maherishalalhashbaz
Member
- Jul 28, 2014
- 9
- 1
Mungu saidia maana Tz walugaluga sana.
Tujikumbushe!
View attachment 196306
Mshauri wa Biashara wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya VIP, James Rugemarila (katikati) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya IPTL akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam kuhusiana na Kampuni ya VIP kumaliza mgogoro uliokuwepo kati ya VIP na IPTL uliodumu kwa muda mrefu. (Kushoto kwake) ni Mkurugenzi Mteule wa VIP, Benedictor Rugemarila. (Wa kwanza kushoto) ni Mshauri wa Masuala ya Usalama wa kampuni hiyo, Kamala Stephen aliyehudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari.
Kampuni ya VIP imemaliza mgogoro wa muda mrefu uliokuwa baina yake na Kampuni ya IPTL katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam tangu Februari 25,2002.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mshauri wa Biashara wa Kimataifa wa Kujitegemeawa wa VIP, James Rugemarila ambaye pia ni Mkurugenzi wa IPTL, alisema kuwa mgogoro huo ulidumu kwa muda mrefu na kuwagharimu fedha nyingi.
Aliongeza kuwa mgogoro huo ulikuwa na tafsiri mbalimbali na
kwa kuwa ulikuwa mahakamani walishindwa kutoa taarifa kwa jamii kuhofia kuingilia uhuru wa mahakama.
Rugemarila alisema kwa kuwa umeisha wameamua kuweka kila kitu wazi ili jamii ielewe na taarifa hizi zitatangazwa kwenye magazeti ya Jambo Leo, The African, Daily
News, Guardian, blogus, Channel Ten, ITV nk.
Akizungumzia zaidi kuhusu Kampuni ya Pan Africa Power Sulutions Tanzani LMT, iliyonunua hisa za VIP kwenye IPTL na kupewa kibali na VIP kuhalalisha ununuzi wa shea za Mechmar katika IPTL, alisema itawakomboa wananchi kwa kupata nishati hiyo kwa bei nafuu.
Aliongeza kuwa katika muda mfupi baada ya kampuni hiyo kuanza kazi itazalisha megawati 500 kwa bei kati ya uscents 6 na uscent 8 kwa kila unit ukilinganisha na bei za sasa zinazotozwa na makampuni ya kuzalisha umeme zilizo kati ya uscent 33 na 55 uscen kwa unit moja.
Hii ni kampuni ya Kitanzania, ambayo ni bahati mbaya tu huyu Mkurugenzi wa PAP, Dr. Harbinder Singh Sethi amefiwa na jamaa yake ndiyo maana hayupo tutamleta mtamuona atakuja Jumatatu mtawasiliana naye, inaonesha Watanzania tunaweza, alisema Rugemarila
Kutokana na hukumu ya Mahakama Kuu, Kampuni ya PAP ilijadiliana na wadai halali wa mikopo ya IPTL na kuingia Mkataba wa kuwalipa wadai wote wa IPTL isipokuwa SCB-HK ambaye hakuwasilisha madai yake.
SCB-HK iliyokuwa ikiidai IPTL fedha ilizotumia kununua deni lililotokana na kufilisiwa kwa MECHMAR kule Malaysia (siyo Tanzania) haijawahi kujadiliana na IPTL kuhusu malipo ya mkopo wake kama upo. Mvutano huu unaendelea ICSID kati ya TANESCO na SCB HK, ukiitaka TANESCO ilipe gharama za kununua umeme ikijumuisha deni la IPTL. Madai ya SCB HK dhidi ya TANESCO yanatokana na madai ya kuwepo kwa deed of Assignment ya MECHMAR kuhusiana na Mkopo wa IPTL ambapo Mtambo wa IPTL uliwekwa kama dhamana ya mkopo. Hata hivyo deed of assignment hiyo haikuwahi kusajiliwa hapa nchini kama inavyotakiwa katika kifungu Na. 172 cha sheria za makampuni Cap. 212 zinavyoelekeza Kwa kutokusajili assignment deed hiyo, SCB HK ilikosa sifa ya kufungua madai yake hapa nchini badala yake ilifungua madai haya ICSID nchini Uingereza kama ilivyoelezwa kwenye kifungu Na. 2.8.2 cha taarifa hii, kitu kinachoonyesha kudharau Mahakama zetu
TANESCO pia ilitoa hoja kwamba Mahakama ya Usuluhishi haina mamlaka ya kusikiliza mgogoro huo kwa vile SCB-HK haikuomba ruhusa ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuwasilisha shauri hilo kwenye Mahakama ya Usuluhishi kwa kuwa haikuandikisha mkopo huo hapa nchini kama inavyotakiwa katika kifungu Na. 172 cha Sheria ya Makampuni Cap 212. Pamoja na TANESCO kuweka pingamizi hili, wakili wake Mkono & Co Advocates hakuitetea hoja hii wakati wa kesi katika ICSID;
Wakati kesi ikiendelea ICSID Mahakama Kuu ya Tanzania iliiondoa kampuni ya IPTL katika ufilisi, TANESCO walimuomba wakili kuwasilisha taarifa ICSID ya IPTL kuondolewa katika ufilisi ili SCB HK iondoe kesi hiyo mahakamani na kuwasilisha madai yake kwa IPTL, kampuni ambayo sasa ni hai (Solvent) kulingana na uamuzi wa Mahakama Kuu. Mawakili wa TANESCO Mkono & Co Advocates, hawakuwasilisha ombi hilo ICSID na kuifanya ICSID iendelee na kesi hiyo hadi ilipotoa uamuzi tarehe 12 Februari, 2014
ICSID katika uamuzi wake ilielekeza SCB HK na TANESCO wakubaliane kuhusu namna ya kukokotoa tariff ndani ya muda wa miezi mitatu na kuwasilisha makubaliano yao ICSID. Mawakili wa TANESCO hawakuonesha dalili yoyote ya kutoridhishwa na uamuzi huo, badala yake walisisitiza kuishauri Serikali na TANESCO itekeleze maelekezo hayo ya ICSID huku wakijua kuwa SCB HK na TANESCO hawana uhusiano wowote wa kimkataba.
