Unaweza kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.
Na kuna njia nyingi za kufanya hivyo. Hapa naomba nikushirikishe moja ambayo unaweza kuifanya popote ulipo bila ya kuharibu ratiba za kile unachofanya sasa.
ANZISHA BLOG, na ninaposema blog simaanishi uanzishe blog ya kuripoti udaku au habari, hapana, hapa nakuambia uanzishe proffesional blog. Blog ambayo utaitumia kutoa suluhisho la matatizo ya watu kilingana na ujuzi, taaluma, uzoefu wa kitu chochote ambacho unajua au unapend akufuatilia.
Baada ya kukuza blog yako, unawez akuwatumia wasomaji wako kuwauzia huduma nyingine ambazo zitakuingizia wewe kipato. Kama huduma za ushauri, vitabu, kozi na vingine vingi.
ANGALIZO; Njia hii sio ya haraka na inahitaji ujitoe kwa kile utakachokuwa unaandikia, ukitenga saa moja kila siku kuandika na kuwashirikisha watu baada ya muda utapata wasomaji wa uhakika na kuendelea kuikuza.
Kama utataka kujifunza zaidi kuhusiana na blog
BONYEZA HAYA MAANDISHI UTAPATA MAELEZO MAZURI ZAIDI.
Nikutakie kila la kheri.