Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,301
- 4,681
Ikicheza ndani ya Dakika 30 za mwisho huku wakiwa pungufu uwanjani Klabu yenye mafanikio kuliko klabu zote hapa Duniani yaani AC Milan imeweza kuwabamiza klabu ya Inter kwa goli moja kwa bila, goli lililowekwa kimiani kunako dakika ya 5 ya mchezo na jiwe kuu la pembeni ambalo waashi walilikataa yaani Zlatan Ibrahimovic.
Ktk mpambano huo ambao Inter ndio walikuwa wenyeji walijikuta wakipelekwa puta muda mwingi.
Kipindi cha pili dakika ya 60 ulimwengu ulishuhudia beki wa Milan Ignazio Abate akipewa kadi nyekundu kwa kosa la kumtendea madhambi Goran Pandev.
Washabiki wa Inter walionekana kuwa tofauti msimu huu baada ya kubeba mashuka makuubwa yenye ujumbe wa kupona haraka na kurudi uwanjani kwa mshambuliaji hatari ambaye ameweka rekodi mpya hivi karibuni Super Pippo Filipo Inzaghi mwenye miaka 37 ambaye ameumia vibaya, kitu kitachopelekea akae nje kwa msimu woote huu uliobaki.
Milan sasa wanaongoza Ligi huku Inter wakiwa nafasi ya Tano.