Insp MJ Eliasi na WP 6052 jirekebisheni

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Wanajamvi,

Leo muda huu kwenye bus la ruti ya Kitunda- Kivukoni kumetokea na tukio ambalo ni la kawaida ila kwa namna ya lilivyokua handled ni very un professional.

Ni kweli dereva ana makosa kwa kushusha abiria sehemu ambayo sio ya kituo hapa kwenye ujenzi wa flyover VETA.

Na baadae Insp wa polisi wa hapa aliyekua inchaji leo MJ ELIAS kumwambia aweke gari pembeni kwa ajili ya kuandikiwa.

Dereva alitii amri na kuweka bus pembeni likiwa na raia wengi.

Dereva aliombwa leseni na akajibu leseni Ameisahau.

Tukio lisilokuwa la kawaida na kinyume cha matarajio ya wengi na kinyume haki za binadamu inspector huyu wa polisi alianza kumpiga makofi usoni dereva na kumfosi dereva kukaa chini.

Kama hiyo haitoshi,WP 6052 aliyekuwepo hapo karibu nae alianza kujibu kwa dharau na kebehi kwa raia waliokua wameshuka kwenye bus ili kuomba warudishiwe nauli wamalize safari kutoka hapo VETA kwenda kivukoni au dereva ataje namba za leseni ili polisi waweze kuingiza kwenye mashine zao ili waandike faini.

WP 6052 alijibu umati kwa kebehi akisema " ole wenu mtu apogee hapa nilipo"

Pasi kuangalia ni umri gani anaowajibu .

Raia walipotaka kujua kwa nini wasisikilzwe WP huyu aliwajibu kwa kufoka "Acheni kelele"

Ni wito wangu kwa Askari kuwa wasikivu na kusaidia kutatua tatizo na si kukomoa makumi ya watu wanaoenda kujenga taifa asubuhi hii.

Hata kama dereva ana makosa,dereva hana leseni ,dereva kafanya kosa hayo yote sio makosa ya abiria na ilipaswa Askari wa hapo veta muwe nambari moja kutafuta solution ya abiria kuwahi kwanza na nyie kubaki na wahusika wenu.

Msivunje sheria kwa kumpiga dereva mbele ya abiria hata kama amekosa. (PRESUMPTION OF INNOCENCE).

Insp MJ ELIAS na WP 6052 jirekebisheni.

Ova.​


20210806_102251.jpg
 
Wanajamvi,
Leo muda huu kwenye bus la ruti ya kitunda- kivukoni kumetokea na tukio ambalo ni la kawaida ila kwa namna ya lilivyokua handled ni very un professional.
Ni kweli dereva ana makosa kwa kushusha abiria sehemu ambayo sio ya kituo hapa kwenye ujenzi wa flyover VETA
madereva wa daladala wanasumbua sana safi sana askari saizi ni makofi tu watafuata sheria wenyewe na nyie abiria mmejitakia kwanini mmeruhusu ashushie abiria hapo na pamekaa vibaya lazima a create foleni
 
Hapo mkuu huu uzi lazima wauone hata Kama siyo member wataambiwa tu, Kwa Askari kutaja Coy number yake ni zaidi ya Jina lake yaani umewachoresha kishenzi, maana mabosi zao wanapita humu.

Askari kuweni na weledi msidharau raia Kuna ambao walishafanya hizo kazi zenu wakaacha,kuachishwa au kustafu. Kuweni professional hampo juu ya Sheria na mbona mnadharau wapanda daladala ikiwa humo Kuna watu ambao Wana vipato sawa na Ndugu zenu..na wengi wenu mnapanda lift kutokana na uniform zenu, anayekupa lift leo kesho anapanda daladala utu wenu upo wapi???
Kuweni wastarabu kazi ukiipenda haikutupi, Tatizo shule ndogo.

Kazi mnayoifanya haisomewi unaajiriwa baada ya kusota CCP Moshi Kifupi ni kazi ya uzoefu siyo taaluma Wala ujuzi kwa maana hiyo na nyinyi bado ni wananchi wa kipato Cha chini nyumba za kota ndiyo zinawapunguzia ukali wa maisha badilikeni uaskari wa kibabe umepitwa na wakati.
 
Polisi muda wengine tunawaonea.. hakuna mtu asiyejua upumbavu wa madereva dala dala.

Anasimama popote ili apakie ama ashushe bila kujali usalama wa watumia barabara wengine.

Kama unaendesha gari huwezi watetea dala dala hata siku 1
 
Aiseeee me nasemaga Askari ajaribu kunipiga kofi tu kwa kosa Kama Hilo ndo atajua kua kupigana sio mpaka ufundishwe.
Ma"fala kama nyie ndo mnakuwaga chambo wa kupigwa makofi na teke!!!!

Uje ujichanganye afu uone:
 
Huyo dereva naye angemoiga ngumi moja tu ya ukweli hadi jino litoke.
Hii nchi sio ya mama zao ni yetu sote.
 
Back
Top Bottom