Inter 0-1 Milan...Ibra the Hero

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,302
4,681
Ikicheza ndani ya Dakika 30 za mwisho huku wakiwa pungufu uwanjani Klabu yenye mafanikio kuliko klabu zote hapa Duniani yaani AC Milan imeweza kuwabamiza klabu ya Inter kwa goli moja kwa bila, goli lililowekwa kimiani kunako dakika ya 5 ya mchezo na jiwe kuu la pembeni ambalo waashi walilikataa yaani Zlatan Ibrahimovic.

Ktk mpambano huo ambao Inter ndio walikuwa wenyeji walijikuta wakipelekwa puta muda mwingi.

Kipindi cha pili dakika ya 60 ulimwengu ulishuhudia beki wa Milan Ignazio Abate akipewa kadi nyekundu kwa kosa la kumtendea madhambi Goran Pandev.

Washabiki wa Inter walionekana kuwa tofauti msimu huu baada ya kubeba mashuka makuubwa yenye ujumbe wa kupona haraka na kurudi uwanjani kwa mshambuliaji hatari ambaye ameweka rekodi mpya hivi karibuni Super Pippo Filipo Inzaghi mwenye miaka 37 ambaye ameumia vibaya, kitu kitachopelekea akae nje kwa msimu woote huu uliobaki.

Milan sasa wanaongoza Ligi huku Inter wakiwa nafasi ya Tano.
 
Thanks GC kwa habari... Vipi Rafa huko hakuwalaumu Gillet and Hicks?
 
thread ya Rosonelli ama Diavolo ipo njiani na wiki hii itakuwa Hewani.
Nawaahidi wakuu.
 
hongereni mashabiki wa AC MILAN kwa ushindi wa derby della madonninna ila nathubutu kusema mwisho wa msimu ndoo ni kwa AJUZA WA TURIN.......
 
Mbon Al-Jazeera leo asubuhi imesema wametoka sare bila ya kufungana na A.C Milan sasa waongoza ligi..................What is happening?
 
Mbon Al-Jazeera leo asubuhi imesema wametoka sare bila ya kufungana na A.C Milan sasa waongoza ligi..................What is happening?

Achana na Al-jazeera weweee.
Wale wanachojuwa ni habari za milipuko tu.
Milan wanaongoza ligi na hao Inter jana wamepodolewa mixer kupaka hina...
 
hongereni mashabiki wa AC MILAN kwa ushindi wa derby della madonninna ila nathubutu kusema mwisho wa msimu ndoo ni kwa AJUZA WA TURIN.......

Juve hawawezi kuchukua ubingwa bila Luciano Moggi...
Subiri msimu ujao akifunguliwa ndo muanze kuchukua vikombe.
 
inzaghi the legend

Inzaghi ndie mshambuliaji wangu booora kabisa Duniani.
Na ktk thread ya AC Milan ambayo iko ktk maandalizi ya mwisho kabisa kabla haijarushwa hapa JF amepewa nafasi kuubwa sana ya kuzungumziwa.

Pippo kaumia, lakini amesema wazi kuwa atarudi uwanjani na atafunga magoli kama kawa.

Kwa kukusaidia tu ni kuwa Pippo keshawafunga Manchester UTD magoli mawili, Bayern magoli mawili, Liverfool magoli mawili, na Madrid magoli mawili na magoli hayo huyafunga ktk mechi moja...

Nani kama Pippo?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom