Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,499
- 34,560
Ni wiki tatu zimepita tangu nishiriki kikao cha maendeleo baraza la Kata ambacho mimi ni member wake kisheria.
Mojawapo ya waalikwa walikuwa ni wakuu wa shule zilizopo katika Kata yetu hii. katika uwasilishaji wa waalimu hao kitu tulichogundua ni kuwa mkakati wa kutoa elimu bure unaelekea kuvuruga tasnia ya elimu nchini. Kasma zilizopelekwa mashuleni zimefika zikiwa na masharti.
Katika masharti ama mgawanyo wa fedha hizo hakuna fungu la kulipia huduma zifuatazo
Hayo ni machache ambayo niliyaokota katika kikao kile. Niliamua kufanya utafiti mdogo katika kata na wilaya zingine kuona kama tatizo ni lile lile. Hivyo nikagundua kuwa utaratibu huu unakanganya mno. Kuna mwalimu mmoja wa taaluma alinieleza kuwa baadhi ya wazazi waliopeleka vijana wao kwenye usaili wa kidato cha kwanza walitaka shule iwapatie fedha za kulipia "medical examination" za watoto wao. tena wengine walisisitiza kuwa wameelezwa kuwa mtoto kalipiwa kila kitu hivyo ni wajibu wa shule kulipia hiyo medical checkup.
Kuna shule moja nilifika na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanataaluma wa pale alinivuta pembeni mwalimu mmoja, akanieleza "..ndugu kwa kuwa wewe umekuja kutaka kujua mazingira halisi ya elimu huku chini, ni jambo jema kufahamu hili..... WAALIMU WAPO KIMYA KANA KWAMBA KILA KITU KIPO SAWA LAKINI MATOKEO YA KIMYA HIKO NI ANGUKO KUBWA LA ELIMU KUFIKIA MWISHO WA MWAKA HUU....
Hili suala la HAZINA na TAMISEMI kutuma fedha mashuleni kwa masharti waliyoyapanga wakiwa ofisini kwao ni zito na linapaswa kurekebishwa. Ingelikuwa vyema kungefanyika yafuatayo
Kinachofanyika sasa ni kwamba Rais amezungukwa na washauri wasiomtakia mema ambao wapo tayari kumshauri kitaalamu aporomoke kiutendaji ili kusaidia mwendelezo wa madudu na utendaji usiozingatia tija nchini. Kuna changamoto nyingi sana ambazo tasnia ya elimu nchini inakumbana nazo lakini hakuna ufumbuzi wa maana unaopatikana. CWT imebakia kutetea maslahi ya waalimu huku ikikwepa kushauri mazingira ya utoaji elimu kutimiza vigezo
Ndugu Rais. Waalimu wapo kimya, usidhani kimya chao ni ujumbe wa kuridhika na yanayoendelea na usidhani kuwa ni maslahi yao pekee yatakayo waridhisha... angalia mazingira ya kazi waliyonayo. Tuwasaidie waweze kuzalisha wasomi watakaoisaidia nchi tusiwapeleke kwenye kona ambayo majuto yake ni zaidi ya mjukuu......
Ni watendaji walewale waliofisadi nchi hii ndiyo ambao bado wapo ofisini wakipiga miluzi ya HAPA KAZI TU huku wakichekelea kila doa linaloichafua nia njema ya serikali kwa watu wake.
Nimetimiza wajibu.

- Walinzi. Hawa wameondolewa katika malipo hivyo maana yake ni kwamba shule zitisitishe mara moja mikataba ya walinzi wa shule. Hapo Maabara zilizojengwa kwa gharama kubwa zimewekwa rehani na shule ambazo zina samani za TEHAMA zimekuwa hatarini zaidi kwani hakuna walinzi tena mashuleni na hakuna maelekezo wala ufafanuzi wowote kutoka ngazi ya Manispaa, mkoa na Taifa katika kupata ufumbuzi
- WAALIMU WA MUDA (Part-Time Teachers) hawa waalimu walikuwa wanaziba pengo la upungufu wa waalimu wanaokosekana hasa wa masomo ya sayansi ambapo utakuta kata nzima yenye shule tano za sekondari ina waalimu wawili wa Kemia, mmoja Physics, Biology na kadhalika.
- WAKUTUBI (Librarians) hawa ni waalimu ama wadau muhimu sana kwenye shule zote. Utakuta kuna shule ambazo wamepata marafiki wa elimu wakawajengea maktaba na kuwapatia vitabu, hivyo ni jukumu la shule kuwa na wakutubi ambao watasimamia maktaba hizo. Mkutubi husomea kuanzia ngazi ya cheti hadi Uzamifu. Hakuna fedha iliyolenga kulipa mishahara ya wakutubi. Maktaba zitafungwa na tutarudi gizani tena
Hayo ni machache ambayo niliyaokota katika kikao kile. Niliamua kufanya utafiti mdogo katika kata na wilaya zingine kuona kama tatizo ni lile lile. Hivyo nikagundua kuwa utaratibu huu unakanganya mno. Kuna mwalimu mmoja wa taaluma alinieleza kuwa baadhi ya wazazi waliopeleka vijana wao kwenye usaili wa kidato cha kwanza walitaka shule iwapatie fedha za kulipia "medical examination" za watoto wao. tena wengine walisisitiza kuwa wameelezwa kuwa mtoto kalipiwa kila kitu hivyo ni wajibu wa shule kulipia hiyo medical checkup.
