iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

Kuna kitu watu wenye maisha yao wanakiita Exclusivity. Maana yake ni upekee. Android nyingi hakuna tofauti kati ya mwenye ya $100 na wa $1000 but apple wanakupa wewe the extra sababu umelipa more. Leo hii mwenye samsung A51 anaweza kufanya almost kila anachoweza fanya mwenye s20 Plus. Ila ukiwa na iphone 7 tuu kuna vitu utakua unavikosa na vipo kwenye iphone 7Plus.

unazijua android za $1000 uliishaishika ukaona inafananaje!!!!

acheni unazi bana,embu kachukue flagship ya samsung 2016 s7 edge niambie inafanana na simu ipi ya android??

mfano uliotoa hapo haulingani hata kidogo,umeringaniaha mbingu na ardhi,hizo ni simu sio sawa hata kidogo,kuanzia nguvu,camera,upana na ubora wa kioo mpaka uimara.

apple wanachofanya ni kucheza na akili za wateja tu wao wakifanya baishara,kwamba tutoe simu mbili moja iwe nyekundu bei iwe juu,na nyeusi na nueupe bei ziwe ndogo.
 
Kifungu cha tano hapo.Muhamishia simu kwa PC ni rahisi na unatumia Itune.Asante
Sio rahisi ukilinganisha na android ambayo ukichimeka tu cable unahamisha mafaili fasta tu kama vile umechomeka flashi.

Huko iphones kila computer ambayo haina itunes unayotaka kuhamishia mafail hutaweza kuhamisha kitu mpaka uingize program hio ya itunes, ni shughuli pevu kiukweli

Nakumbuka chuoni watu wenye iphones ilibidi wawe wanabeba flash kuprint assignment zao maana stationery walikuwa hawataki habari za itunes, sisi na android zetu tulizigeuza ziwe multi purpose tunatunza vitu na kuvihamisha kirahisi
 
Na makumpuni mengi ya simu yanamuiga apple kafanya nini ndipo nayo yatoe matoleo mapya.
Apple anakwenda na wakati ujao.
Be blessed
wamuige apple kwa kipi wakati iphones ina mapungufu kibao 😂😂 unataka waige kuuza simu bila charger na earphones yani simu inakuja kivyake tu 😂😂 ama kweli apple anagonga faida, yani chaja utanunua wewe, earphonea wewe na ukitaka kutumua earphones za waya hapo bado ununue adapter zao 😂😂, mwenye mapungufu haigwi
 
1. i phones ni gharama, Hapa sitazungumza sana, nachoomba tu nenda duka linalouza i phones mpya (sio mitumba / refurbished) kaulize bei, Inabidi uwe vizuri kiuchumi tofauti na huku android kuna simu hata za laki kwa wenye bajeti finyu ila pia kuna simu za gharama kuliko hata iPhone kwa wanaojiweza kiuchumi. Hata hivyo bado wapo wasiojiweza kiuchumi wanaolazimisha kununua i phones, kundi hili hununua simu hizi kwa lengo la kufeki maisha waonekane wapo vizuri kimaisha.

3. Hakuna tundu la kuingiza earphone hizi zilizozoeleka za pini, hapa hadi ununue vifaa vya ziada, huku android ukinunua ear phone unaitumia hapo hapo

3. Andaa laini moja tu, kuna matoleo machache sana yenye laini 2.

4. Kudownload nyimbo hata humu jamiifroums ama mtandaoni ni ishu nzito

5. Kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye pc ni shughuli pevu.

6. Apps kibao zipo android kuliko iphone

7. Unaweza ku root android ukabadili hata os na kuipiga sarakasi simu kadri utakavyopenda , Kwa iphone kuna zoezi la jail break, hapa utaweza tu kufanya baadhi ya vitu ambavyo android vinawezekana tayari hata bila kufanya rooting kama kubadili mwandiko, kuseti ringtone iwe muziki anaotaka, n.k Jail break ni kama mtu aliyefungwa kitambaa machoni kutolewa kitambaa ili aone, rooting ya android ni kama kupewa darubini

8. Hutaweza kusikiliza radio bila bando, kama upo vijijini sehem isiyo na internet fanya utaratibu wa kununua radio.

9. Android utaweza kuback up vitu vyako kwenye memory card na pia unaweza kubadili battery kwa wepesi bila hata kwenda kwa fundi, lwa iphone hizi feautures sahau.

10. Kwenye i phone ku customize vitu kuna vikwazo, mfano ringtone utachagua tu wanazotaka wao iphone na inakuwa sekunde 30 tu, huku android ringtone uutaweka hata ya kingwendu ni wewe

11. kitaa cha notification hakipo kwenye iphone, mfani message ikiingia kama simu ipo silent huku android kataa kanawaka.

12. hutaweza kuseti default app, utaweza kudownload app mbadala ya kufungua mafaili lakini hutaweza kuiseti iwe ya moja kwa moja, kika ukifungua faili litafunguliwa na app ya mwanzoni

13. andoid kuna feauture ya multiple user account, simu inakuwa kama facebook, kila moja ana user name yake na password, naweza kumuazima mtu simu akaitumia bila kujua taarifa zangu na akiniruduishia basi na login kwenye user yangu.

14. Battery kwa iphone ni tatizo, wenzangu wenye i phones wanajiteteaga i phone sio simu ya kutumia tumia kila muda basi naishia kucheka tu napoona wanatembea na power benki simu zao zinapokata moto.

15. Kwenye android unaweza kutumia simu kama remote kwa vifaa kama samsung, lg ,n.k....huko kwa apple so rahisi labda kwa tv zao za apple tv

16.Watu wengi huwa wanadhani iPhone ndio kinara kwenye kamera, hili si kweli, Kuna simu kibao tu kama xiaoni, google, oneplus 8 zina kamera nzuri zaidi kuliko iPhone yoyote


Wewe mahitaji yako yakiwa ni finyu, lazima uridhike na iPhone yenye features chache, Mimi mahitaji yangu yakiwa mapana, mwenye Iphone huwezi kunielewa nikitaka simu yenye features nyingi


Mapungufu ni mengi ila wacha niishie hapa
Mtoa mada unatumia simu gani na je huwa unafwatilia matoleo mapya (latest) ya simu mbalimbali?
 
Hiyo android haina jina nijibu na hilo nililokuuliza kama huwa unafwatilia matoleo mapya ya simu mbalimbali
Ukijibu lengo langu ndio utalipata
Mkuu umeshindwa kuelewa hata kichqa cha habari ya hii post? Hebu tafuta hata mtu wa karibu yako akueleweshe lengo la huu uzi.

Kiufupi huu uzi unawakilisha simu za ndroid zote duniani, wewe sema unachotaka kisha ntafanya reference kwenye simi yoyote ya Android hata kama imetoka jana.

Kwani shida nini 😁😁
 
Mkuu umeshindwa kuelewa hata kichqa cha habari ya hii post? Hebu tafuta hata mtu wa karibu yako akueleweshe lengo la huu uzi.

Kiufupi huu uzi unawakilisha simu za ndroid zote duniani, wewe sema unachotaka kisha ntafanya reference kwenye simi yoyote ya Android hata kama imetoka jana.

Kwani shida nini 😁😁
Kwa kifupi hijielewi
 
Mimi situmii iphone na sina mpango wa kununua hiz simu kama nipo ndani ya nchi mfano wa Tanzania au nchi maskini zaidi ya Tanzania, lakini iphone ni moja ya simu zenye features zinazotakiwa kwa dunia5ya Leo.
Tunachoashindwa kujua ni kwamba Dunia hipo mbali sana kiteknolojia na internet ndiyo kila kitu ndiyo maana iphone wanahitaji internet connections hata kama radio, wenzetu nchi za mbele internet siyo tatizo .

Kwa maandaleo ya technology sasa vitu kama earphone za pin/wire, memory card, slot za kuweka sim kadi zaidi ya moja kwenye simu, mambo haya yanafikia mwisho zimebaki nchi ambazo hazijapiga hatua kiteknolojia.

