NYONGEZA: Pentium zilikuwa ni Processor 1 inafanya kazi kwenye Computer kama CPU. Baadaye wakaja na CoreDUAL ambazo ndani zilikuwa ni Processor Pacha. Baadaye wakaja na Core2Dual ambazo zinakuwa ni Processor pacha mbili. Ila hizi zote zinakuwa zinafanya kazi pamoja kila kukitokea kazi ya kufanya. Sasa hivi wamekuja na hizo mkuu kaandika hapo zenye Alama ya i3, i5 au i7. Hizi nazo zina procssor nyingi ndani ila zinafanya kazi kidogo tofauti na hizo Core Dual. Maelezo yake ndiyo haya hapa chini:>>>>
Hizi Processor zinafanya kazi kwa maelezo mazuri ni kama yale maroli yenye matairi mengi na kama halina mzigo mkubwa au halina kabisa, linanyenyua baadhi ya matairi juu na yanakuwa hayakanyagi chini/kutumika. Mzigo ukiwa mkubwa basi yanashushwa ili kusaidia yale mengine na wakati huohuo kuugawanya mzigo kwenye matairi mengi ili gari lisiharibu barabara kwa uzito.
Hizo processor nazo huwa ndani ziko nyingi na kama kuna kazi kidogo, bazi zinafanya kazi chache tu au moja na nyingine zinapumzika na hivyo ku-Save energy. Kama kazi zikiongezeka, basi inaongeza na processor zaidi kufanya kazi. Ila zote zimefungiwa ndani ya CPU moja na zinafanya kazi moja, mbili.... zote.