IPO ya Voda inauzwa kwa wasio Wazawa

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,503
2,378
Bloomberg News inaripoti kwamba kampuni mbili za mutual fund za Tanzania zimeanzisha mbinu ya kukwepa marufuku ya serikali ya kuuza hisa za kwanza za Vodacom, IPO, kwa wateja wasio Watanzania kinyume na sheria.

Bloomberg News haikuzitaja kampuni hizo wala zinauza hisa hizo nchi gani.
 
Naomba link ya hii habari tafadhari.

Nimeiona Bloomberg News Television, king'amuzi cha DSTV. Nimeitafuta kwenye mitandao siioni wala kwenye local media . Sasa sijui wazungu wanajuaje vitu vya ndani ambavyo sisi wenyewe hatuvijui.
 
Naomba link ya hii habari tafadhari.

Link hii hapa.

Hii IPO haijafanya vizuri kwani kufikia sasa wawekezaji wamenunua asilimia 2.3 tu ya hisa zinazouzwa.

Edit.

Samahani hapa nilichemsha pakubwa. IPO ya TICL ndio iliofeli (imeomba nyongeza ya muda) sio ya VODA. Hio asilimia 2.3 ni ya TCCIA Ltd na sio Vodacom.
 
Link hii hapa.

Hii IPO haijafanya vizuri kwani kufikia sasa wawekezaji wamenunua asilimia 2.3 tu ya hisa zinazouzwa.


Duuuuuu... Only 2.3% ?

IPO iliyofanywa na NMB imewafunika by far. Sasa hii haiwezi tena kuitwa the biggest IPO ever.
 
Duuuuuu... Only 2.3% ?

IPO iliyofanywa na NMB imewafunika by far. Sasa hii haiwezi tena kuitwa the biggest IPO ever.

Kweli. Nadhani hali ya uchumi kipindi kile na sasa ni tofauti. Timing ya IPO pia inachangia....
 
Back
Top Bottom