Insha Maridadi 1: Farasi wa Magufuli Wamegoma Kunywa Maji...

Mdogo wangu Chahali acha jazba kabla ya kujenga hoja.Hata wewe ukiwa Rais hakuna jinsi ndugu zako na rafiki zako wakatosheleza kuwa wasaidizi wako.Hakuna mapambano bila changamoto,ukisoma hoja ya Ndugu Mwanakijiji kwa makini utaelewa,rudia kusoma.Hivi Ile hela uliyoahidiwa na Kinana ulishalipwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee chalii sasa umeandika nini? Ndio kashalipwa. Haya faster Nenda na wewe ulipwe B7
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
Umezunguuuuka Hadi unatia huruma

Muda WA maneno murefu kama kamba umekwisha.... Go straight to the point

Unfortunately huna point kwenye hili, ungetoa suggestions

Kaput
 
Mkuu watanzania ni desturi yetu,Nyerere na ualimu wake hawakumelewa licha ya kutawala nchi miaka 27.Katunga vitabu wee vya ujamaa na kujitegemea ,Mwongozo,tujisahihishe,It can be done play your part lakini hatukujitambua,
Labda nikupe wazo tu,Tanganyika ilipata uhuru kabla ya kujitambua,na hadi leo hatujajitambua.
Ndio maanake Mwingereza alitaka atutawale miaka mingine isiopungua 70.Tatizo si Magufuli tatizo lipo nje ya box.
 
Ukweli ni kwamba, watu wengi walio serikalini ambao mzee anawateua based on their qualifications (vyeti vya darasani) ni wezi na wachora michongo ya kupiga hela. Ukiona watu wanapanga safari kupeleka ndege ulaya ili ikapakwe rangi na kuna bajeti washaweka wazi, ujue walafi ni wengi.

Sio vibaya, baba mwenye nyumba akaja na formula yake ya kuajiri watu ambao wanaweza kumsaidia ku-deliver anachotaka.

Kuna taasisi moja duniani wao katika mfumo wa kuajiri wanafuangalia Character, then Competence na mwisho Chemistry ili kupata working culture.
Tukiwa wakweli, uwezo wa mavyeti kwa wasaidizi wa JPM uko vizuri sana, hakuna anaebisha. Ila wengi wana bad character. Wengi ni wezi, wanatamani fursa ilikiwa wazi wapige hela (suala la kupaka ndege rangi ni moja ya nini baba mwenye nyumba anatuambia).
Competence ni outcome ya mtu kuwa kwenye field baada ya kupewa nafasi. JPM mwenyewe hakuwa anajulikana kabla ya Rais Mkapa kumpa nafasi 1995 ya inaibu waziri. Tokea hapo akapata fursa ya kupanda juu. Paulo Makonda mpaka sasa kuna mjadala mkubwa wa vyeti vyake, na mpaka sasa delivarables zake zina wanawafunika watu kibao wenye ma-vyeti yao.
Katika Watanzania mil 55, sio vibaya akahukua vijana mtaani maana nao ni Watanzania na wana njaa ya kuonyesha uwezo wao.'
Creativity na spirit ya kuwa industrious nayo iko chini sana kwa watu wanajivunia kuwa watumishi wa umma.
Mzee, usione vibaya kutafuta vijana wenye vision on how solve problems which are facing Tanzanians.
Kama kwenye korosho, mpaka sasa nashindwa kuelewa kwanini wizara ya fedha, viwanda na biashara wameshindwa kumfanya mzee atabasamu kwa kuona tunauza katika Global standard.
Hao wenye simu ya mzee mbona hawampi hizi ndogondogo. Kwa wale wenye simu nami mnigee, mimmegee mzee on how he should go about to maximize value ya korosho
 
Mwanakjiji anataka kutwambia kuwa mwenye farasi ni mzuri ni mwema lakini Farasi ndo wabaya!, Ila hajaeleza ubaya wa Farasi ni upi maana amekiri kuwa kazi nzuri wanafanya!

