Guys am honestly speaking on this. Mm ni mtumiahi wa juu sana wa internet. Kwa wiki natumia Kuanzia GB 100 na kuendelea. Hivyo nahitaji mtandao wa bei nafuu na kasi ili kufanikisha biashara zangu
TiGO. Hawa jamaa wana mtqndao mzuri kwenye baadhi ya maeneo ambayo wana amini yana potential customers. Kama mlimani city. Posta .masaki. Na sehemu muhimu hapa dar. Kwa mikoani sijui
AIRTEL. Hawa jamaa wana vifurushi vikubwa vya bei rahisi sana hasa kama una tumia vocha za UNI. Mtandao wao ni wa kawaida sanaa na pia una kera kama unahitaji spidi. Kwa watu wanaotumia net kwenye sim kwa ajili ya kubrowse na kudownload files ndogo hawezi ku experience hili tatizo
HALOTEL. hawa jamaa wanatumiwa na watu waliochoshwa na huduma za Tigo airtel na voda. Mtandao wao hauna consistency. Leo upo vizuri kesho hamna kitu. Kwa dsm hali ni mbaya sana sasa hivi. Ila juzi nilikua morogoro mjini mtandao upo vizuri kabisa
TTCL. Hawa jamaa wana mtandao wa kasi sana hasa ukiwa baadhi ya maeneo. Ila mtandao wao unakatakata sana hawana stability kabisa. Pia hawa jamaa hawana 2g hivyo basi 4g na 3g zikishake tuu mtandao unakatika kabisa no network hadi utakapo kaa sawa
VODACOM. hawa jamaa nawaheshimu sana. Wanajua nn wanacho kifanya. Mtandao wao upo kasi sana mjini na vijijini. Ukiwa na Edge (E) ya voda unaweza fanya kazi kama kawida utandhani una 3G ya tigo au airtel. Pia 4G yao ni balaa la kutishaaa. Mimi huwa nadoenload hadi MB 7 kwa sekunde 1. Kitu ambacho sijawahi kukiona hapa bongo.
Pia kuna mtandao kama smile. Nasikia net yao ipo poa ila wana bei kubwa ya bandles pia hawana huduma ya sms na voice calls.
Mitandao mingine kama Smart sina experience nao maana hata hawajitangazi
Ikifika weekend lazima zifike GB 100
NOTE: Natumia internet ya vodacom. Though nimechakachua modem ya Airtel soooooo imekua multipurpose
Sent using
Jamii Forums mobile app