa na Marekani au
Ali Larijani, Mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, amesema kwenye mahojiano na televisheni ya taifa la Iran kwamba "hawaelekei kwenye kuunda silaha za nyuklia, lakini ikiwa Marekani itafanya makosa katika swala hilo basi Iran italazimika kuelekea kwenye mkondo huo kwa sababu inapaswa kujilinda."

Kauli hii ameitoa saa chache baada ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei, kuahidi kuijibu Marekani endapo Trump atatimiza tishio lake la kulishambulia taifa hilo la Kiislamu.

Larijani amesisitiza kauli hiyo ya Kiongozi Mkuu kwamba Iran italazimika kuchukua hatua tofauti iwapo Marekani itaishambulia nchi yake kwa mabomu au kupitia kwa Israel.

"Tumesema kuna amri ya kidini inayokataza kutengeneza silaha za nyuklia, tunatoa ushirikiano kwa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) na hivyo hatupangi kujielekeza kwenye silaha ya nyuklia, lakini Marekani ikifanya makosa kuhusiana na suala la nyuklia la Iran, itatulazimisha kufuata njia hiyo, kwa sababu Iran inapaswa kujilinda."

Katika mahojiano siku ya Jumamosi, Trump alisema "yatafanyika mashambulizi ya mabomu" ikiwa Iran haitakubali kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Kulingana na shirika la habari la NBC, Trump pia alitishia kuiadhibu Iran kwa kuiwekea vikwazo vya ushuru".

Iran: Tishio la Trump ni dharau kwa mataifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei, amesema kupitia chapisho kwenye mtandao wa X, kwamba tishio hilo linaashiria "kudharau amani na usalama wa kimataifa, ambalo ni jambo la kushangaza".
washirika wake. Hayo ni kufutia kitisho chj rais wa Marekani Donald Trump aliyesrma ataishambulia Iran kijeshi.

Ameonya juu ya "matokeo" ambayo hayajabainishwa iwapo Merekani itachagua njia ya "vurugu".

Wizara ya mambo ya nje ya Iran pia iliitisha kikao na ubalozi wa Uswizi, ambao unawakilisha maslahi ya Marekani nchini Iran hapo jana Jumatatu, kupinga vitisho vya rais Donaldtrump. Marekani ina kambi 10 katika eneo karibu na Iran, na jumla ya wanajeshi 50,000.

Tangu aingie madarakani mwezi Januari, Trump amerejesha sera yake ya kushinikiza, ambayo katika muhula wake wa kwanza aliiondoa Marekani kutoka kwenye makubaliano ya kihistoria kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na akaiwekea tena vikwaz nchi hiyo.
 
Iran itakachofanya ikishambuliwa itatupa nyuklia yake israel halafu nayo itageuzwa majivu, bora isitumie nyukilia inyukane kwa silaha za kawaida. Itakuwa tupa nikutupie, yenyewe ndiyo itachakazwa na kuchakaa chakari
 
Mnadhani ni rahisi hivyo. Kwa roho mbaya ya Iran angekuwa na nukes hata Leo angerusha pale Tel Aviv
 
Haya sasa wale wa "I voted for Trump because he is anti-war".
Trump ni mwehu na wafuasi wake ni wehu kama yeye nilisema kabla hajawa Rais nasema sasa akiwa Rais na nitaendelea kusema hata asipokuwa Rais.

Moja ya madhaifu ya mfumo mzima wa kidemokrasia ni kuwa hata vichaa wana sauti na maamuzi ya kuchagua kichaa mwenzao kuwaongoza.
 
Mwenye roho mbaya ni iran au israle .. iran ni nchi yenye utu sana wanapinga mauji ya utakaso wa kikabila ila west wote wanaunga
Nenda kwenye root....usichimbue juu juu..
Kwani yeye angekaza fuvu nini kingemgharimu?
Yaani unawatetea watu ambao ndugu zao wa damu hawawasaidii..mbona waarabu wenzao wapalestina wameufyata?
 
Trump ni mwehu na wafuasi wake ni wehu kama yeye nilisema kabla hajawa Rais nasema sasa akiwa Rais na nitaendelea kusema hata asipokuwa Rais.

Moja ya madhaifu ya mfumo mzima wa kidemokrasia ni kuwa hata vichaa wana sauti na maamuzi ya kuchagua kichaa mwenzao kuwaongoza.
Ni sababu moja tu, kawatimua wabeba box, mnahasira utadhani mmezaliwa huko

Tengenezeni uchumi wa ncho zenu

Kwa akili yako, unataka Trump awe mzuri kwako wewe unayekaa matabe huko?

