IP Adress ya Zantel utata mtupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IP Adress ya Zantel utata mtupu!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Tumsifu Samwel, Sep 19, 2009.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Leo nimeingia kwenye website ya Big Brother Africa ili niweze kumpigia Dada yetu Elizabeth kura,cha kushangaza sikuweza kufanikiwa kupiga kura kwani nimeambiwa kuwa tayari ni meshapiga kura wakati sijapiga kura.natumia modem ya Zantel ya CDMA, ikanibidi niunganishe computer yangu na simu yangu ya mkononi ambayo natumia line ya zantel ya GSM nako nikaambiwa kuwa tayari nimesha piga kura.

  Nilipo angalia IP Adress yangu ya kwenye line ya GSM ilifanana na ile nayo tumia kwenye modem yangu ya CDMA,nika gundua kuwa karibu wateja wote wa zantel wa GSM na CDMA wanatumia IP Adress moja,hivyo mwenzako akikuwahi kufanya kitu ambacho una ruhusiwa kufanya mara moja wewe hutoweza kufanya hivyo.

  Kwa mfano unataka kudownload file kwenye rapidshare hutoweza kufanya hivyo kama kuna mteja wa zantel amekuwahi kwa kudownload,au kama ukifanikiwa mtu wingine akiitaji kudownload hatoweza ampaka asubirie kwa mda sana.
  Wadau hivi hii ni sawa kweli kwa wateja karibu wote kutumia IP Adress moja ? je na Kiusalama inakuwaje endapo mtu akifanya uhalifu kwenye mtandao upatikanaji wake utakuwa je?
   
  Last edited by a moderator: Sep 19, 2009
 2. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Halafu mtindo wao huu mpya wa kukata Tsh,600/= unapu unganisha mtandaa kwenye modem ya CDMA unaudhi sana maana sio watu wote watakao tumia hizo MB 5 wanakupa wakata wana kukuta kiasi hicho.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huo ndio mtindo wa Tanzania wa kufanikiwa kufanya watu wake wasiwe na uelewa na mambo haya
   
 4. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Inabidi ufafanue kidogo kuwa unamaanisha nn mtindo wa Tanzania?
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mazee hii kali. Nadhani ni mimi sielewi au kuna la ziada maana sijawahi sikia watu wana-share IP address.
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  We mzushi ulikuwa wapi siku ngapi hizi --- ndugu angalia bei si wanasema rahisi ? Urahisi huo ni kwa sababu wanashare bandwidth kati ya wateja unakuta mfano wateja 200 wana ip address moja na wanashare wengine mia hiyo hivyo , hata hivyo linapotokea suala la uhalifu kwa mfano nikienda zantel pale wanaweza kunilocate wewe ulipo na kifaa chako ( hii ni etisalat dunia nzima ) , mimi natumia broadband sifanyi sharing na mtu yeyote am dedicated
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Asante kwa ufafanuzi wako ,Je ni sawa watu 200 kushare IP Adress moja?
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  sio sawa mfano halisi ni huo hapo kwamba unapotaka kupiga kura inakuwa ishu , mfano ungekuwa unachat kwenye irc kama darhotwire hiyo address ikiwa banned wote hamuwezi kuingia kwenye chat zamani ilikuwa hiyo enzi za raha.com inatawala , zantel ni kampuni ndogo haiwezi kuwa na uwezo wa kutosheleza wateja wake ndio maana mnashare ila ni siri hawataki kusema yaani hapo sawa na yule aliyekuwa kwenye internet cafe tu anayelipa buku kwa saa
   
 9. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hili tatizo huwa nakutana nalo sana ila sikuwa najua jinsi ya kusolve hili atizo
   
 10. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #10
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huu mfumo wakushare IP Adress kwa hapa Bongo ni kwa mitandao karibu yote wanafanya aka kamchezomna hii inatokana na sisi wa tumiaji wa huduma hizi kutojua haki yetu,hivyo wao wanatupeleka wanavyo taka wenyewe..