The fact is Mwenye Farasi hajui what exactly nini kazi yake!!

Mpaka sasa hivi Ben Saanane kapotea
Kanguye Kapotea
Lissu kapigwa vyuma waziwazi
Watu wamepotea MKIRU

Mambo ya msingi kabisa lakini serikali yake imemute!

Tatizo unafikiri haya ni mambo yote ya Rais; ni vizuri watu walalamikie watu wahusika. Mkimlalamikia Rais kwa kila jambo ndio mnaona kwamba Rais anatakiwa kufanya kila kitu. Suala la MO kwa mfano; ni suala la polisi siyo la Magufuli. La Saa Nane ni suala la polisi...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
Honestly kuna Watanzania wengi sana ni wavivu wa kufikiri, kumbukeni alichosema Rais Mkapa.
Prezaa anatakiwa apate thinkers na kuwa entrust wapige kazi.

Sio kanisani tulifundishwa Yesu alikuja kwa Wayahudi, wakampotezea, ikabidi wokuvu uende kwa watu wa nje ambao waliitwa mataifa.
Kama farasi hakubali kunywa maji ili mzigo uende, huku mtaani kuna farasi wengi sana ambao wanaweza kutoa matokeo tarajali
 
Unataka kumdanganya nani kuwa John ahusiki na hayo unayoyasema Rais anayezuia uhuruwa habari,bunge live na vyama vya upinzani kuongea ni mwizi na ana makandokando kuliko kawaida.Usitake mimi nionekane mjinga eti niamini John ahusiki na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya upinzani,kama unadhani hivyo basi wewe ndiyo mjinga.
John atavunja rekodi ya ufisadi ya miaka 50 toka nchi ipate uhuru.
Nakuonea huruma kwa kudhani watanzania ni wajinga,farasi wanafanya anachofanya mfugaji....wamemgomea kula peke yake wao wanywe maji.
Una akili kupindukia ndugu,umemjibu mtu mwingine lakini nimeelewa mimi ,nimefarijika mimi.
 
Tatizo unafikiri haya ni mambo yote ya Rais; ni vizuri watu walalamikie watu wahusika. Mkimlalamikia Rais kwa kila jambo ndio mnaona kwamba Rais anatakiwa kufanya kila kitu. Suala la MO kwa mfano; ni suala la polisi siyo la Magufuli. La Saa Nane ni suala la polisi...
Watu wanamsukumia lawama Rais sababu kila kukicha utasikia 'tumefanya hili kwa amri ya mamlaka kutoka juu'

Basi na sisi tunapeleka lawama kwa mamlaka iliyoko juu.
Jeshi la Polisi lisingekuwa POLICCM hakika wananchi tungeliamini utendaji wake.

Hebu rudi kidogo kwenye sakata la kupigwa risasi lisu. Polisi washatuambia uchunguzi umeshindwa kuendelea sababu mashuhuda wako nje.
Lakin hapo hapo wameshindwa kutuambia hata aina ya silaha iliyotumika kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa kwenye eneo la tukio.

Ukirudi dakika chache kabla ya tukio lenyewe haswa mkuu wa nchi anatamka hadharani kabisa 'malipo ya msaliti yanajulikana'
Na hapo kashatoka kutuelezea namna Lisu alivyokuwa anaomba taarifa za Accacia kutoka kwa Mwanyika.
 
Bwawa ruba ameingia ndio maana farasi hawataki kunywa maji kwani kuingiza midomo yao bwawani ni kuhatarisha uhai wao mimi yangu macho tu
Tutaelewana tu
Nb Magufuli si bingwa wa kupiga push ups ?
Kwanini asiwatie mateke Farasi ? Thubutuuu !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How do you fight corruption without:
Free press, Free opposition, Free Civil Society, Free Parliament, Free Judiciary, Free Anti-Corruption Organ, Free Speech, Academic Freedom to Research and Publish statistics, Free social Media, ...?

A lone soldier cannot fight corruption unless that solder is corrupt too.
Good point.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
Moja ya sababu kubwa inayomfanya Rais aendelee kufeli ni kuzungukwa na watu wanafiki ambao kazi yao kubwa ni kumsifia hata kama anaelekea shimoni,huu ni udhaifu mkubwa alioutengeneza mwenyew kwa kupenda sifa asizostahili.Ukiondoa neno Rais,John ni mtu wa kawaida na mwenye fikra za kawaida sana.Kutokana na mifumo yetu mibovu iliyoasisiwa na katiba neno Rais linamfanya aonekana exceptional yaani ana akili kuliko wote jambo ambalo halina ukweli wowote kwa sababu hakuna mahala imeandikwa kuwa Rais lazima awe na akili kuliko wote.Kutokana na sababu hizi zilizompa rais mamlaka makubwa ya kufanya lolote analotaka ndizo zinazosababisha watu wanaomzunguka wakose nguvu na hivyo kuwa opportunist kwa either kupiga vigeregere au kukaa kimya kimya mwenye nguvu afanye.
Kwa maoni yangu mleta maada ni miongoni mwa watu wanafiki either kwa kulinda maslahi binafs au uelewa mdogo katika kutambua mfumo/style za uongoz wa John.Acha kuzungukazunguka chanzo cha matatizo ni yey mwenyew kwa kuwa yupo self centred,tumeshuhudia wasaidiz wake wenye maono tofauti akiwatumbua hvyo wengine wameona bora taifa lipate hasara kuliko kupoteza nafas zao
 
Yani ktk watu ambao nimeshawatoa kwenye kundi la JF GT basi ni huyu Mwanakijiji.
Maandiko yake amekua akiandika kama vile mtu ambaye hajafikiria.
Kweli wewe unakuwaje mpuuzi kumsafisha magufuli kwa uozo huu alioleta kwenye nchi hii.
Hakuna mtu mbaya na muovu km magufuli,yeye kama ni mwema na akemee uovu uliopo nchini kwa sasa.
Hatupendi kuhukumu kwa sababu sio kazi yetu llkn magufuli ni mbaya mno.
Anajua muda wa kujifanya mwema ili kuwapoteza wajinga wa kitanzania,muogope sana MUNGU wewe mwanakijiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Mzee Mwanakijiji mimi hua sisomi hekaya zake,kwa sababu anakera sana,nyeusi yeye husema nyeupe,hajui hata kusoma body language za watu,hawezi kutofautisha propaganda na hali halisi.Ana macho lakini haoni,ana masikio lakini hasikii.
 
Kwamba magufuli hana Siasa za chuki?
Mdogo wangu Chahali acha jazba kabla ya kujenga hoja.Hata wewe ukiwa Rais hakuna jinsi ndugu zako na rafiki zako wakatosheleza kuwa wasaidizi wako.Hakuna mapambano bila changamoto,ukisoma hoja ya Ndugu Mwanakijiji kwa makini utaelewa,rudia kusoma.Hivi Ile hela uliyoahidiwa na Kinana ulishalipwa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda na hao wanaolipa milioni 5 kupaka gari rangi linalogharimu milioni 7 nao wanalizwa wanahitaji kufanya ukaguzi wa ghafla!
May be, lakini hata kwa kulinganisha na bei ya kpaka rangi nyumba, hiyo 5 million inaonekana ni ndogo. Anyway., siko familiar sana na bei za Bongo.

Lakini Kitendo cha Rais kuacha kazi na kwenda kukagua maendeleo ya project/kazi ya million 5 inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tatu.
 
Wataalamu wa ndege hebu watuambie kuhusu suala la Rangi, hivi zile rangi za ndege huwa ni rangi tu au kuna engineering aspect nyingi zinazingatiwa maana ninavyofahamu kule angani kuna hali tofauti sana na huku hivyo kila kiendacho kule lazima kuwe na calculations za kitaalamu ili mambo yaende sawa. TUJITAHIDI KUFIKIRI JAMANI.
 
Back
Top Bottom