Insha Maridadi 1: Farasi wa Magufuli Wamegoma Kunywa Maji...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1553794907026.png
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
 
Umezunguka Sana Mkuu
Katiba ipi unayoizungumzia watendaji wa chini watekeleze?

Kuna kitu kinaitwa "Tone at the top "Katika sayansi ya vihatarishi yaani "Risk management "wapanga mipango au mikakati ni watu wa juu hapa hujumuisha watawala na bodi husika, Ubovu utakaonyeshwa na Tone at the top kwa kujua au kutokujua huacha madhara makubwa kwa watu wa chini

Hakuna kitu muhimu Kama mawasiliano yaani Communication Kati ya mkuu juu na taasisi za chini, kuna muda yapasa maoni yachukuliwe chini na kupelekwa juu

Huu mfumo wa kutegemea watu baadhi juu kuweka malengo kwa taifa zima ni kazi kubwa

"It is easy to manage Risk than Crisis "ni rahisi kupunguza au kuweka sawa vihatarishi kuliko kusubiri Janga, Janga likitokea Lina gharama kubwa sana

Nini kifanyike :

Mamlaka kuanza kusikiliza maoni na mahitaji ya wadau au wananchi wanataka nchi ya namna gani?

Mamlaka iangalie nini imepelekea punda kugoma kunywa maji yaani hawa watekeleza sera, Je walishiriki kutengeneza sera na mikakati au wanalazimishwa tu kutekeleza bila maoni yao kusikilizwa

Muda hautoshi lakini naunga Juhudi zako mwana kijiji kama wengine
 
Unataka kumdanganya nani kuwa John ahusiki na hayo unayoyasema Rais anayezuia uhuruwa habari,bunge live na vyama vya upinzani kuongea ni mwizi na ana makandokando kuliko kawaida.Usitake mimi nionekane mjinga eti niamini John ahusiki na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya upinzani,kama unadhani hivyo basi wewe ndiyo mjinga.
John atavunja rekodi ya ufisadi ya miaka 50 toka nchi ipate uhuru.
Nakuonea huruma kwa kudhani watanzania ni wajinga,farasi wanafanya anachofanya mfugaji....wamemgomea kula peke yake wao wanywe maji.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.

Watendaji wengi wa serikali sio wabaya kielimu. Wana shida ya ethics....wana shida ya working culture. Wengi wako kimaslahi kuliko kikazi. Hawana wanachojua zaidi ya kuhakikisha wanapata hela nyingi pale fursa inapotokea.
Rais wetu anapambana. Ukisikiliza anachosema kuhusu rushwa, unaona kabisa ana maanisha. Lakini rushwa bado ipo ndani ya serikali na kandarasi zake.
Watumishi wengi ni wala rushwa wakubwa. Kupambana na rushwa ni kazi ya aina yake.
JPM asikate tamaa...hayuko mbali sana na kutoboa kutoka kwenye lindi la haya matatizo

Wengi wameshaanza kuchoka. Wengi wanajua anamaanisha. Aendelee mbele. Atapata askari waaminifu watakaomuunga mkono.
 
Ukitaka kumaliza mzizi wa fitna kuhusu rushwa nchi ipitishwe sheria ya mtu akitoa rushwa na kupokea rushwa wanyongwe!
Hata wahujumu uchumi na mafisadi wanyongwe hapo kidogo tutaenda Sawa!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana hela ya rushwa ndio inanunua mavogue...inajenga maghorofa....inaunua ticket za watu wanaoenda Dubai kufanyana.

Yaani shida tupu
 
Mwana Kijiji, It does not make sense to hire smart people and tell them what to do. We hire them so they can tell us what to do. Hii ya kushangilia kupaka rangi ya ndege kwa shillingi milioni saba inaweza kututokea puani. Ndege yaweza kuruka mara moja kwenda Mwaanza na kurudi na rangi imeisha!
 
How do you fight corruption without:
Free press, Free opposition, Free Civil Society, Free Parliament, Free Judiciary, Free Anti-Corruption Organ, Free Speech, Academic Freedom to Research and Publish statistics, Free social Media, ...?

A lone soldier cannot fight corruption unless that solder is corrupt too.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea hao "farasi" kugoma kulazimishwa kunywa maji. Nitaorodhesha baadhi.

1. Wengi wa wateuliwa wa Magufuli ni marafiki zake kama sio ndugu zake. Wakati urafiki unaweza kuwa asset kwa maana ya "rafiki yangu ameniamini na kunipa jukumu hili, na kufanikiwa kwa jukumu hili ni kufanikiwa kwake, na kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwetu sote" urafiki pia unaweza kuwa liability kwa maana ya "hata nikiharibu hawezi kunichukulia hatua." Hawa ndio hao farasi wanaogoma kunywa maji si kwa sababu "huwezi kumlazimisha farasi kunywa maji" bali wanamuona "mshikaji" zaidi kuliko rais.

2. Magufuli anaweza kuingia kwenye historia ya Tanzania na pengine beyond kwa kugawa vyeo kwa watu wa kitengo. Nadhani katiba inamruhusu, lakini hata kama ingekuwa haimruhusu, Magufuli amejitanabaisha kuwa mtu asiyejali sheria. Kuna matatizo mawili katika kukitegemea kitengo kama pool ya kuteua viongozi mbalimbali. Kwanza, we all know how useless TISS is. Hili halihitaji mjadala. Goes without saying kuwa ni vigumu kwa taasisi useless kuzalisha watendaji wazuri. Kwa maana nyingine, kitengo is a wrong place kuwa pool ya viongozi watarajiwa.

Pili, wengi wa watendaji wa TISS wana mapungufu. Hiyo ni mada nyingine lakini matatizo yanaanzia kwenye mfumo wa ajira na oversight.

Kingine, ni preconception miongoni mwa watu wengi wa kitengo kuwa wanaogopwa na "raia" (watu wasio maafisa wa kitengo). Whether ni kweli wanaogopwa au la, most of them huwa kama wana dharau flani kwa "raia" including wale waliowateua kushika nyadhifa za "kiraia."

Kadhalika, kuna some sense of entitlement, kwamba "nimeteuliwa kwa sababu mie mtu wa Kitengo." And to make matters even worse, wengi huamini kuwa hata wakitumbuliwa, wataweza kurudi kitengo. Basically, they have nothing to lose wakiboronga huko wanakopewa madaraka.

Umeeleza kirefu kuhusu huyo bwana aliyegomewa na farasi kunywa maji lakini hujampatia ushauri "rafiki" yako. Tukumbuke kuwa rafiki wa kweli ni yule sio tu atakusifia ukitenda vyema lakini pia atakukosoa unapokosea.

Mie kama wewe ni watu tuliompigia kampeni Magufuli. Whether mchango wetu ulisaidia au la, sio muhimu. Lakini baadhi ya wenzetu mmeamua kubaki kwenye campaign mode na kuvaa miwani za mbao ambapo kamwe hamtaki kumkosoa.

Magufuli hawezi kufanikiwa katika ndoto zake za "kuikomboa Tanzania" endapo ataendelea kuwekeza katika siasa za chuki. Kukandandamiza haki za wapinzani na media kunaweza kumfanya atawale kwa amani lakini moja ya athari za wazi ni kwamba itamuwia vigumu kufahamu madudu ya watendaji wake (hasa ikizingatiwa kuwa kitengo ni kimeo: kina uhaba wa skills za intelligence na kinakabiliwa na tatizo hatari la uzalishaji taarifa feki).

Way forward, ninyi wapambe mnapaswa kuanza kukemea makosa/mapungufu sambamba na kushauri. Pia mnapaswa kupigia kelele umuhimu wa umoja wa kitaifa badala ya hizi siasa za chuki ambazo kwa vyovyote vile haziwezi kuwa na matokeo mazuri kwa sababu chuki huzaa chuki.

Samahani kwa mchango mrefu.

