Ipi Bora kata ya hydram water pump, solar system na pump ya mafuta

Lizo mkristu

Member
Oct 31, 2019
69
80
Mimi ni namiliki shamba la parachichi mkoani njombe ukubwa NI heka10 na shambo lipo juu ya mlima na kwenye upunde wa mlima chini ya mlima huo ndio kuna bonde na chanzo cha mto sasa naitaji kumwagilia miti hii ya matunda je nitumie pump ipi kujaza tank Kati ya hydram water pump,solar pump na pump za mafuta na ipi inagarama nafuuu.aksante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salama mkuu?

Sasa mjomba wewe wekeza kwenye hydrum pump.

Hizi ni rahisi kuzitumia kwani hizi hutumia mtiririko wa maji au Stream kujiendesha.

Hizi hazitumii mafuta hivyo kukoa gharama na pia hazite pollution.

Pia hufanya kazi usiku na mchana.

Simple ideas, big benefits.

Hizi pumps zipo za uzito wa 68kg na za uzito wa juu kabisa yaani 250kg
 
Mimi ni namiliki shamba la parachichi mkoani njombe ukubwa NI heka10 na shambo lipo juu ya mlima na kwenye upunde wa mlima chini ya mlima huo ndio kuna bonde na chanzo cha mto sasa naitaji kumwagilia miti hii ya matunda je nitumie pump ipi kujaza tank Kati ya hydram water pump,solar pump na pump za mafuta na ipi inagarama nafuuu.aksante.

Sent using Jamii Forums mobile app
zote ni mtihani mkubwa. Kila moja ina changamoto za kutosha. Njombe jua linazingua sana, ni muda mfupi sana katika mwaka utakuwa na jua la kutosha, vinginevyo ufunge panel za kutosha. Hydram kama fundi anaifunga vizuri na kuna poromoko stable ( maji hayapungui) ni nzuri, ila ikianza kuzingua, ni changamoto sababu mafundi ya hiyo kitu ni wachache mno. Pump ya mafuta ni changamoto zaidi kwenye kiwese na usafirishaji wa kiwese kwenda shamba kila wakati. Kama unapata fundi, hydram iwe namba moja, ije solar na umalizie na pump ya mafuta. Nipo palee Kifanya nasubiri mrejesho mkuu.
 
Back
Top Bottom