Mkuu haihitaji umri mkubwa sana kutujua watanzania. Hata kijana mbichi kabisa anatosha kutufahamu. Kwa kizazi hiki na vizazi kadhaa vijavyo hakuna mtanzania ataamka kwa tafsiri ya mtoa mada. Labda kuamkia humu kwa kukoment kwa hasira tuu. Akitoka hapo adamke kupanga foleni saa 10 usiku ya kupata namba ya nida.
Akipata nafasi aangalie bunge la chama kimoja kwenye nchi ya vyama vingi.
Baada ya hapo asome kwenye highlights jinsi serikali inavyopambana kuhalalisha wabunge 19 wasio na chama kuwepo bungeni.
Asubirie msimu wa kupitisha bajeti agombezwe na kufokewa na waziri mwenye dhamana kuhusu tozo na akemewe kua kama hawezi ahamie burundi, apatwe na hasira, aje aandike uzi mitandaoni, kesho aamke akale chapati mbili na maharage asonge mbele na maisha.
Asubiri debe la mahindi lifike elf 30 aje alielie utadhani haoni mahindi yanayoenda kenya kule mpakani. Viongozi waje waseme asiwe na wasiwasi, kuna akiba ya kutosha.
Asubiri polisi wauwe watu kwa hila ama tamaa ya pesa kisha waseme walikua magaidi. Au wawe wazembe kiasi kwamba vitoto vijiite "panya road" na "watoto wa ibilisi" walitikise taifa kisha askari wakurupuke, wauwe hata watu waliochelewa kurudi nyumbani kisha watangaze vifo vya panya road.
Watanzania hawa
Wangekua wakuamka wangeamka siku nyiiingiii...