IPTL/PAP: Hatuna kesi na TANESCO

wakuu! mnanikumbuka lkn? naomba hii kazi muiacche Mara moja nitawalipua mmoja baada ya mwingine achaneni na huu upuuzi wa kutetea wezi wa rasilimali zetu ni hayo tu ila kama hamtaacha nitakuja hapa JF kuueleza umma wa watanzania juu ya kutumika kwenu
eeeehhhheee !!!!!! kweli mambo magumu kafulila kaamua aje mwenye haya karibu
Anza sasa kutuongopea tunakusubiri
 
ahahaaaaa!!!!!!!!!!! wachaaa wewe !!! wewe kumbe unasubiri maandamo wenzako tupo landmark tushaandamana
 
Unajitekenya mwenyewe alafu Unajichekesha mwenyewe!..Tutolee ----- wako.Mtu akifilisika hoja utaona tu,We umeona wapi watu wanamtetea mtuhumiwa JF???Basi mahakama ihamie JF. Hii ni mijadala tu bwana Kafulila.Tunajua Ubunge ndo hvo supu umeitia nazi, unatafuta kick kwa kudanganya Watanzania,na pesa ya ku survive..Hakika wewe ni Katumbili :rip:
 
Kafulila siku zote hanaga uvumilivu ndo maana huko nyuma aliwahi kuitwa sisimizi mara tumbili.... Yaweza kuwa wanamjua vizuri huyu jamaa, sasa jasho lazima limtoke kwa ujinga wake na tamaa zake.
 
wakuu! mnanikumbuka lkn? naomba hii kazi muiacche Mara moja nitawalipua mmoja baada ya mwingine achaneni na huu upuuzi wa kutetea wezi wa rasilimali zetu ni hayo tu ila kama hamtaacha nitakuja hapa JF kuueleza umma wa watanzania juu ya kutumika kwenu

Acha upuuzi wako ndugu,wewe mtu mzima sasa,nenda kawalipue kwanza wanaokulisha sio kuvamia watu usiowajua, na bado tutaheshimiana mwaka huu
 
Kafulila amefeli kutofautisha Kampuni ya IPTL iliyotokana na Muungano wa kampuni ya Mechmar (Malaysia) Berhard (70%) na VIP(30%), na kampuni ya PAP/IPTL iliyoundwa baada ya kununuliwa kampuni kwa kampuni hizo hapo juu,hivyo kitendo cha kuzungumzia utendaji kazi wa kampuni ya IPTL(CHINI YA PAP) kwa kuihusisha na kampuni ya IPTL chini ya Mechmar na VIP ni kuionea PAP na kuikosea kampuni hii ya PAP/IPTL.
 
Kweli hatuna haja ya kubishana na mtu asiejielewa nini anachotaka

Hapana kafulila hajafeli kutofautisha kati ya hayo makampuni, anajua fika kila kitu shida ni kuwa ameamua kwa makusudi kuchafua taswira ya IPTL baada ya PAP/IPTL kukataa kumpa fedha aliyoiomba kwao eti ili afunge mdomo,sasa kinachofuata IPTL wameamua sharia itawale wamempeleka mahakamani na watapeleka ushahidi wa jinsi alivyoomba fedha ili anyamaze, na bilioni 300 atawalipa IPTL, ILI LIWE FUNZO KWA WABUNGE WENYE UCHU WA FEDHA ZA HARAKA HARAKA..
 
hata hivyo sio mbaya kuweka ushahidi wa raia mwema mkuu, we kama unao weka
 
kweli kabisa
 
kwani mimba yako wewe ilitungwa kupitia tigo au?
 
Huna mamlaka yoyote hapa hivyo kaa kimya. Tangu nianze kupost hapa miaka 7 iliyopita hata wamiliki wa JF hawajawahi kuniambi nini cha kupost au kutopost.

hata hivyo sio mbaya kuweka ushahidi wa raia mwema mkuu, we kama unao weka
 
IPTL/PAP YAMVAA KAFULILA, YASEMA ANATUMIKA VIBAYA
· YAMWITA MUONGO NA AACHE KUWEWESEKA

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP), ambayo ni mmiliki halali wa kampuni ya
IPTL imempuuza, kumshangaa na kumdharau mbunge wa Kigoma Kusini-NCCR Mageuzi, David Kafulila kwa
taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Oktoba 5, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu na Mshauri wa sheria IPTL/PAP, Joseph Makandege imesema
Kafulila anaweweseka na hii inatokana na umma kushindwa kukielewa anachokisimamia ndio maana
analazimisha masuala ya uongouongo yaaminiwe na umma.