Nina mengi ila muda unanibana kuandika, lakin iphone ni simu ambazo wewe na Mimi tulio ktk maandaleo finyu ya technology siyo walengwa rasmi.
Tambua features za iphone ndizo zinazo takiwa kwa Dunia ya Leo, hasa ukizingatia uharifu sasa unahamia ktk mitandao.

Kwa nchi ambazo hazijapiga hatua kiteknolojia simu kama Samsung, nokia ndiyo type yetu kwa wale wapenda simu za cheap simu kama techno na infinix zinatosha.
Hizi ni siasa tu haujaongea fact yoyote ya technology
 
Mkuu. Naomba kukurekebisha kwa mambo machache na uchache huu ukawe mwingi kwako. Natumai kama ni mtu wa kujifunza utapata somo kubwa sana. Tambua kwamba kabla iphone hajaingia sokoni kulikua na makampuni tycoon ambao pia walikua sokoni na walikua wanafanya vizuri na bei zao zilikua sio za kitoto. Naomba nikujibu point zako moja baada ya nyingine kama ifuatavyo

1)Kusema iphone ni gharama naomba nikupinge kwa ukali sana. Kwenye sim unatakiwa ujue kuna matabaka ama niseme grades. Kuna Flagship, kuna midrange na budget smartphone. Zunguka dunia nzima ni ngumu sana kukuta Flagship inauzwa hizo bei unazosema za laki nakitu.
Tizama kielelzo cha picha hapa chini
View attachment 1634975
View attachment 1634976
Ukitazama hapo ni iPhone 11Pro Max ya mwaka 2019 na samsung s20Ultra ya mwaka huo huo. Ukitazama kwa UK sim hizo zinauzwa bei sawa kabisa, ukija Marekani, Samsung ni ghali zaidi, ukirudi india sim hio iPhone inauzwa ghali zaidi ya samsung.
Hii inatokana na facts na variable nyingi sana ila trend ni hio. Tizama sim nyingi sana za Android huwa Ghali mwanzo ila miezi baadae zinapungua value pakubwa sana, kinachokufanya uone iphone ni ghali ni sababu market value yake inabaki juu kwa muda mrefu. Mtu mwenye laki nne ni ngumu kumuelewesha kwamba iphone 7/7Plus simu iliotoka mwaka 2016 mpaka leo bado hawezi ipata mpya kwa bei hio atasema ni expensive.

2) Ni ajabu sana mpaka mwaka 2020 bado unashangaa kutokua na tundu la earphone. Hili swala walilalama sana watu 2016 na leo hii ndo trend. Kila sim inayojielewa inaelekea huko.
View attachment 1634985
Hii ni Samsung Galaxy Note 20 ultra. Nioneshe tundu la headphone hapo. Japo wameweza kuweka tundu lote hilo kubwa la S-Pen ila wameignore kabisa earphone. Kubali ukatae hio ni technologia inayokufa taratibu.


3) Mkuu tatizo tupo dunia ya tatu ndo maana unapata tabu kidogo kuelewa na unahisi kwamba kuna tatizo mahala. Kumbuka iphone yuko many steps ahead. Dunia saivi inaelekea kwenye virtual /E-Sim. Inaachana kabisa na mambo ya physical sim. Kama umeona kwanzia iphone Xs- latest zinakua na dual sim. Sasa ziko za dual physical sim ambazo ni HK version na ziko ambazo dual sim yake ni E-Sim (Electronic Sim)
View attachment 1634996

Hii huhitaji kuwa na line. Kwa wenzetu unaenda Kampuni yako ya mtandao wanakupa QR code unascan unapata line ndani ya sim yako. Tanzania tutafika huku ila sijui lini. TCRA walitazame hili.

