iOS 17: Apple wameleta Contact poster. Kazi nzuri

iOS 17: Apple wameleta Contact poster. Kazi nzuri

Hii michezo tumefanya sana kwenye zile Nokia za Symbian, kitambo sana.
 
Samsung unaweka hata video ukitaka
Umenikumbusha, kuna lisimu la keypad lilikuwa linaitwa Oking linasauti kali.

Lile lisimu lilikuwa na uwezo wa kusevu video kama ringtone

Sasa kuna mwehu mmoja alisevu Movie ya kichina kama ringtone

Akipigwa simu utasikia sauti za mashaolin wanapigana halafu katikati ya mapigano unakuta wanapoa wanapiga stori kidogo afu wanaliamsha tena
 
Kivumbi leo 🤣🤣🤣🤣
😀😀 basi kuna namna tunamix files.
Kama ni kuweka vipicha tunaweka kitambo tu.
Hii ya kuwaamsha wenye Android waje kusema ni marudio, me nasubirii itoke mu update mje kutupa tofauti.
 
Unaijua contact poster

Apple kwenye series mpya ya iOS ya 17 wameleta feature mpya inaitwa Contact poster uwezo wa kuweka picha za watu kwenye namba zao za simu.

View attachment 2649367

Contact poster inakupa uwezo wa ku customize namba Zako za simu ulizo zisave kwa kuweza kuweka picha zao kwenye namba pamoja na mabango zinazo muonyesha muhusika Fulani.

Ni feature nzuri sana kwani wakati unapiga simu utaweza kuona picha ya muhusika Ikiwa full tena yenye kupendeza kama Bango kupitia simu yako.

Labda unampigia simu mama yako , baba, mchumba au rafiki nk kwenye kioo chako kitatokea picha yake Ikiwa na mfumo mzuri wa kupendeza ni feature nzuri sana inapatikana kwa watumiaji wa iOS ya 17.

Jinsi ya kuseti kwa watumiaji wa beta version fanya hivi fungua app yako ya phone >> tafuta contact>>chagua user card >>chagua contact photo & poster chagua Editi

Kama ndo unafanya setting kwa mara ya Kwanza chagua customize >> utachagua kati ya contact poster au photo kwaiyo utaweza kuchagua toka kwenye camera, photos,memoji pamoja na monogram.
• camera >> utaweza kupiga picha live
• photo >> inakupa option ya kuchagua picha zilizopo kwenye simu
• memoji >>utaweza kuchagua avatar mbalimbali na kuweka kwenye namba
• monogram >> inakua mfumo wa ujumbe Ikiwa na style tofauti tofauti

Vip unaionaje hii feature kwenye simu yako ushaanza kutumia au lah tuachie maoni yako ?

View attachment 2649368View attachment 2649369
View attachment 2649366
Hii feature mbona nimeitumia zamani sana.android sony xperia sijui z1 au 2 miaka hiyo. Sio kitu cha kipekee wala kipya. Hata kwenye symbian pia.Apple huwa anachukua vtu vya zaman ana viimplement better na kisasa halafu anavipa majina mazuri kama vile jambo la ajabu. Sijui retina display, sijui dynamic island
 
Hii feature ni kwamba caller ndo anaset picha gani itokee Kwa watu kila akipiga cm , Kama Mimi napigiwa simu na mtu A, call ikiingia ntaona picha yake aliyoiset yeye kupitia cm yake Kwa anavyotaka aonekane Kwa watu .

That’s the difference [emoji115]
 
Mbona ya mda mrefu hii! Inamaana hao apple ndio wanafikia sasahivi!? Au sijaielewa au inatofauti gani au chaziada kipi ! kushinda hizi zingine !!?
 
Mbona ya mda mrefu hii! Inamaana hao apple ndio wanafikia sasahivi!? Au sijaielewa au inatofauti gani au chaziada kipi ! kushinda hizi zingine !!?
Soma uzi kwa makini
 
Hii feature ni kwamba caller ndo anaset picha gani itokee Kwa watu kila akipiga cm , Kama Mimi napigiwa simu na mtu A, call ikiingia ntaona picha yake aliyoiset yeye kupitia cm yake Kwa anavyotaka aonekane Kwa watu .

That’s the difference [emoji115]

Hapa sasa imeleta maana.
 
Niliwahi kutumia Nokia N73 ya zamani ilikuwa ya kuslide...ilikuwa na hii feature...
Ni miaka zaidi ya nane imepita sasa
 
Hii feature ni kwamba caller ndo anaset picha gani itokee Kwa watu kila akipiga cm , Kama Mimi napigiwa simu na mtu A, call ikiingia ntaona picha yake aliyoiset yeye kupitia cm yake Kwa anavyotaka aonekane Kwa watu .

That’s the difference [emoji115]
Nimekuelewa sanaa 😆
 
Back
Top Bottom