Makandege alisema Kafulila anajua fika kwamba IPTL ni mali ya PAP, baada ya VIP na MECHMAR kuuza hisa
zao kwa PAP na hili jambo sio siri na limeripotiwa katika vyombo vyote vya habari Tanzania anaweza
akarejea taarifa ya aliyekuwa mmiliki wa VIP, James Rugemalira aliyeitoa Agosti 29, 2013.

Katika taarifa ya Rugemalira, Makandege alisema mmiliki huyo wa VIP alieleza namna ya mchakato wa
manunuzi ulivyokwenda baina ya PAP na VIP, hivyo Kafulila aache kuota ndoto za alinacha kwa kuwa kila
mwenye akili timamu anafahamu kwamba IPTL/PAP inauzia umeme TANESCO tangu mwaka 2002 na mwaka 2006,

VIP na MECHMAR iliingia katika mgogoro wa kimaslahi na kupelekea kusainiwa kwa makubaliano ya kisheria
ya ESCROW na hatimaye na kufunguliwa kwa akaunti ya ESCROW, ambayo BoT alikuwa wakala wa ESCROW na si
mmiliki wa fedha za ESCROW.

"Kafulila amefulia, hivi jiulize ukiwa wakala wa M Pesa au TIGO, unakuwa mmiliki wa M PESA au TIGO
PESA hiyo, Kwa hiyo BoT alikuwa wakala wa fedha za ESCROW na sio mmiliko wa fedha za ESCROW,''ilisema
taarifa hiyo.

Makandege alisema Kafulila anafahamu fika kuanzia tangu kusaniwa kwa makubaliano ya ESCROW Julai 5,
2006, TANESCO walikuwa wanaendelea kupatiwa umeme kila siku, kwa kiasi kilekile wanachokihitaji wao mpaka leo hii na anajua kwamba, TANESCO walikuwa hawailipi IPTL na badala yake fedha walikuwa wanaziweka katika akaunti ya ESCROW, Je Kafulila alitaka tuwape umeme bure TANESCO. Je yeye anapofanya kazi bungeni halipwi?, Anapokaa katika vikao vyake hapewi posho au wanaomtuma kueneza uongo
hawamlipi?. Kafulile aache kutumika vibaya.

"Dunia nzima inafahamu sasa kwamba PAP/IPTL imepewa dhamana ya kuzalisha megawati 2000 nchini Kenya na
hilo inathibitika katika barua kutoka serikali ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge Agosti 19, 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.,''ilisema.

Taarifa hiyo, ilieleza barua ya Kenya kumtaka Singasinga Seth azalishe umeme Kenya ilikuwa ina kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari ''Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania''.

Makandege alisema Kafulila anaposema Singasinga Seth haruhusiwi kufanya biashara Kenya, wakati Singasinga huyo huyo, ameshapewa kibali cha kuzalisha umeme na kuuza Kenya ikiwa ni mara 20 zaidi anayozalisha Tanzania, Hivyo ni kichaa pekee anayeweza kuamini upuuzi huu wa Kafulila.

''Tunapenda kuwasisitizia watanzania waendelee kumpuuza mtu huyu kwani kwa sasa amevurugwa ndio maana anahamishahamisha mijadala na kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri huku akijua ESCROW ni jambo la kisheria na si la kisiasa na yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya ESCROW hata kwa njia ya mtandao

ili siku nyingine asiendelee kulishwa ujinga wa namna hii bila kujua ukweli wa ndani kufanya hivyo ni kufedhehesha watanzania kwamba wanawachagua wabunge wenye uelewa mdogo kama Kafulila''. ilisema taarifa hiyo.

Ilisema uelewa finyu huu wa Kafulila unamsababisha ashindwe kutofautisha kati ya mali ya umma na mali binafsi, fedha za umma zilizopo BoT na uwakala wa ESCROW wa BoT, kazi za serikali na kazi za mbunge kazi za IPTL/PAP na kazi za TANESCO tunasisitiza IPTL/PAP sio shirika la Umma wala mali ya serikali,

Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.

Hivyo, tunawahakikishia watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh. 80 uko mbioni kukamilika ili watanzania wafurahie huduma ya umeme na wachagize maendeleo yao japo kina Kafulila na wapinzani wetu wa kibiashara hawapendi watanzania wafaidi matunda yao.
 
usipanic mkuu mbona hilo suala halihitaji kuzungumza kwa kutumia nguvu nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…