Inverter au Generator? Naomba ushauri wandugu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inverter au Generator? Naomba ushauri wandugu.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Tundapori, Apr 24, 2011.

 1. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kutokona na migao ya Stima (Umeme) isiyoisha Bongo ninaomba ushauri juu ya njia gani zaidi inakuwa bora kati ya Inverter au Generator kwa ajili ya Standby Power Source.
  Taja faida na hasara ya Inverter au Generator.
  Asanteni bandugu kwa misaada /Ushauri wenu.
  Paska njema.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Matumizi ya G ni lazima ujiimalishe ktk maswala ya mafuta ni gharama kwa upande mwinge ila inategemea na mfuko wako
  lakini ktk issue ya Inverter unaongelea maswala ya solar power-umeme jua,mala nyingi initial cost huwa ni kubwa sana ila baada ya hapo utafaidi umeme jua kwa mda mrefu pasipo kuingia gharama nyingine ulipaji bili na ununuaji wa mafuta,ingawaje inategemea na solar pannel utakazo funga hapa naongelea size za module zako

  ila umeme jua ndio wa uhakika zaidi hauto kupa mawazo sana
   
 3. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Asante engmtolera kwa ushauri mzuri.
  Actually nazungumzia kuhusu kuzicharge battery kwa kutumia umeme wa Tanesco bila kutumia solar panels.
   
 4. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ningependa kusikia majibu ya wataalamu kuliko kusema kwa kuwa sina amani sana na kile nachokifahamu. Basi ngoja niseme kidogo nikijuacho ila wataalam watanisahihisha nikikosea, nikizingatia kujibu swali ulilouliza.

  JENERETA
  FAIDA:

  1. Gharama ya kununua jenereta yaweza kuwa ndogo kuliko combination ya inverter na betri ikiwa tuta-assume umeme utaotolewa na Generator (G) uwe sawa na ule wa Inverter & Battery (I&B). Maana yake ni kuwa I&B kutoa umeme sawa na G (kwa maana ya idadi ya appliances zitazoweza kuwashwa) basi pesa ya kununua I&B itakuwa kubwa kuliko G. Utahitaji battery very powerful.
  2. G haihitaji kuchajiwa, ni mafuta tu. Matumizi ya mafuta kwa G si makubwa kivile, labda higher kidogo kuliko pikipiki. Kama mfuko si mbaya sana Gen inaweza kuwa affordable kwa ununuzi wa kwanza na matumizi yasiyokuwa ya mara kwa mara sana.
  HASARA

  1. Kelele. Druuuuuuuuuuuuu, Triiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!! Sasa hata muziki hatusikii vizuri, kelele kwa majirani. Nadhani kuna G zisizo na kelele lakini zitakuwa na bei kubwa. Wadau watatufahamisha hapa.
  2. Moshi. Risk za mambo ya Petrol na moto.
  3. Yaweza kuibwa kama haina ulinzi mzuri maana huwa tuna tabia ya kuweka nyuma ya nyumba kukwepa moshi na kelele.
  INVERTER
  FAIDA

  1. Hakuna kelele.
  2. Hakuna kununua mafuta kwa sababu battery zinachajiwa na umeme wa TANESCO wakati upo. Huenda ukalazimika kubadilisha "maji" ya battery katika kipindi cha labda mwaka mmoja kama battery inatumia maji. Zipo battery zisizotumia maji (Dry cells) na wauzaji wanadai zinaweza kukaa miaka hadi mitano kabla ya kuchoka kabisa na kuhitaji kununua nyingine, so dry cells hakuna mambo ya kumwaga maji. Bora kununua dry cells.
  HASARA

  1. Bei kubwa (labda laki 5 na ushee) kupata vyote battery na inverter vyenye kiwango kinachokubalika angalau kuwasha taa mbili tatu za energy saver, computer, TV na redio. Nilimuuliza mtu mmoja akaniambia kwa vifaa nilivyovitaja battery yenye nguvu (alisema N200 hadi N300 hivi) yaweza kuwasha hadi 8 hrs mfululizo kabla ya kuhitaji kuchajiwa tena lakini kwa matumizi madogo ya TV na taa siku mbili tatu zaweza kufika kwa matumizi yasiyo ya mfululizo sana, sina ushahidi.
  2. TANESCO wasipowasha umeme for some days itabidi usubiri hadi warudishe ndipo ucharge battery yako, hakuna kununua petroli ya dharura. Lakini nadhani ni rare kwa umeme kukatika muda mrefu kiasi cha siku mbili au zaidi.
  Hivyo ningeulizwa nishauri nini cha kununua kama pesa ya awali si tatizo, ningeshauri Inverter. Generator ni kama umeme mkubwa (idadi ya appliances) unahitajika na kuna mazingira yanayosapoti eg kukwepa kelele, moshi, wizi na pesa ya mafuta.

  Wadau watanisahihisha na kuchangia zaidi. Umeme kukatika ovyo ovyo kunaniathiri sana. Tena sana.
   
 5. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  D. Asante
  Hapo kwa udondoaji wako wa haya maswala kweli umenigusa. Naanza kuuona mwanga taratibu.
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kama ni matumizi madogo ya nyumbani kwa taa, fridge na TV gor for an inverter!!!

  Tiba
   
 7. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Ni kwa matumizi ya nyumbani tu. Kwa ajili ya taa za energy savers 30, tv 2, fridge 1 na freezer 1.
   
 8. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  inverter zinauzwa wap?
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo fridge yako ina power rating gani? Maana nijuavyo mimi, fridge huwezi ukaiweka katika class la appliances zenye matumizi madogo, labda useme ya wastani. Na hata power ya inverter sidhani kama inaweza kuendesha fridge ya kawaida. Typical rating za fridge ni 400W na kuendelea!
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa na Generator kwa miaka 5 sasa lakini pia nimenunua inverter kwa ajili ya incubator ya watts 120 nimeona tofauti kidogo. Nashauri kama una fedha bora nunua inverter kwani haina kelele na hutahitaji kununua petrol mara kwa mara.

  Nimeshindwa ku run G kwa sababu mafuta yanapanda na ukiwasha generator kwa masaa 4 lazima itatumia lita 2 na nusu za petrol ila inverter ukishaicharge kwa charger ya volt 12 unatumia kirahisi.
  Ila nashauri kama unataka kununua inverter kwa ajili ya matumizi ya nyumba nzima nunua ya watts 2000 ambayo ni kwenye laki 750,000 na betri yake laki 200 na charger laki na 30 hivi. kama umeme haukatiki zaidi ya mara moja kwa wiki hamna haja ya kununua solar. Ila kama unakatika kuanzia siku 3 hadi 4 kwa wiki ni bora ununue solar kwani hutaweza ku charge na kutumia.
   
Loading...