International Friendly - Namibia vs Tanzania

Magoli yote ya mchezo yamefungwa na wachezaji wa Namibia..

Stars ambayo ilitangulia kupata bao dk ya 89 kuelekea dk ya 90 kwa mchezaji Emilio Martin wa Namibia kujifunga mwenyewe.

Kwenye dakika za majeruhi Namibia wakafanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Penduleni Nekundi.
 
Taifa Stars imeinyuka Namibia jioni hii kwa bao 1-0 nyumbani kwao Jijini Windhoek katika mfululizo wa FIFA Friendlies. Katika michezo mingine ya ukanda wa jirani, Zambia imeitandika Uganda 2-1; Zimbabwe 4 Malawi 1; Burundi 1 Rwanda 1; Msumbiji 1 Angola 1 wakati kama wengi mnavyojua Sauzi wametandikwa bila huruma 5-0 na Wabrazil! Afadhali hata sisi tulipata bao 1 mwaka 2010 tuliponyukwa 5 uwanja wa Taifa na jamaa hao Wabrazil.
 
Mbona wadau wanasema 1-1? na hata ikiwa 1-0 ndio kuduwaza? Kweli masikini akipata ile kitu ulia mbwata.
 
Rainford Kalaba yuko ndani ya kikosi cha Zambia dhidi ya Uganda,Emma Okwi,Hamis Kiiza yuko ndani ya kikosi cha Uganda dhidi ya zambia leo.Kwanini Tanzania haina Ulimwengu na Samatta dhidi ya Namibia?
Flight connections zilishindikana kwa sababu wana mechi inawasubiri weekend.Kina Okwi na Kiiza imewezekana kwa sababu ya connection ya KQ.
 
Niliwahi kusema awali kuwa huu mchezo umeangukia kati kati ya kalenda ya champion league ya Afrika,complications ni nyingi kwenye kuunganisha ndege. By the way Masuke mbona huulizi kuhusu mwinyi kazimoto?
 
Dorogo kocha msaidizi unayemtaja ni Sylvester Marsh,anaumwa amelazwa,tumuombee.
 
Last edited by a moderator:
.... hizi ni mechi zipo ktk ratiba ya FIFA, timu hii imekwenda Namibia na Salum Madadi ambaye ni kaimu mkurugenzi wa ufundi wa TFF......Na timu hii imefanikiwa kufanya mazoezi siku moja tu.
Yale yale ... timu haina manager halafu imefanya mazoezi siku moja tu! Get serious, stop horsing around!
 
Mbana kuna uzi humu unaousiana na hyo mechi..ni namibia 0 tanzania 1
 
Stars hawajafunga goli ni namibia wamejifunga..hatuna timu kabusa,yaani bi aibuuu
 
Kwanza nimshukuru ndetichia kwa majibu then kuhudu timu hao walioenda sioni kama ndio key players wetu timu pale haija kamilika kama ambavyo tumeizoea walipoifikisha wamejitahidi pongezi zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…