  Hivi juzi tu nilisika chama cha watumiaji wa huduma za masiliano walikutana kujadili juu ya gharama za mawasiliano kuendelea kuwa juu ingali ujio wa SEACOM ulisemekana ungeleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano,sijui walifikia wapi na kikao chao icho maana sikuweza kupata kilicho zungunzwa huko.Watumiaji wa huduma hizi za mawasiliano inatubidi tujue haki zetu.
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hivyo vyama vyenyewe havina pros hawaaliki watu ambao wanaweza kuuliza maswali magumu na ambayo yanaweza kufundisha wengine wanaitana wenyewe hili ni tatizo sana kwa nchi yetu hata huu ujio wa seacom nchi haikuwa tayari kwa mradi huu kwa sababu hatuna sheria za mitandao na miundo mbinu mingine hata fiber iliyokwepo ilikuwa haitumiki ipasavyo
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Nadhani hawana I.P za kutosha, hata TTCL kuna wakati nilikuwa napata tatizo hili, kwenye Rapidshare unaambiwa I.P yako inadownload tayari.
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  watu wote wanaopata service toka TTCL ni tatizo kubwa kwao hata sehemu nyingi sana za vyuo ziko hivi halafu sasa mtu akitaka kufanya reserch inayohusu kitu hichi sijui atafanyaje kwa wateja mmoja mmoja
   
 14. C

  Chuma JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wadau hili ni jambo la kawaida kitaalamu. IPv4 address zipo chache na haziruhusu kila mtu kuwa na yake. Technology inayotumika ni NAT. Network Address translation. Hii inafanyika kwasababu moja wapo ni uchache wa IP address na pia security wise.

  Wale wanaotumia rapidshare ingieni kulipia msipende dezo.na rahisi sana.ukiwa na dola5 unadownload unlimited kwa mwezi mzima.Unaweza kuwatumia baadhi ya Members wa JF kukulipia na pesa yao ukawapa ndugu zake hapa Nyumbani.

  Hivi sasa baadhi ya baadhi ya company zimeanza kutumia IP version 6 ambayo hio itafanya kila mmoja awe na IP yake duniani.Simu mpya za Nokia nyingi zipo supported. lkn pia ISP providers nao wanatakiwa infrastructure zao ziweze support IP version6. Windows 2008 ipo supported na IP version6..so it will take time hii change kuchukua nafasi yake.Baadhi ya Nchi tayari ipo ktk Operation.

  Si HAKI ya Mteja kuwa IP address ya peke yake.so far some companies wanakulipisha ili kuwa Public IP ya kwako. Hao watu 200 mliowataja wachache sana. Mnaweza kuwa zaid ya 200 mkawa mnashare the same IP.

  Shy Kuwa na dedicated link haimaanishi kuwa una dedicated IP, unaweza kuwa una share IP lkn bado una dedicated Bandwidth.

  ...So please tuache kuwalaumu Zantel,TTCL or other ISP companies.
   
 15. E

  Exaud Minja Member

  #15
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Na mimi pia natumia mtandao wa ZANTEL CDMA MODEM na tatizo hilo lipo.
  Namimi pia tafizo hilo nalipata pia kwenye kudownload file unaambiwa free download yako imefikia mwisho wakati ni mara yangu ya kwanza. Kweli tunakosa haki zetu kwenye hii huduma.

  Sasa malalamiko yetu yatafikaje kwa walengwa?
  Tusiishie kulalamika tu bila solutions ni naomba kama kuna uwezekano wa malalamiko yetu kupelekwa kwenye magazeti tena kurasa za mbele tusaidiwe.

  KWELI ALIYEANZISHA USEMI WA MTEJA NI MFALME HAKUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA.
   
 16. s

  susu Member

  #16
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  It is wrong to share Ip adress and dont understand why they did that.guess customer should rise up since it breach of security for sharing and will be easy for hacker to catch it.
   
Loading...