Intelligensia juu ya Mabomu ya Arusha

melchior

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
230
214
Let us think inside the box, outside the box and trash the box and think without a box as well.

Inside the box

CCM wamepanga njama ya kulipua bomu kwenye mkutano wa CHADEMA ili wananchi waogope kuhudhulia mikutano ya chadema. Tuhuma hizi zinakuzwa na maneno ya Mwigulu Nchemba ambaye katika mikutano yake alionya kwamba watakaohudhulia mikutano ya chadema watakufa pamoja.Pia vifo vilivyofanya na polisi kwenye mikutano ya CHADEMA huko morogoro na iringa pamoja na utekwaji na uteswaji wa Ulimboka na wengineo vinafanya watu wengi ikiwamo viongozi wa CHADEMA waamini kuwa CCM ilitumia polisi kufanya hujuma hizi.

LAKINI, kwanini yalipuliwe siku ambayo ni mwisho wa kampeni?Lengo lingekuwa ni kuwatisha wananchi wasihudhulie mikutano ya chadema basi bila shaka bomu lingelipuliwa mwanzoni kabisa mwa kampeni.

Outside the box

Kuna wengine wanaamini CHADEMA wamejilipua wenyewe ili kutafuta umaarufu na huruma ya wapiga kura pamoja na kuipaka matope serikali ya CCM pamoja na jeshi lake. Fikra hii inachukuliwa kwa uzitio kwani hata katibu mwenezi wa CCM Nape Mnauye katika tarifa yake kwa vyombo vya habari anatuaminisha hivyo.

LAKINI, kiongozi gani yupo tayari kumwaga damu kwani tunaambiwa bomu lililipuka jirani na jukwaa kuu na miongoni mwa waliokufa ni kiongozi wa CHADEMA. Isitoshe kulikuwa na mpango wa kutengeneza mlipuko mkubwa zaidi ambao ungeleta madhala zaidi kwani Tenki la mafuta la gari la matangazo lilikutwa limepigwa risasi kwa mategemeo lingelipuka.

Trash the box and think without the box

Mimi nafikiri kuna mtu/ kikundi cha tatu ambacho tunatakiwa tukiweke kwenye tafakari zetu wakati tunamtafuta mchawi katika hili. Kikundi hiki kinaweza kuwa ndani ya nchi ama hata nje ya nchi. Tujiulize je ndani ya nchi kuna kikundi kinapenda kuona CHADEMA na CCM kwenye malumbano? Je kuna kikundi ama mashirika ndani ya nchi hakipendi kuona watanzania tunaishi kwa amani? Je kuna Vikundi vya nje ama nchi za nje ambazo hazipendi kuona watanzania tunaishi kwa amani? Je kuna nchi ama vikundi tuna uhasama navyo?

Ndai ya nchi sina uhakika kama kuna kikundi ama chama cha siasa kisichopenda kuona CCM na CHADEMA wakilumbana ama kinachopenda tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, labda TISS watakuwa wanajua. Kuhusu vikundi nchi za nje ambavyo vina uadui na Tanzania, nina uhakika na M23. Kikundi hiki cha wanamgambo wanaopigana Congo ambao inaaminika wanafadhiliwa na serikali za Rwanda na Uganda havijafurahishwa na hatua ya serikali ya Tanzania kupeleka majesi yake kwenda kulinda amani Congo. Sijui vikundi vingine nadhani TISS wana idadi ya ya vikundi tulio na uadui navyo.

Kuhusu nchi pia nina uhakika kwamba tuna uadui na Malawi kutokana na mgogoro wa mipaka kule ziwa nyasa. Pia nina uhakika tuna uhasama na Rwanda na Uganda kwakuwa tumeingilia Maslahi yao kwa kupeleka majeshi Congo. Sina uhakika na nchi nyingine ila nadhani TISS watakuwa wanajuia nchi ambazo tuna uhasama nao kwasababu ndio kazi yao , ingawa Kenya lazima tutakuwa na uhasama nao kwenye masuala ya kibiashara.

Kwanini natilia mashaka vikundi vya nje ya nchi ama nchi majirani zetu?

Kwasababu aina ya bomu lililolipuka katika kanisa la Joseph mfanyakazi Olasiti ni ile ile iliyolipuka katika mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA. Ni bomu la kiwandani na limetengenezwa China. Mabomu haya ni kwaajili ya majeshi sio polisi. Ikumbukwe kipindi kile bomu lilipolipuka kanisani , kulikuwa na Tension kubwa sana kati waislam na wakristo. Motive ya mlipuaji ilikuwa ku spark vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakristo na waislam. Hii ilishindikana baada ya wakristo kuendelea kuonyesha uvumilivu pia ilikuja gundulika kwamba mtu aliyerusha bomu ni mkristo mwenzao. Nadhani dhamira ya kikundi ama nchi iliyotaka tuingie katika Mapambano ya wenyewe kwa wenyewe ili fail.

Wakati huu ambapo kulikuwa na Tension kubwa kati ya mahasimu wa siasa CCM na CHADEMA hapa Arusha tunaona hali hii inajirudia. Motive ni ile ile ya kutaka tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, wakati huu katu ya wafuasi wa CHADEMA na CCM.
Viongozi wetu wanatakiwa wawe makini sana wanapotoamatamko yao kwani tukianza kuuana hakuna atakayepona. Kwamfano kakukuwa na haja ya Mh Lukuvi ama Nape kutoa matamko ya namna ile ama jeshi la polisi kuzuia wafuasi wa CHADEMA kufanya maombolezo ya wafuasi wao waliouawa katika mlipuko.

