Instagram kuficha 'likes' ni sahihi?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1573479290648.png


Habari zenu wadau, bila shaka Jumatatu inaenda vyema.

Kumekuwa na taarifa kuwa mtandao maarufu wa Instagram unatarajia kuanza mchakato wa majaribio ya kuficha 'likes' kwenye post.

CEO wa Instagram, Adam Mosseri, amesema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuondoa ushindani na kuweka mkazo zaidi kwa watumiaji kufahamiana na watu wengine, badala ya kuweka umakini mkubwa kwenye idadi ya likes wanazozipata kwenye kurasa zao. Japokuwa watumiaji bado watakuwa na uwezo wa kuona likes zao, kitendo cha kutozionyesha kwa umma bado hakijapokelewa vizuri na watu wengi.

Mtandao huu umefanya mabadiliko mengi miaka ya hivi karibuni na kiukweli mimi naona kama vile wanajaribu kuondoa originality ya platform yenyewe. Sababu yao haina mashiko ukizingatia kwamba watu wamekuwa wakiconnect vziuri tu hata sasa ambapo likes zinaonekana.

Anyways, majaribio ya hili yanatarajia kuanza hivi karibuni na tusbiri tuone matokeo yatakavyokuwa, Mimi binafsi naona waache mambo kama yalivyo.

Nakaribisha maoni.
 
Back
Top Bottom