Kuna shule moja nilifika na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanataaluma wa pale alinivuta pembeni mwalimu mmoja, akanieleza "..ndugu kwa kuwa wewe umekuja kutaka kujua mazingira halisi ya elimu huku chini, ni jambo jema kufahamu hili..... WAALIMU WAPO KIMYA KANA KWAMBA KILA KITU KIPO SAWA LAKINI MATOKEO YA KIMYA HIKO NI ANGUKO KUBWA LA ELIMU KUFIKIA MWISHO WA MWAKA HUU....
Hili suala la HAZINA na TAMISEMI kutuma fedha mashuleni kwa masharti waliyoyapanga wakiwa ofisini kwao ni zito na linapaswa kurekebishwa. Ingelikuwa vyema kungefanyika yafuatayo
- Wizara ingeitisha mapendekezo kutoka manispaa na Halmashauri zote nchini kuhusiana na mgawo kwa maeneo ambayo fedha za kuendeshea shule.
- Manispaa na Halmashauri zingetoa maagizo hayo Kata
- Maagizo kutoka Kata zifikie Bodi na Kamati za shule kuandaa na kutuma mapendekezo yao.
Kinachofanyika sasa ni kwamba Rais amezungukwa na washauri wasiomtakia mema ambao wapo tayari kumshauri kitaalamu aporomoke kiutendaji ili kusaidia mwendelezo wa madudu na utendaji usiozingatia tija nchini. Kuna changamoto nyingi sana ambazo tasnia ya elimu nchini inakumbana nazo lakini hakuna ufumbuzi wa maana unaopatikana. CWT imebakia kutetea maslahi ya waalimu huku ikikwepa kushauri mazingira ya utoaji elimu kutimiza vigezo
Ndugu Rais. Waalimu wapo kimya, usidhani kimya chao ni ujumbe wa kuridhika na yanayoendelea na usidhani kuwa ni maslahi yao pekee yatakayo waridhisha... angalia mazingira ya kazi waliyonayo. Tuwasaidie waweze kuzalisha wasomi watakaoisaidia nchi tusiwapeleke kwenye kona ambayo majuto yake ni zaidi ya mjukuu......
Ni watendaji walewale waliofisadi nchi hii ndiyo ambao bado wapo ofisini wakipiga miluzi ya HAPA KAZI TU huku wakichekelea kila doa linaloichafua nia njema ya serikali kwa watu wake.
Nimetimiza wajibu.
Ni kweli waalimu wapo kimya kimya kabisa:
1. Ndani ya siku 100 Wahandisi wamelipwa bilioni 400, waalimu wanadai takribani bilioni 50. Hakuna hata anayetukumbuka.
2. Wanafunzi walikuwa walichangia hela kidogo kwa ajili ya mitihani kila J'mosi, kwa sasa hakuna hata hela ya kununulia ream. Vifungu husika vimepelekwa ukaguzi kanda na bodi.
3. Wanafunzi walikuwa wakichangia 10,000/- kwa mwaka kwa masomo ya ziada kwa wengi wao hawaelewi ndani ya muda uluioainishwa kwenye ratiba.
4. Wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wanakaa chini (sakafuni), pamoja na robo ya visato vya juu. Siku za nyuma kidato cha kwanza na waliokuwa wanahamia walikuwa wakija na viti na meza.
5. Fomu ya kujiunga na kidato cha kwanza ni moja nchi nzima, kama kwamba mahitaji ya mwanafunzi ni sawia nchi nzima.
6. Takribani kila wiki Mkurugenzi anaongeza masharti na kanuni. Majuzi ametoa barua ikiwataka waalimu shule zote za halmashauri kuomba ruhusa siku ya Ijumaa tu (isipokuwa kwa vifo na ugonjwa), hata kama mshahara umetoka Jumatatu, kama kwamba ili hali shule zipo zaidi ya 80 km toka halmashauri.
7. Wakuu wengi wa shule, kupitia TAHOSSA wanaisaidia serikali kuwakandaniza waalimu. Kwa mfano kuwatisha.
8. Maafisa Elimu wanapokuja kwenye vikao vya bodi , na mambo mengine ya kiofisi hawawasikilizi waalimu ili hata kujadiliana changamoto, kwa kuwa huwa wamepoozwa kwa bahasha za kaki. Kwa mfano, haiwezekani mdani ya miaka 10 hakuna bajeti ya shule iliyowahi kukataliwa au kufanyiwa maboresho na badi.
9. Wakaguzi, hasa toka halmashauri wanakuja kukagua huku wakiwa hawana sifa (wengine huwa ni wakaguzi wa shule za Msingi, wanakagua na kutoa makaripio hata kwa masomo waliyajua, kwa mfano aliyekuwa mwalimu wa shule ya Msingi anakuja kukagua hesabu, Kifaransa, ...shule ya Sekondari ili hali hajui kabisa).
10. Ukosefu mkubwa wa vitabu na vifaa vinginevyo vya kufundishia na kujifunzia.
11. Mwanafunzi 'kutukuzwa' kuliko mwalimu. Maafisa Elimu wapo mstari wa mbele kuwaonya vikali waalimu, ili hali makosa kama utoro sugu, mimba, utovu mkubwa wa nidhamu (kama ulevi, ...) kutoshughulikiwa kabisa.
Kimya kina mshindo. Natamani Prof. Ndalichako akaze kamba ili black & white ijulikane kupitia matokeo ya NECTA.
Mungu ibariki Tanzania.