Kafulila Hatuwezi kuwalipa SCB-HK kama unavyotaka wewe, Tanzania haijawahi kuingia mkataba na SCB-HK
View attachment 195834
tumemquote hapo alipokuwa akiongea na mwandishi wa Raia mwema.
Watu hamfanyi kazi kwa bidii, ustaadi na uadilifu, msimamie rasilimali mlizopewa na huyo Mungu, mnaomba miujiza ya Mungu kuwezesha umeme ushuke bei, yaani Mungu awezeshe umeme ushuke bei kwa watu wanaolala nyumbani kuanzia asubuhi mpaka jioni, kwa watu wasiosimamia rasilimali vizuri, kwa watu wasiochukua tahadhari bali wanamwomba Mungu ugonjwa wa Ebola usiingie nchini mwao, wanamwomba Mungu alete mvua badala ya kujenga mabwawa ya kuvuna maji, Eeee Mungu una kazi sana. Haya omba Mungu akujengee nyumba na akusomeshee watoto wako.
Kwelo ccm inajua jinsi ya kitega mitego yake ili ipate kura zetu! Hii yote ni njia za kutafuta point za kusimamia pindi muda wa kampeni utakapokuwa umewadia kwa kigezo kuwa waonewe huruma ya kubaki madarakani ili wakamilishe ndoto zao! Kuwa macho sana nao.
Kwelo ccm inajua jinsi ya kitega mitego yake ili ipate kura zetu! Hii yote ni njia za kutafuta point za kusimamia pindi muda wa kampeni utakapokuwa umewadia kwa kigezo kuwa waonewe huruma ya kubaki madarakani ili wakamilishe ndoto zao! Kuwa macho sana nao.
kwani vibaya mkuu?
ndio, ni vibaya Mkuu, kwa sababu tayari waliotangulia wakati dunia inaumbwa walimwomba Mungu akawasikia na kutuweka kwenye nchi yenye rasilimali nyingi, kwa hiyo tunachopaswa kufanya ni kumwomba Mungu atujalie afya ili tuweze kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo, lakini sio kuendelea kumsumbua Mungu atuletea maendeleo ilihali tunashinda vijiweni na kuwafuata wanasiasa kwa maslahi yao binafsi.
sasa hawaogopi hasara?na walikuwa wapi siku zote mpaka wasubiri uchaguzi?
Hizo mbwembwe za uchaguzi 2015,afadhali mturudishie fedha zetu mlizotuibia kupitia tegeta escrow account na richmond.
Hivi ni kweli unaendelea kuamini kelele za kafulila? naomba nikukumbushe yafuatayo;
Kafulila alisema Seth ambaye ni mwenyekiti mtendaji wa PAP/IPTL ni fisadi na kwamba serikali ya Kenya imempiga marufuku kuwekeza nchini humo. Jibu lake likawa hili;
KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kungaa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.
Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.
Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.
Katika mwendelezo wa porojo zake akaja na la Prof. Tibaijuka, akimta Mkurugenzi wa PCCB Dr. Hosea amkamate na kumshitaki Prof. Tibaijuka kwa kuhongwa pesa za akaunti ya Escrow. Ukweli ni huu;
PAP wamekanusha kuwa pesa alizopewa Prof. Tibaijuka hawahusiki nazo bali ni za mwanahisa wa zamani wa iptl bwana James Rugemalira ambaye wakati anatoa pesa hizo hakuwa mwanahisa kwani alishauza hisa zake 30% kwa PAP. Mchakato ambao ulifanyika kwakuzingatia sheria na nyaraka zipo Brela.
Hizo mbwembwe za uchaguzi 2015,afadhali mturudishie fedha zetu mlizotuibia kupitia tegeta escrow account na richmond.