Ipi ni lugha ya taifa la tanzania

Eng. SALUFU CA

Senior Member
May 12, 2010
145
16
Ndugu wanajamvi nimesikia kwa muda mrefu kuwa lugha ya taifa hili la Tanzania ni kiswahili, cha kushangaza ni kwamba kwenye shughuli nying za kitaifa tunatumia kiingereza kama lugha kuu, kudhihirisha hilo leo hii dakika chache zilizopita kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam hotuba zote zimetolewa kwa kiingereza sanasana kiswahili kilikuwa kinachomekewa tu kama vile lugha ya kigeni, naombea mnijuze hivi ni kweli Kiswahili ndio lugha ya taifa hili au ni nadharia tu?
 
Kuna tofauti kati ya National language (Lugha la taifa) na Official language (do I say Lugha Rasmi la serikali?).
Kwa maelezo haya, ni sawa kama kingereza kinatumika in formal meetings and gathering.
 
lugha ya taifa ni kiswaengili maana hata hicho kiswa hili kinachozungumzwa kinakuwa ni tafasili ya kiingeleza ,kwa mfano utamsikia mtangazaji wa redio furani au tv anasema"jambo hilli likifanyika hivi mwisho wa siku madhara yatatupata sote" badaala ya kusema "jambo hili likifanyika hivi HATIMAE madhara yatatupata sote" na ifahamike wazi kwamba viombo vya habari huaminia sana na lolote linalosemwa huchukuliwa ndio lugha lasmi na hatimae huzoeleka.
 
Tanzania Official language(s)
Swahili (de facto)
English (Higher courts, higher education)
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom