Tafuta charger original , pale mjini kati ya extelecom na sanamu ya askari kuna chager original , nunua waya na plague yake , isipochage utapata shida kupata fundi mwenye uwezo anaezijua Iphone kwani itakua imeua 'power ice' kutokana na charger mbovu.
Tatizo haifiki huku imegoma kuchaji tokea juzi kama picha inavyo onyesha
Jaribu kutafuta chaja ya hiyo simu kama haitochaji ujue kuwa battery imekufa, battery ikishakufa simu haitochaji zaidi ya kuonyesha battery iliyoanza kuchajiwa lakini hutaona progress yoyote ya kuingia chaji kwenye simu.
Duh niko mbali sana na hiyo mitaa kwa vile kunajamaa yangu hapo mjini nitamwelekeza afike mitaa hiyo kwa ajili ya kunitafutia
068 445 9109 ongea na huyu fundi umuelekeze tatizo lako.
Kama anajua jinsi ya kukusaidia, itume hiyo simu kuja Dar kwa ndugu yako akupelekee kwa huyo fundi, akishaitengeneza unamlipa then huyo ndugu yako anakutumia kurudi huko serengeti.
Sidhani kama battery au charger inahusika hapo, iliwahi kunitokea na solution ilikuwa ku hold Home button na power button at once au (unaanza power button then in a split second press home button) kwa muda. Iliwaka na inaendelea mpk leo