Ipi ni mashine bora ya gemu kati ya Xbox One na Ps4

Ipi ni mashine bora ya gemu kati ya Xbox One na Ps4

I vote for Xbox One, I have to admit, nilikua fan mkubwa sana wa Play Station, lakini Sony walipotoa Play Station 3 na Microsoft walipotoa Xbox 360 niliamua kuzi test zote mbili.. Aisee Xbox ni moto, mara ya kwanza niliona controller za Xbox ni za ajabu lakini nilipozitumia for the first time kwenye GTA 4 ndo nikaamini controller hizo ndio nzuri zaidi hasa kwa sisi tunaopenda Action Adventure games na sasa naagiza Xbox One na pre order Assassin's Creed Unity, Silent Hills na GTA 5.
 
Nitakuja uniuzie
 
All in all.. unataka kitu roho inataka we ni fan wa Xbox bt mim ni was PS..ni kama unavyo mpenda msichana kwako utamuona ni mkal xna bt for mi ohh..shit huyo hajanivutia hata kidogo(ni mfano)..
 
Hivi hizo xbox one na ps4 Tanzania zishafika na wanaziuza wapi na ni shillingi ngapi? ps3 niliionaga mlimani city kipindi cha nyuma sana...
 
Hivi hizo xbox one na ps4 Tanzania zishafika na wanaziuza wapi na ni shillingi ngapi? ps3 niliionaga mlimani city kipindi cha nyuma sana...

bora uagize mkuu. Xbox One inauzwa kwa USD 399 ambayo si zaidi ya laki saba, na wanakutumia bure (free shipping). Visit website yao, nunua moja kwa moja kwenye Microsoft Store yao.
Hawa wengine wakizileta hapa ndo unaona wanauza mpaka milioni moja na ushee, wanataka faida tu. Bora uagize moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wenyewe, hupat shida.
 
mi ni PC Gamer ila nje ya PC napenda PS4...
kuna games za kutosha za maana, Xbox wana exclusives za ovyo.. PS4 wana xckusives za hatari, game kama Infamous Second son tisha sana.. kwenye graphics PS4 na xBox hawana tofauti, wote wanarun games zao 1080p kwa 60fps vzr tu, sema kwa aliyezoea PC games mwenye rig ya ukweli ka NVIDIA GTX780ti hatotaka kugusa console kabisa..

Kwa anayeongelsa kinect, kinect ni ovyo, haina support kabisa softwares chache zinarun kwa kinect.. Sony subiri wanakuletea Project Morpheus, virtual reality glasses exclusive kwa PS, hiyo xbox lazima wafunge maduka...
 
xbox wana exclusive za ovyo??? acha utani kaka unapozungumzia exclusive za xbox moja kwa moja kinachonijia akilini ni halo, namaanisha lile game ambalo limebuniwa na yule yule genious wa movie PETER JACKSON. halo limechukua tuzo nyingi sana na kama wewe unakataa sio game zuri sijui nitakusaidiaje.
halo-video-game-1-1343923086-view-0.jpg

NIKUPE TU STATISTICS NDOGO JAPO HALO LIPO XBOX TU ILA NDIO GAME LA 3 KWA KUUZA NAKALA NYINGI KWENYE HISTORIA YA VIDEO GAMES

ukija kwenye magari unajua kabisa kuna kitu kinaitwa FORZA mimi sio mpenzi wa kukimbiza haya madude lakini huwezi jiita mpenzi wa magari ikiwa hata video ya youtube ya forza hujaiangalia
2372724-6163165706-93d4d.jpg

hayo ni mawili makubwa ila kuna magame kibao yenye majina ni exclusive kwenye xbox one kama
1.titanfall
2.d4
3.dead rising 3
4.killer instinct
5.na mengine mengi

pia ukumbuke kaka microsoft ni kanmpuni ya kutengeneza magame pia games kama halo ni product ya ndani hivyo hayana time kama exclusive za ps4 ambazo baada ya mwaka zitakuja xbox one.

tuje kwenye kinect, ukiidharau kinect then wewe ntakuita adui wa teknolojia, kitu ambacho kinatafsiri kiziwi anachosema kikakuletea kuwa maneno, kitu ambacho kinafanya ukuta wowote uwe touch screen unakiita ovyo. sababu tupo kwenye games tusitoke nje ya mada tustick hapa hapa kwenye xbox one.

kinect game 1 fighter within
angalia game la kinect hapo

pia ukumbuke kinect si ya kuchezea games tu inatumika kutambua gestures hivyo huhitaji remote unapokua una explore app zako za xbox just unamove mikono unaponavigate.
 
Last edited by a moderator:
xbox wana exclusive za ovyo??? acha utani kaka unapozungumzia exclusive za xbox moja kwa moja kinachonijia akilini ni halo, namaanisha lile game ambalo limebuniwa na yule yule genious wa movie PETER JACKSON. halo limechukua tuzo nyingi sana na kama wewe unakataa sio game zuri sijui nitakusaidiaje.

NIKUPE TU STATISTICS NDOGO JAPO HALO LIPO XBOX TU ILA NDIO GAME LA 3 KWA KUUZA NAKALA NYINGI KWENYE HISTORIA YA VIDEO GAMES

ukija kwenye magari unajua kabisa kuna kitu kinaitwa FORZA mimi sio mpenzi wa kukimbiza haya madude lakini huwezi jiita mpenzi wa magari ikiwa hata video ya youtube ya forza hujaiangalia

hayo ni mawili makubwa ila kuna magame kibao yenye majina ni exclusive kwenye xbox one kama
1.titanfall
2.d4
3.dead rising 3
4.killer instinct
5.na mengine mengi

kinect game 1 fighter within
angalia game la kinect hapo

pia ukumbuke kinect si ya kuchezea games tu inatumika kutambua gestures hivyo huhitaji remote unapokua una explore app zako za xbox just unamove mikono unaponavigate.

Mtanzania sina bifu na xbox, preference yangu ipo tu kwenye PS... unavosema gestures kwenye kinect usidhani PS camera huwezi fanya gestures, inafanya vzr tu, sema kuplay games kwa action kama kinect ndo huwezi, na kinect games ni za ovyo huwezi kuta AAA game inatumia kinect, umeongelea Forza, hilo game moja lisikupe kichwa, kwenye PS kuna games nyingi tu za racing kali zaidi, hilo game mbona la kawaida sana physics zake, hadi indie developers wanafanya kwa engines kama Unreal fasta tu.. Game moja lisifanye ukaona platform imejaa games za maana.. cheza game ka Crysis 3 ultra uone inacheza poa sana kwenye PS ila kwenye xbox utatoa machozi inavokwama

advertisement za microsoft zisikupe kichwa huku hujacheza game lenyewe unaishia kuangalia youtube videos, nimetumia console zote mbili ila niko kwenye PC, umeongelea titanfall, huku 2 inakuja kwenye PS4, afu halo game la tatu kwa kuuza unaongelea xBox peke yake, ongelea kwa ujumla hata top 20 haimo., halo sipendi story zao.. hiyo ni preference yangu pia usiniquote vby.. PS wana AAA games kibao kuliko xBox, unavosema microsoft ni game makers, unadhani Sony sio?? sony wameanza games zamani kabla ya microsoft ka hujui

Once again mtanzania, sina bif na microsoft, sema preference yangu iko kwa Sony wanajaribu sana kupush tech kwenye next gen... subiri VR ikija ndo utakaa kimya kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mtanzania sina bifu na xbox, preference yangu ipo tu kwenye PS... unavosema gestures kwenye kinect usidhani PS camera huwezi fanya gestures, inafanya vzr tu, sema kuplay games kwa action kama kinect ndo huwezi, na kinect games ni za ovyo huwezi kuta AAA game inatumia kinect
makali yamepungua eeh. unajua fika kuwa kinect inadestroy pes eye hizi ni baadhi ya games zinazotumia kinect
1.forza motosport (sema ni game ya ovyo)
2.tom clancy's ghost reckon
3.steel battalion
4.mass effect 3
5.tiger woods pga tour
6.gunstringer
7,child of eden
8. rise of nightmare
9.just dance
10.fable the journey

kaka kama game hizi mass effect, ghost reckon na kina forza ni za ovyo sure wewe sio gamer. hizo ni chache ila zipo nyingi zaidi.

, umeongelea Forza, hilo game moja lisikupe kichwa, kwenye PS kuna games nyingi tu za racing kali zaidi, hilo game mbona la kawaida sana physics zake, hadi indie developers wanafanya kwa engines kama Unreal fasta tu.. Game moja lisifanye ukaona platform imejaa games za maana..
forza nimetoa kama mfano kuzima kauli yako kuwa exclusive za xbox ni ovyo na halipo moja nimekutajia magame matatu kama halo, titanfall na hio forza na nimetoa kama tu mfano sio kwamba ndio hayo hayo

advertisement za microsoft zisikupe kichwa huku hujacheza game lenyewe unaishia kuangalia youtube videos, nimetumia console zote mbili ila niko kwenye PC, umeongelea titanfall, huku 2 inakuja kwenye PS4,
hivi unajua maana ya exclusive? ngoja nikueleweshe kaka.

kwenye game exclusive inamaanisha kampuni inatoa game kwa ajili ya console fulani kwa muda fulani kabla ya kurelease lile game kwenye console zote. as long as titanfall ipo xbox sasa hivi tunaiita exclusive hata kama bado mwezi itoke ps4. ikishapita ule muda wa exclusive basi ndio watatoa na huko kwenye psa4

afu halo game la tatu kwa kuuza unaongelea xBox peke yake, ongelea kwa ujumla hata top 20 haimo., halo sipendi story zao.. hiyo ni preference yangu pia usiniquote vby..
nakubali kuhusu nje zipo game ambazo zimeuza zaidi ila kwenye top 10 kuna game 1 tu la juzi juzi nalo ni gta v tena lipo mwisho mwisho game zinazouza sana hazitoki kwenye console kubwa list mpaka sasa inaongozwa na tetris ikifuatiwa na super mario.

PS wana AAA games kibao kuliko xBox, unavosema microsoft ni game makers, unadhani Sony sio?? sony wameanza games zamani kabla ya microsoft ka hujui
mimi si mpenzi wa shooter games nacheza sana rpg/strategy games na nimemaliza series yoyote ya age of empires ya microsoft. toka nipo mdogo nacheza age of empire kama hutajali hebu taja title za game zilizotengenezwa na sony ambazo ni blockbuster. maana unavyoongelea age of empire unaongelea game ambalo ni legend.

Once again mtanzania, sina bif na microsoft, sema preference yangu iko kwa Sony wanajaribu sana kupush tech kwenye next gen... subiri VR ikija ndo utakaa kimya kabisa

miaka na miaka sony alikua anabebwa na erricson kwenye research mbali mbali since erricson ajitenge hakuna cha maana toka sony kaka. kwenye research na kugundua vitu vipya ni ndoto sony kumpita microsoft

by the way kama unafatilia news microsoft research wameshafanuikiwa kustream games toka online kwa fps za kutosha tu. hivyo subiria soon tutacheza games za console kwenye lumia zetu
 
Back
Top Bottom