Intelligent woman (Mwanamke mwerevu)

Intelligent woman (Mwanamke mwerevu)

livewise1

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2019
Posts
837
Reaction score
972
[emoji109] JF mambers!

Mwanamke mwerevu akikupenda, anakuchunguza upo vipi!? Unapenda ujinga ujinga au hupendi!
Vile ulivyo, kama unapenda ujinga ujinga anakuja kwa staili hiyo hiyo ili akunase...kama hupendi anakuja kistaarabu ili akunase pia.
Akisha kunasa ...anakukoleza baadae anapindua meza kibabe!!!

Ku step out ndio suala ambalo litakuwa ndio strength yako (ukiweza) au weakness yako ukishindwa.[emoji28]

Homeboy mmoja alikuwa anataka kuowa mwanamke ambaye anajitambua na kujua nini maisha.
Akaja bibie mmoja ambae amezalishwa na jamaa akatelekezwa mpaka leo (watu wa kigoma kesi yenu hii)
Akajieleza kistaarabu kwa vile jamaa amejiweka kiustadhi mstaarabu mtaani kwao na mpaka baadhi walimsifia alipokuwa akisema anataka mke mwenye uwerevu na maisha anayajua.

Huyu bibie anajua kuwa jamaa ana mtoto ambaye mama yake ni marehemu (ustadhi alifiwa na mkewe kipindi cha korona19)
Jamaa akaona mke ni huyu sasa, akaowa na wamezaa mtoto mmoja. Hivyo jumla pakawa na watoto 3, wa jamaa na wawili wa mkewe.
Hivi majuzi jamaa amepagawa mkewe amemwambia hataki kuishi na mwanae (wa marehemu) kama vipi ampeleke kwa bibi yake.
Wakati huo huo mwanamke analazimisha mtoto wake wa kwanza ubini uwe wa mumewe wa sasa(abadilishiwe jina la baba eti kisa mwanamke anasema hataki kuliskia jina la babake maana alimtelekeza)
Rangi halisi ya mke imeanza kuonekana...

Baada ya jamaa kumrudisha mwanae kwa bibi ake..mke mahaba kama yote kwa jamaa na kujibebisha!!
Jamaa akamwambia NATAKA KUOWA MKE WA PILI AMBAYE ATAISHI NA MWANANGU ULIYEMKATAA. Na ameamua kumuowa rafiki mkubwa sana wa mkewe maana alionesha huruma aliposkia rafiki yake hataki kuishi na mtoto wa mume, akamshauri lakini waapi...
Timbwili lake mpaka saivi jamaa anashinda kijiweni tu...mida mibovu ndio anarudi.

Nimemwambia afanye kile anaona ni sahihi kwake maana pale kesha nasa na meza ishapinduliwa!!

NB: [mwerevu imetumika tu kama camouflage term]
 
Mimi siku zote huwa nasema,sifa za mtu unayemtaka ziwe moyoni mwako, ukikutana na mtu unajua huyu anazo unajisogeza au hana uachane nae. Masuala ya kujitangazia nataka mwanamke/mwanaume wa hivi mara vile utaishia kukutana na waigizaji wa kiwango cha Hollywood yakakukuta ya mtoa mada

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli
 
Muhuni kapindua meza, mpemba chaliiiii.
Yaani kuna wanawake akili zao wanazijua wenyewe, sasa huyo single mama amepata sehemu ya kustirika badala akae kwa kutulia analeta upuuzi wake.
Sema watu hawakumbuki fadhila...keshasahau
 
[emoji109] JF mambers!
Mwanamke mwerevu akikupenda, anakuchunguza upo vipi!? Unapenda ujinga ujinga au hupendi!
Vile ulivyo, kama unapenda ujinga ujinga anakuja kwa staili hiyo hiyo ili akunase...kama hupendi anakuja kistaarabu ili akunase pia.
Akisha kunasa ...anakukoleza baadae anapindua meza kibabe!!!
Ku step out ndio suala ambalo litakuwa ndio strength yako (ukiweza) au weakness yako ukishindwa.[emoji28]

Homeboy mmoja alikuwa anataka kuowa mwanamke ambaye anajitambua na kujua nini maisha.
Akaja bibie mmoja ambae amezalishwa na jamaa akatelekezwa mpaka leo (watu wa kigoma kesi yenu hii)
Akajieleza kistaarabu kwa vile jamaa amejiweka kiustadhi mstaarabu mtaani kwao na mpaka baadhi walimsifia alipokuwa akisema anataka mke mwenye uwerevu na maisha anayajua.

Huyu bibie anajua kuwa jamaa ana mtoto ambaye mama yake ni marehemu (ustadhi alifiwa na mkewe kipindi cha korona19)
Jamaa akaona mke ni huyu sasa, akaowa na wamezaa mtoto mmoja. Hivyo jumla pakawa na watoto 3, wa jamaa na wawili wa mkewe.
Hivi majuzi jamaa amepagawa mkewe amemwambia hataki kuishi na mwanae (wa marehemu) kama vipi ampeleke kwa bibi yake.
Wakati huo huo mwanamke analazimisha mtoto wake wa kwanza ubini uwe wa mumewe wa sasa(abadilishiwe jina la baba eti kisa mwanamke anasema hataki kuliskia jina la babake maana alimtelekeza)
Rangi halisi ya mke imeanza kuonekana...

Baada ya jamaa kumrudisha mwanae kwa bibi ake..mke mahaba kama yote kwa jamaa na kujibebisha!!
Jamaa akamwambia NATAKA KUOWA MKE WA PILI AMBAYE ATAISHI NA MWANANGU ULIYEMKATAA. Na ameamua kumuowa rafiki mkubwa sana wa mkewe maana alionesha huruma aliposkia rafiki yake hataki kuishi na mtoto wa mume, akamshauri lakini waapi...
Timbwili lake mpaka saivi jamaa anashinda kijiweni tu...mida mibovu ndio anarudi.

Nimemwambia afanye kile anaona ni sahihi kwake maana pale kesha nasa na meza ishapinduliwa!!

NB: [mwerevu imetumika tu kama camouflage term]
Je anayetumia chupa ya soda anaweza kuwa mke bora?
 
Back
Top Bottom