4) Kumbuka kwamba kuna kitu kinaitwa loyalty. Kwako wewe mtumiaji unaweza ona umebanwa kudownload miziki ila kumbuka illegal download ni kosa kisheria na unaweza fungwa. Lakini pia kwa wasanii hii inawasaidia wao kuboost digital sales zao. Hii ni mbinu ambayo tunakoelekea itakua implemented in most platforms. Imagine wewe kama unauza duka la mangi tuseme (alafu kuna namna 50% ya watu wanaweza kuchukua bidhaa zako bila wewe kunufaika, hio imekaa vipi?)

5)sijaelewa unaamanisha nini kusema shughuli pevu. Nadhani swala la security basi kwako ni dogo sana. Unafahamu kwamba sim nyingi za Android kwa kuwa na option ya Debugging mode, mtu anaweza tengeneza sim virtual kwenye computer alafu akachukua sim yako na akaipaste kila kitu kwenye computer hio virtual na kuwa na uwezo wa kuona kila kilichopo kwenye sim yako. Je hicho ndicho unachotaka? Mimi nimetumia iphone tangu mwaka 2007 na android pia nimetumia. Sijawai ona hio shughuli pevu unayoisema wewe labda unieleweshe.

6)Naomba nikusahihishe hapa. Na nikutume ukafanye tena research. Ichi unachozungumzia kilikua kweli 2016 kurudi nyuma. Sasaivi tizama kampuni nyingi kubwa za apps, kuna hata tweaks au niseme vionjo ambavyo vinawekwa kwenye iphones tuu. Kuna apps ambazo huanza na kuingia kwenye iphones kwanza kabla ya android “mfano hai games kama Fortunite” pia application kama instagram na whatsapp na snapchat zinafanya vizuri sana kwenye iphone sababu kila iphone inapata a tailor made app. Mfano mwaka huu 2020 zimetoka iphone nne zenye ukubwa tofauti wa screen iphone seii, iphone 12mini, iphone 12/12pro na iphone 12Pro Max, ni rahisi kwa izi application kutengenezea kila sim application iliokua edited special for hio sim. Ila kwa android sababu ni soko zima la sim zaidi ya 500 tofauti tofauti basi inatengenezwa one app fits all ndo unaona kunakua na mvutano wa picha na video.


7) SECURITY IS KEY FEATURE KWENYE SIM NDO MAANA NILIKUAMBIA MWANZO WEWE KUA NA UWEZO WA KUGARAGAZA SIM YAKO KUMBUKA UNAWAPA UWEZO HUO HUO WATU WASIO NA NIA NZURI NA WEWE


8)nataka uchukue samsung Flagship yeyote ya latest toka 2018-2020 alafu sikiliza nayo offline radio alafu njoo tena hapa leta argument. Again iphone wapo mbele technological. Vitu wanavotoa na kuviacha wengine hufuata muda mfupi badae.

9)Mkuu naanza kuamini kwamba kuna uwezekano hii kitu umecopy paste mahala ukabadili lugha na hii ilikua post ya 2016 kurudi nyuma.
View attachment 1635005
Hii ni Note 20Ultra. Kubadili battery kwenye hii sim ni mtihani and so is many Androids. By standards iphone ni moja kati ya sim rahisi sana kubadili battery tofauti na hizo android zako.
Kwenye swala la storage na kuback up sim kwenye memory card, nikurudishe tena SECURITY

10) Kama kitu hujui sema sijui, ukiskia mtu kasema kitu flani hakiwezekani embu fanya research kwanza kuliko wewe nawe kuruka kwamba haiwezekani.
View attachment 1635006
Hii ni sim yangu na utaona nina Ringtone ya Ratvanny naogopa. Sasa wewe sijui uliona wapi kwamba haiwezekani.

11) Again technology inapoenda taa zinatoka. Na kuna option kwenye iphone ya kuset flash light ikuallert.

12)Tena narudia kama hujacopy paste hii kitu kutoka mwaka 2016 basi hujawai tumia iphone ama hujafanya research. Default apps unaweka vizuri tuu.
View attachment 1635014

Email zangu zote nafungua kwa Gmail app, Safari ndo Default browser nilioweka. Kuweza kuset hivi nenda settings alafu app unayotaka mfano Google Chrome alafu utapata option ya make this Default browser.

