INTERNET BUNDLES: Vodacom Vs Tigo Vs Airtel Vs Halotel

INTERNET BUNDLES: Vodacom Vs Tigo Vs Airtel Vs Halotel

Vodacom sio kweli mimi natumia voda kwaajili ya internet tu

Nikijiunga gb1 naweza kuangalia video siku. Nzima huwa najiunga saa nne usiku mpaka saa nne usiku ,hapo natizama videos na mambo kibao

Kuhusu spidi hakuna shaka voda ndio inayoongoza kuliko mitandao yote ndio maana binafsi na line ya voda ila kwaajili ya net tu

Tatizo kubwa ya voda ni gharama ila kwa internet hawana mpinzani utafiti nimeufanya kwa dar tu

Gharama ndogo nahisi halotel kama hawajapandisha
Kwa gharama unazotumia kununua hiyo gb 1 kwenye voda. Kwa ttcl unapata mara 2.

Kuhusu speed labda ufafanue. Kwa mjini hasa Dar TTCL HANA MPINZANI maana speed yake ni mara 3 ya huyo voda na mara 5 ya wengine.

Amini nakuambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vodacom sio kweli mimi natumia voda kwaajili ya internet tu

Nikijiunga gb1 naweza kuangalia video siku. Nzima huwa najiunga saa nne usiku mpaka saa nne usiku ,hapo natizama videos na mambo kibao

Kuhusu spidi hakuna shaka voda ndio inayoongoza kuliko mitandao yote ndio maana binafsi na line ya voda ila kwaajili ya net tu

Tatizo kubwa ya voda ni gharama ila kwa internet hawana mpinzani utafiti nimeufanya kwa dar tu

Gharama ndogo nahisi halotel kama hawajapandisha
Gharama na speed jaribu TTCL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nipo na halotel, niliwakubali mapema sana tokana na kasi ya internet yao na gharama zao kuwa chini ila kwa sasa hapana.

Halotel wamebobea katika wizi wa kimtandao kuliko unavyoweza kufikiri. Ni usanii sana kutuuzia mb bei rahisi halafu zinaisha haraka mno. Zile MB600 za week mwanzoni zilikuwa zinakaa hadi siku 4 kwa kuperuzi, kudownload na ku stream. Leo hii wamezipunguza unapata mb500 ambazo zikimaliza masaa 24 unashukuru mungu. Something is wrong somewhere sio bure.

Pia kingine nachoshangaa huwa nikiingia youtube sikuhizi ni kosa. Yani hata kama nilijiunga bundle lile la GB 1.2 la week nikasema niangalie video mpya ziliotoka labda video 3 tu, nakuwa nimeshajiandaa kisaikolojia kuambiwa nina MB 5 zimebaki baada ya masaa kadhaa kupita.
Eti nakuwa nimeshajiandaa kisaikolojia.
 
Airtel nakiri ndio wenye vifurushi vya uhakika ila mtandao upo chini hadi ladha ya vile vifurushi inakuwa haipo tena yaani
 
Back
Top Bottom