Interview Zimejaa Uonevu Na Upendeleo Mkubwa

Jul 13, 2012
13
3
Kumekuwa na wimbi kubwa la kuwalazimisha watu kuajiriwa kwa kinyume na baadhi ya haki za binadamu. Kwa mfano mtu anaitwa kwenye interview halafu huko.

Nadhani unatakiwa huu uwe wakati wa interiew zichunguzwe kama zinakidhi masharti ya kisheria hapa nchini. Kwamba interview inapofanyika basi awepo afisa wa wizara inayohusika na usimamizi wa sheria ya kazi (Labour Law).

Au kuwe na utaratibu wowote kuhakikisha kwamba interview ilikuwa ya haki kulingana na sheria yetu na ilikidhi vigezo vya sheria zetu za kazi, na mamlaka zinazosimamia sheria hii zijue.

Hii itasaidia ukiukwaji fulani unaotokana na serikali kujitoa kufuatilia kinachoendelea kati ya waajiri na waajiriwa.

Baadhi ya maswali kwenye interview yanaelekea kabisa kukiuka sheria ya kazi. Mfano mtu anaulizwa kwamba je, pamoja na kuwa na kazi zako je ukipewa kazi ya mtu mwingine utalalamika au utakataa?

Ukweli sheria haiko hivyo maana unachotakiwa ni kukataa kama hakuna malipo ya ziada. Huwezi kufanya kazi zako halafu uongezewe ya mtu au watu wengine halafu usione kuwa mzigo umeongezeka halafu eti uendelee kukaa kimya.

Lakini kwa ufinyu wa ajira ambao serikali inaujua, unadhani ni nani katika interview atajibu kwamba sintakubali kuongezewa mzigo wa kazi zingine. Matokeo yake ni kwamba karibu kila mmoja wetu anajikuta kulazimika kujibu kwamba anakubali.

Matokeo yake unajikuta unaanza kazi kweli una list ya kazi zako kisheria lakini unaongezewa kazi za ziada bila ya makubaliano. Ukiuliza unabanwa kwamba ulikubali hivyo siku ya interview.

Hivyo, naona ni wakati wa serikali kuliingilia hili maana haina maana kusema ajira zipo wakati serikali ikifanya uchunguzi makini kwa namna hii ni kama ajira hazipo.

Jadili
 
Huu ni uzembe huna mazoea ya kufanya kazi au competence yako kwenye kazi unazopewa ina walakini ,maana haiingii akilini boss wako aku overwork kiasi hicho.Wabongo mnalilia ajira mkipewa ajira mnaanza matatizo .Sijui mkoje nyie, ndo maana wenzetu Kenya, Uganda wame occupy nafasi nyingi nchini mwetu ambazo sisi wenyewe tulipaswa tuwepo
 
Back
Top Bottom