Internet exploler imevunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Internet exploler imevunjika

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Chibidu, May 11, 2012.

 1. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani kuna mtoto amepinda mpaka basi! amenichekesha, amemdai dingi yake amnunulie vitu kibao. Ngoja na nyie niwachekeshe kabla JF haija collapse usiku huu.
  Huyo mtoto yuko sekondari, akampigia simu dingi yake ili ampe bili anayodaiwa huko shule. Dogo bila kumpa dingi nafasi ya kuuliza maswali akaanza;
  " Dady skuli tunatakiwa kununua twitter, harafu kuna kitabu mwalimu katuambia tukanunue kinaitwa facebook".
  Dingi akauliza hicho kitabu kinauzwa shilingi ngapi?"
  Dogo akajibu " shing efu tisa"
  Kisha dogo akaunganishia "afu dady, nimeenda hospital daktari kaniambia meno yangu yana bluetooth, kwahiyo nadaiwa shing efu selasini kwa hiyo naomba nitumie haraka"
  Dingi kijasho kikaanza kumtoka akamsisitizia "sasa jitahidi kusoma kwa bidii, si unaona gharama zilivyokubwa mwanangu?"
  Dogo likadakia "afu baba nilisahau internet exploler yangu imevunjika, ila nintendo yake bado nzima kwahiyo naomba niongezee efu ishirini na ile WiFi yangu imeharibika, yenyewe ni shingi efu kumi tu. Kwahiyo naomba nitumie kwa m-pesa leo leo". Dingi kijasho kikamtoka ikabidi akate simu tu.
  Du toto balazuli hili.
  Jamani usiku mwema ngoja nikalale. Asante kwa ancle pochipochi wa radio wani kwa kuniandaa kwa usingizi kwa hiki kichekesho chako.
   
 2. driller

  driller JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1,119
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  teh teh kwani wewe hujawahi kudanganya kwenu..!? na huyo dingi kweli ni kiazi..!
   
 3. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  nimecheka niaje!
   
 4. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi nilipokuwa F2 nilikuwa namdanganya dingi kuwa tunatakiwa kwenda na hela za basenburner na za amoeba.
  Za basenbuner alinipa. Niliporudi term nyingine kuomba hela za amoeba akanistukia maana kuna siku alienda hospitali akiwa anaumwa tumbo daktari akamwambia anaugua amiba (amoeba). Nikaumbuka
   
Loading...