CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 855
Ipo Siku Nitaenda Kulala Geti La Ikulu.
Inawezekana msomaji usiamini haya, ukaona ni mzaha tu. Ila ipo siku kwa kweli nitaenda kulala mlangoni ama getini mwa ikulu ili Rais atakapokuwa anatoka anikute na nimweleze kwa nini nimechukua hatua hiyo.
Mimi nimekuwa mfanyakazi na mlipaji kodi mzuri tu kwa kipindi chote wakati nimeajiiriwa. Nimekuwa mlipaji kodi mzuri kwa sababu hakuna namna ambayo mfumo wa ajira rasmi unamruhusu mfanyakazi akwepe kodi. Hongera wafanyakazi wote Tanzania. Licha ya kuwa mlipaji mzuri wa kodi, mimi kama mfanyakazi ndiye naiwezesha serikali ya nchi yangu kuvuna kodi toka kwa waajiri binafsi, no mfanyakazi no kodi toka kwa mwajiri kwenda kwa serikali. Amini usiamini!
Kwa nini nitachukua hatua hii. Nitachukua hatua hii ili nipate nafasi ya kumuuliza Rais, kwa nini serikali yake imezuia pesa za watu kupitia mifuko ya jamii kama vile PPF, NSSF n.k., wakati pesa hizo ndiyo tegemeo pekee la vijana kuzifanyia biashara, kilimo na hata kujikimu kimaisha baada ya kupoteza ajira? Nitamuuliza Rais kwa sababu naamini tangu yeye aingie madarakani ndiyo tatizo hili limeanza. Hapo awali, wafanyakazi walioacha ama kuachishwa kazi, waliweza kuchukua pesa zao kupitia kitu kinaitwa 'fao la kujitoa'. Ila hivi sasa, fao la kujitoa limesitishwa kwa kile kinachodaiwa utekelezaji wa sheria ya hifadhi ya mifuko ya jamii.
Nitamuuliza Rais pia, mimi kijana wa miaka thelathini na wale wenye miaka ishirini na kitu, tutaishi vipi kipindi hiki ambacho tumepoteza ajira? Nitamuuliza pia, je, angekuwa yeye kwa hali kama hii ya kulazimishwa kuishi mpaka miaka 55 au 60 bila kazi kutokana na kufukuzwa, ama bila biashara angejisikiaje?
Nitafanya hivyo kwa sababu pesa iliyozuiliwa na serikali kupitia mifuko ya jamii ni jasho langu na wala sikuiba kwa mtu.
Lakini wakati nikichukua hatua hiyo, pia najiandaa kulishitaki shirikisho la vyama vya wafanyakazi--TUCTA na chama shiriki ambacho kilikuwa kinafaidika na asilimia mbili toka mshahara wangu wa kila mwezi, kwa kushindwa kupigania haki yangu. Nitawashitaki ili wanilipe asilimia mbili ambayo ilikuwa ikikatwa toka kwenye mshahara wangu kwa kipindi chote ambacho mimi nilikuwa mwanachama.
Eee MUNGU Nisaidie Na Unipe Ujasiri. Ameni.