Halikadhalika hakukuwa na sababu ya viongozi wa CHADEMA kuwatuhumu polisi moja kwa moja kabla ya kuwa na uhakika wa kinachoendelea kwani wakati wa matukio kama ya uchaguzi polisi huwa wanaletwa toka kila kona ya Tanzania kwahiyo sio rahisi polisi walio katika scene kujuana, kitu kinachoweza kutoa mwanya kwa wahalifu ku camouflage kama police na kutekeleza adhma yao(kumbuka tunaambiwa polisi walimtorosha mrusha bomu je tuna uhakika ni polisi wetu, ama ni agents wa maadui zetu?).
NB; Rejea maneno ya rais wa Rwanda baada ya hizi kash kash aliposema Kikwete Kikwete anajidai kupatanisha nchi za wenzake wakati kwake kumshinda.

Pia bomu la kanisani lililipuka pindi tu askari wetu walipokuwa deployed kwenda rwanda;Rejea maneno ya M23 kwenye mitandao yao ;ikumbukwe kenyan hawafurahishwi na our mega development projects kama za ujenzi na upanuaji wa bandari zetu, na reli utajiri wa gas, ujenzi wa bomba na impact zake katika uchumi hapo baadae n.k.


Sina Chama

Naomba kuwasilisha.
 
That has to be the most pointless per thoughts pored into it because no matter how hard you think, and no matter how hard you try to convince people, and no matter how passionately you believe
 
That has to be the most pointless per thoughts pored into it because no matter how hard you think, and no matter how hard you try to convince people, and no matter how passionately you believe

There was no need of quoting the whole thread!
 
Sina Chama...Naomba kuwasilish
Kwa comment yako hiyo ya mwisho umejivua nguo na kubaki uchi; huna chama, so what! Hii yako ni red herring kwani swala la nani walihusika liko wazi wala halina mjadala!
 
mwanzo nilikua nadhani mabomu yale ni siasa au dini. Kwa sasa nimeamini si chadema si ccm si wa kristo wala si waislamu wanaohusika na mabomu haya. Ni njama za jirani zetu. Jiulizeni kwa nini mabomu hayalipuki Sumbawanga au Songea? Ni Zanzbar na Arusha tu!
 
That has to be the most pointless per thoughts pored into it because no matter how hard you think, and no matter how hard you try to convince people, and no matter how passionately you believe

Have you read and understood the whole article.....
 
Naomba mnisamehe kwa kuwa nadokeza umbea wenye ukweli.
Kwamba siku za milipuko ya bomu darajani Zanzibar siku chache silizopita, siku hizo walikuwepo Wakenya waliofanana na watu wa Usalama na walikaa katika mahoteli maeneo hayo ya Dajani.
Nadokeza tu.
 
Mkuu naamini Kenya inaifanyia hujuma kubwa Tanzania,bahati mbaya serekali imelala usingizi mzito.

Naomba mnisamehe kwa kuwa nadokeza umbea wenye ukweli.
Kwamba siku za milipuko ya bomu darajani Zanzibar siku chache silizopita, siku hizo walikuwepo Wakenya waliofanana na watu wa Usalama na walikaa katika mahoteli maeneo hayo ya Dajani.
Nadokeza tu.
 
Mkuu naamini Kenya inaifanyia hujuma kubwa Tanzania,bahati mbaya serekali imelala usingizi mzito.
Hivi ni kwanini tu wepesi wa kupeleka vidole kwa nchi nyingine? Je, usalama si suaka la serikali kulifanyia kazi? Serikali dhaifu imefanya hata utendaji wa taasisi nyeti kuwa dhaifu na kutowajibika. Muda mwingi vyomba vyetu vya usalama vipo busy na wapinzani, sijui lini hawa viongozi wetu wataamka toka usingizi huu wa uzembe na ujinga.
 
Naomba mnisamehe kwa kuwa nadokeza umbea wenye ukweli.
Kwamba siku za milipuko ya bomu darajani Zanzibar siku chache silizopita, siku hizo walikuwepo Wakenya waliofanana na watu wa Usalama na walikaa katika mahoteli maeneo hayo ya Dajani.
Nadokeza tu.

Mkuu,makanisa na biashara ya Watanganyika zinachomwa na Wakenya? Mapadri walio uliwa nao ni Wakenya??
 
mwanzo nilikua nadhani mabomu yale ni siasa au dini. Kwa sasa nimeamini si chadema si ccm si wa kristo wala si waislamu wanaohusika na mabomu haya. Ni njama za jirani zetu. Jiulizeni kwa nini mabomu hayalipuki Sumbawanga au Songea? Ni Zanzbar na Arusha tu!

Wakenya walilipua uzinduzi wa Kanisa Katoliki ili wapate manufaa gani ktk eneo ambalo moja ya Wageni walio kuwa wamehudhuria ni Viongozi wa Kanisa toka Kenya??
 
kamanda kova na big boss hivii hii intelijensia yenu inafanyaga kazi chadema tu wanapotaka kuongea na wananchiii? Sasa inakuwaje kwenye hii milipuko ya mabomu hatusikii intelijensia imefanya kazi au ndiooooo naniliuuuu??????
 
Mkuu kwa hiyo hata CDM sasa wana amini mkutano wao ulilipuliwa na Wakenya??
serikali inawajua wahusika wote kwani kikwete alikataa kuunda tume ya majaji ili ukweli uwekwe wazi mpaka leo amenyamaza kimya kwa sababu wahusika ni makada wa ccm tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa raisi pamoja na wabunge wa ccm tutaendelea kuwalaani kwa kuawa watu wasiokuwa na hatia na haya mabomu arusha kila siku mnataka nn
 
Nafikiri ni Zanzibar au Arusha kwa sababu ni rahisi kuingia na kutoroka baada ya kutenda uhalifu kwa maeneo kama iringa mhalifu anaona kuna uwezekano wa kukamatwa.
 
Back
Top Bottom