Instagram inavyoweza kubadilisha kipato cha mtu

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Habari, Kwa jina najulikana kama Secretary Pompeo, Leo nataka nikuandikie ukweli unaohusu mtandao wa Instagram jinsi unavyoweza kubadilisha maisha ya mtu katika suala zima la kipato.

Kwanza kabisa, nakumbuka kipindi Cha miaka miwili nyuma, nilikua nikiingia Instagram naona post za mtu anajiita carrymastory, nilimdharau sana, nikawa najisemea "hivi huyu dada kakosa kazi hadi aje mitandaoni huku kuleta Mambo ya udaku!", Sikujua, Ila Sasa nimejua.

Jinsi followers wanavyozidi kuongezeka katika account yako ndio jinsi unavyozidi kuukimbia umasikini, Leo mtu Kama carrymastory, mwenye Followers 1.8M akikuambia anaingiza sio Chini ya Million 3 kwa mwezi kwa ajili ya matangazo usishangae, najifikiriaga, Kama Mimi mwenye page yenye followers laki na nusu naingiza sio Chini ya 60,000/= kwa siku, je huyu mwenye followers 1.8M atakua anaingiza kiasi gani???

Sometimes nawaza Sana, kwasasa pesa zipo mtandaoni, maana page zangu za Instagram mbili kwa siku zinaniingizia faida kubwa ambayo siwezi kuipata hata kwa siku 3 kwenye biashara ninayofanya.

Usione mtu anapage ya udaku ukamdharau, au ukaona anapost matangazo ya waganga, Nguvu za kiume au mengineyo ukamdharau, unaweza kuta huyo mwenye hiyo page kwa mwezi anamuacha mbali Sana Mwalimu mwenye Degree anaefundisha Shule ya Secondary, Tena anamzid hata karibia mara3 ya mshahara wake.

Nilikua nadharau Sana page za matangazo/habari au Udaku za Instagram, lakini baada ya kumiliki Page mbili kubwa, aisee nimeamini, pesa zipo mtandaoni, hasa hasa instagram.

Na asikudanganye mtu, wale wanaocomment kua wanauza account, ni waongo, kuuza account Instagram yenye followers wengi ni sawa na kuuza fremu ilioko maeneo ya kariakoo, Hufikirii tuu page unayoweza kumuingizia mtu 40,000 kwasiku anawezaje kuiuza kwa 100,000?? Inakua ni utapeli, na hata Kama akikuuzia itakua ni ya kuboost, followers wake wanakua sio wa Tanzania, wanakua ni wa nchi za nnje ambapo hiyo haisaidiii, Bora uwe na page yenye 10k lakini wa Tanzania tupu kuliko kua na Page yenye followers 50k halafu karibia wote ni wazungu, waarabu na nchi za mbali huko, haifai hiyo na haitakulipa.

Wakati naanza kutumia page zangu hizi mbili za Instagram kibiashara kwakua Zina followers wengi nikawa na kua busy sana na simu, ikapelekea nikawa hata sihudumii wateja wa dukani kwangu ipasavyo maana mda mwingi nipo busy na simu, hiyo ikapelekea niajiri mtu, awe Kama Admin anaendesha page zangu zote mbili, jioni nakua naangalia tuu maendeleo yake kwa kukagua post anazopost, kwa siku namlipa 15,000 inamaana kwa mwezi ninamlipa jumla ya shilingi za kitanzania 450,000.

Vijana tuweni wajanja pesa zipo mtandaoni, tusilalamike hamna ajira.
 
Kupiga hela inakuhusu wewe sasa makelele ya nini?

Endelea kupiga ela tuache tulime matikiti shungubweni.
 
akikujibu uni-tag tafadhali

Hawezi kujibu hizo account kwasababu uzi wake umebase kwenye idea....yani hana hizo account kama anavyodai (labda kama anafikiria/ndio amefungua hizo pages za udaku)
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Hawezi kujibu hizo account kwasababu uzi wake umebase kwenye idea....yani hana hizo account kama anavyodai(labda kama anafikiria/ndio amefungua hizo pages za udaku)
Ngoja nikuorodheshee, kumbe nawew una wivu sikujuaga
 
Hawezi kujibu hizo account kwasababu uzi wake umebase kwenye idea....yani hana hizo account kama anavyodai(labda kama anafikiria/ndio amefungua hizo pages za udaku)
Haya waambie na wenzako wakafollow page zangu
Bongetrending_habari
Udaku_mastory

MTU akiweka suala la serious nyie mnatafuta namna ya kumkosoa, Yani wabongo sijui tunakwama wapi ndio maana hatuendelei
 
Kumbe ndio maana naonaga hao hao wenye acount zao wakasema (kwa matangazo njoo in box tuongee)kumbe ndio biashara yenyewe wanaenda kuzungumza huko
 
Ndio hivyo mkuu, Mimi mwenyewe mwanzo nilikua sielewi
Aisee kama ni hivyo waaingiza hela sana kuna jamaa (ni mtangazaji)kwenye page yake ni matangazo tuu mtaalamu wa nguvu za kiume na dawa. Basi nikashangaa hai yeye anasapoti hayo mambo kumbe anaingiza hela asee
 
Haya waambie na wenzako wakafollow page zangu
Bongetrending_habari
Udaku_mastory

MTU akiweka suala la serious nyie mnatafuta namna ya kumkosoa, Yani wabongo sijui tunakwama wapi ndio maana hatuendelei

We nae,sasa wivu wa nini hapo?
Nimekwambia utaje hizo pages tukakuongezee followers

Ngoja nikuorodheshee, kumbe nawew una wivu sikujuaga
 
Aisee kama ni hivyo waaingiza hela sana kuna jamaa (ni mtangazaji)kwenye page yake ni matangazo tuu mtaalamu wa nguvu za kiume na dawa. Basi nikashangaa hai yeye anasapoti hayo mambo kumbe anaingiza hela asee
Yani usipime, Mimi Kuna jamaa aliniambia kipindi hicho kua kwa siku wanaingiza hela nying Sana nikawa nabisha, haya maisha hayana formula
 
Tuambie na njia unayotumia kupata followers, kwani hapo ndio kuna changamoto sana na ndio watu wengi wanaposalenda

Binafsi na kubaliana na wewe kabisa kwani nimeona katika digital platform kuna fursa nyingi sana za kupiga ela.
 
Tuambie na njia unayotumia kupata followers, kwani hapo ndio kuna changamoto sana na ndio watu wengi wanaposalenda

Binafsi na kubaliana na wewe kabisa kwani nimeona katika digital platform kuna fursa nyingi sana za kupiga ela.
Akikujibu niite nije
 
Instagram naipongeza kwa kuwasaidia wasanii wengi wa hapa Tz. Wangekufaa njaa wengi wao maana ndyo source ya kipato wqlichobakiza tofaut na kudanga
 
Back
Top Bottom