13) SECURITY. Kasome kuhusu uwezo wa ADB na SDK alafu hutathubutu tena kulog in kizembe zembe kwenye sim za watu.

14) hao wenzako wanatumia iphone gani boss? Na hizo Powerbank wanatembea na powerbank gani? Naomba nikupe mfano, mtu mwenye iphone 11Pro Max anauwezo wa kukaa na chaji kwenye sim yake kwanzia saa moja asubuhi mpaka saa tisa mchana. Thats a fact. Iphone huonekana ina battery ndogo ila hakuna sim yenye optimization kama iphone, ukizingatia na kuwa na ABionic Chips basi hii inawapa mileage kubwa zaidi tofauti na sim ambazo zinatumia 3rd part chipsets.
View attachment 1635022
Utaona hapo tofauti ya iphone na zingine ni ndogo sana and by 2020 standards, still promising.

15)ECO SYSTEM MKUU ndo maana unaona hata kwenye sim tu skuizi app zinataka ubaki kwneye app zao. Unafungua link inafunguka in app built browser kukuweka built in. And thats what apple is doing. Ndo maana as a company wanazidi kua successful.

16)Hili linaweza kuwa na ukweli kwa asilimia kadhaa but as research shows, video zinazochukuliwa kwenye iphone zinakua more stable na vivid kuliko on anyother smartphone. Nikutume ukaangalie iphone big event wakati wanazindua hizi 12lineup utaona jinsi gani wamechange game la camera kwenye sim.


Nimechukua muda kidogo kukuandalia makala hii natumai utaisoma kwa upana na utaelewa sana.
0786371107 kama kuna ziada.
Siafiki suala lako la kutoa earphone ni suala la kujielewa..hyo ni marketing purpose makampuni yapige pesa za earbuds
 
wamuige apple kwa kipi wakati iphones ina mapungufu kibao unataka waige kuuza simu bila charger na earphones yani simu inakuja kivyake tu ama kweli apple anagonga faida, yani chaja utanunua wewe, earphonea wewe na ukitaka kutumua earphones za waya hapo bado ununue adapter zao , mwenye mapungufu haigwi

Samsung wameshaiga na hilo kama hujui,ishatangazwa kuwa na wao wataacha kutoa charger.Inaonyesha wewe sio mfuatiliaji umeamua tu kuongea vitu ambavyo hata huvijui. Source: Samsung to stop bundling chargers with phones next year, report says
 
Mkuu umeshindwa kuelewa hata kichqa cha habari ya hii post? Hebu tafuta hata mtu wa karibu yako akueleweshe lengo la huu uzi.

Kiufupi huu uzi unawakilisha simu za ndroid zote duniani, wewe sema unachotaka kisha ntafanya reference kwenye simi yoyote ya Android hata kama imetoka jana.

Kwani shida nini

Huwezi kuwakilisha android zote duniani wakati zina features na specifications tofauti kabisa. Mtu anayetumia Tecno au Samsung ndogo hizi hawezi kufanana na anayetumia Samsung,Sony au LG flagships eti kisa ni android zote sababu hata android zenyewe versions zake pamoja na UI zake zipo tofauti kulingana na hadhi ya simu unayoitumia.
 
wamuige apple kwa kipi wakati iphones ina mapungufu kibao unataka waige kuuza simu bila charger na earphones yani simu inakuja kivyake tu ama kweli apple anagonga faida, yani chaja utanunua wewe, earphonea wewe na ukitaka kutumua earphones za waya hapo bado ununue adapter zao , mwenye mapungufu haigwi

Mkuu ukiacha ushabiki ingia fanya research. Utagundua sim zingine zimeiga vitu vingapi kutoka apple. Kuwa na mapungufu haimaanishi kwamba huwezi kuwa mfano. Kuna mambo mengi hasa kwenye pattern na patent android nyingi zinakopi kutoka iphone.
 
Back
Top Bottom