Trump ni Raisi wa watu wa Marekani na si vinginevyo
 
Iran itakachofanya ikishambuliwa itatupa nyuklia yake israel halafu nayo itageuzwa majivu, bora isitumie nyukilia inyukane kwa silaha za kawaida. Itakuwa tupa nikutupie, yenyewe ndiyo itachakazwa na kuchakaa chakari
usipangie watu cha kufanya,sio israeli tu itakayoangamizwa na Iran,kaa hapo kwa kutulia,Iran sio Unguja
 
Iran imesema haitakuwa na njia nyingine ila kutumia silaha za nyuklia endapo itashambuliwa na Marekani au
Ali Larijani, Mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, amesema kwenye mahojiano na televisheni ya taifa la Iran kwamba "hawaelekei kwenye kuunda silaha za nyuklia, lakini ikiwa Marekani itafanya makosa katika swala hilo basi Iran italazimika kuelekea kwenye mkondo huo kwa sababu inapaswa kujilinda."

Kauli hii ameitoa saa chache baada ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei, kuahidi kuijibu Marekani endapo Trump atatimiza tishio lake la kulishambulia taifa hilo la Kiislamu.

Larijani amesisitiza kauli hiyo ya Kiongozi Mkuu kwamba Iran italazimika kuchukua hatua tofauti iwapo Marekani itaishambulia nchi yake kwa mabomu au kupitia kwa Israel.

"Tumesema kuna amri ya kidini inayokataza kutengeneza silaha za nyuklia, tunatoa ushirikiano kwa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) na hivyo hatupangi kujielekeza kwenye silaha ya nyuklia, lakini Marekani ikifanya makosa kuhusiana na suala la nyuklia la Iran, itatulazimisha kufuata njia hiyo, kwa sababu Iran inapaswa kujilinda."

Katika mahojiano siku ya Jumamosi, Trump alisema "yatafanyika mashambulizi ya mabomu" ikiwa Iran haitakubali kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Kulingana na shirika la habari la NBC, Trump pia alitishia kuiadhibu Iran kwa kuiwekea vikwazo vya ushuru".

Iran: Tishio la Trump ni dharau kwa mataifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei, amesema kupitia chapisho kwenye mtandao wa X, kwamba tishio hilo linaashiria "kudharau amani na usalama wa kimataifa, ambalo ni jambo la kushangaza".
washirika wake. Hayo ni kufutia kitisho chj rais wa Marekani Donald Trump aliyesrma ataishambulia Iran kijeshi.

Ameonya juu ya "matokeo" ambayo hayajabainishwa iwapo Merekani itachagua njia ya "vurugu".

Wizara ya mambo ya nje ya Iran pia iliitisha kikao na ubalozi wa Uswizi, ambao unawakilisha maslahi ya Marekani nchini Iran hapo jana Jumatatu, kupinga vitisho vya rais Donaldtrump. Marekani ina kambi 10 katika eneo karibu na Iran, na jumla ya wanajeshi 50,000.

Tangu aingie madarakani mwezi Januari, Trump amerejesha sera yake ya kushinikiza, ambayo katika muhula wake wa kwanza aliiondoa Marekani kutoka kwenye makubaliano ya kihistoria kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na akaiwekea tena vikwaz nchi hiyo.
Trump namuona kama mtoto kautaka,apatiwe mshedede atulie
 
Na sisi Tanzania tukishambuliwa na Burundi tutayatuma makomando wetu ambao hupasua matofali kwenye maonesho ya taifa
 
Vita nzuri jamani, mnaona sasa middle East hakuna anataka kupigana na Israel. Unapigana kiume unapigwa kiume unaleta heshima kwa aliyekupiga.

HAMAS walikuwa na moto sana, sasa naona wameanza kudebweda. Lakini ndivyo ilivyo lazima mshindi apatikane.

Nasubiri pale juu Ukraine na Russia watamaliza vipi ligi.
 
Hii dunia ni ya ajabu sana! USA ana Nuclear, Russia ana Nuclear, Israel ina Nuclear, nchi za ulaya zina nuclear ila Iran hatakiwi kuwa na Nuclear..

Anachotakiwa kufanya Iran ni kutest Nuclear kama alivyofanya North Korea tu basi.. vinginevyo watamsumbua sana
 
Yaani dini inazuia alafu hapo hapo watalazimika kuzitumia. Kweli shetani ana nguvu kwenye moiyo ya baadhi ya watu mpaka mtu aache agizo la Mungu.
 
Back
Top Bottom