Ipi ni Tiba sahihi ya Mba wa kichwaani?

Ipi ni Tiba sahihi ya Mba wa kichwaani?

Kama ulipo Kuna maji ya chumvi na sabuni unayotumia ni ya kipande huwezi kupona MBA kamwe.Sasa ufanye vipi epuka sabuni ya kipande kichwani tumia Shower gelly ama kama usawa unakaba basi jitahidi utumie shampoo.Ila sabuni za vipande hizi sijuwi mnaita medicated soap ndo chanzo Cha MBA.
Yan umenifungua macho..mimi mba hazijawahi kuisha aisee!
 
Kama ulipo Kuna maji ya chumvi na sabuni unayotumia ni ya kipande huwezi kupona MBA kamwe.Sasa ufanye vipi epuka sabuni ya kipande kichwani tumia Shower gelly ama kama usawa unakaba basi jitahidi utumie shampoo.Ila sabuni za vipande hizi sijuwi mnaita medicated soap ndo chanzo Cha MBA.
Mh
Muoge mtakate, msisingizie sabuni…
Wanawake wanaosuka baadhi wana mba sbb nywele haipati maji mara kwa mara.

BabaMorgan nyoa kipara, wakati ukiendelea na matibabu.
 
Msaada wa tiba ya mba kichwaani au sabuni inayoweza kuwapunguza??

Natanguliza shukrani
Kanunue shampoo nzuri haswa z wahindi na wazungu achana na shampoo za mtaani zinazo uzwa buku buku pili kuwa msafi kwa kuosha nywele na shampoo kila wiki anza kuosha na shampoo kisha suuza nywele na maji ya white vinegar pia kuwa makini nansaloon haswa za uswazi zinaambukiza sana mba sababu ya kuchangia vitana pia unaweza mix dawa za aspirin na white vinegar maana ndo rahisi apple cider vinegar gharama sana mix kisha nawia kichwani massage kichwa chote kwa dakika kadhaa kisha ukoshe na shampoo upakae mafuta kama ya nazi au olive oil mba wengine wanatokana na ukavu wa ngozi pakaa mafuta vitana chanuo lako vioshe pia na shampoo siku ukitoka kunyoa saloon OSHA nywele
 
Nenda duka la dawa mwambie nahitaji yale mafuta ya MBA ambayo yapo kwenye kikopo fulani hivi Cha kijani jina lake limenitoka ni ya mgando fulani hivi yanatoka South Africa, hayo mafuta ndio kiboko ya MBA yanatibu kabisa kabisa hakikisha unapakaa kila siku asubuhi na jioni au usiku kabla ya kulala na hakikisha unamaliza kikopo kizima yaan umalize dozi nzima sio unafika Nusu unaona umepona unaacha kupaka yanauza 7,000/- nadhani labda Bei iwe imepanda
 
Back
Top Bottom