I stand to be corrected

kupaka ndege rangi ni mradi mdogo kwako Mzee ila kwa huyu Kiki man Sina hakika Kama anauwezo wa kuona udogo wa huo mradi.Nasikia tarehe moja anaenda mtwara .msikilize tu atakavyo watwisha mizigo ya mavi wenzake juu ya issue ya korosho
 
Watendaji wengi wa serikali sio wabaya kielimu. Wana shida ya ethics....wana shida ya working culture. Wengi wako kimaslahi kuliko kikazi. Hawana wanachojua zaidi ya kuhakikisha wanapata hela nyingi pale fursa inapotokea.
Rais wetu anapambana. Ukisikiliza anachosema kuhusu rushwa, unaona kabisa ana maanisha. Lakini rushwa bado ipo ndani ya serikali na kandarasi zake.
Watumishi wengi ni wala rushwa wakubwa. Kupambana na rushwa ni kazi ya aina yake.
JPM asikate tamaa...hayuko mbali sana na kutoboa kutoka kwenye lindi la haya matatizo

Wengi wameshaanza kuchoka. Wengi wanajua anamaanisha. Aendelee mbele. Atapata askari waaminifu watakaomuunga mkono.
pole Sana,kasome report za CAG ndo utaelewa Kama anachoongea ndo anachomaanisha
 
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea hao "farasi" kugoma kulazimishwa kunywa maji. Nitaorodhesha baadhi.

1. Wengi wa wateuliwa wa Magufuli ni marafiki zake kama sio ndugu zake. Wakati urafiki unaweza kuwa asset kwa maana ya "rafiki yangu ameniamini na kunipa jukumu hili, na kufanikiwa kwa jukumu hili ni kufanikiwa kwake, na kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwetu sote" urafiki pia unaweza kuwa liability kwa maana ya "hata nikiharibu hawezi kunichukulia hatua." Hawa ndio hao farasi wanaogoma kunywa maji si kwa sababu "huwezi kumlazimisha farasi kunywa maji" bali wanamuona "mshikaji" zaidi kuliko rais.

2. Magufuli anaweza kuingia kwenye historia ya Tanzania na pengine beyond kwa kugawa vyeo kwa watu wa kitengo. Nadhani katiba inamruhusu, lakini hata kama ingekuwa haimruhusu, Magufuli amejitanabaisha kuwa mtu asiyejali sheria. Kuna matatizo mawili katika kukitegemea kitengo kama pool ya kuteua viongozi mbalimbali. Kwanza, we all know how useless TISS is. Hili halihitaji mjadala. Goes without saying kuwa ni vigumu kwa taasisi useless kuzalisha watendaji wazuri. Kwa maana nyingine, kitengo is a wrong place kuwa pool ya viongozi watarajiwa.

Pili, wengi wa watendaji wa TISS wana mapungufu. Hiyo ni mada nyingine lakini matatizo yanaanzia kwenye mfumo wa ajira na oversight.

Kingine, ni preconception miongoni mwa watu wengi wa kitengo kuwa wanaogopwa na "raia" (watu wasio maafisa wa kitengo). Whether ni kweli wanaogopwa au la, most of them huwa kama wana dharau flani kwa "raia" including wale waliowateua kushika nyadhifa za "kiraia."

Kadhalika, kuna some sense of entitlement, kwamba "nimeteuliwa kwa sababu mie mtu wa Kitengo." And to make matters even worse, wengi huamini kuwa hata wakitumbuliwa, wataweza kurudi kitengo. Basically, they have nothing to lose wakiboronga huko wanakopewa madaraka.

Umeeleza kirefu kuhusu huyo bwana aliyegomewa na farasi kunywa maji lakini hujampatia ushauri "rafiki" yako. Tukumbuke kuwa rafiki wa kweli ni yule sio tu atakusifia ukitenda vyema lakini pia atakukosoa unapokosea.

Mie kama wewe ni watu tuliompigia kampeni Magufuli. Whether mchango wetu ulisaidia au la, sio muhimu. Lakini baadhi ya wenzetu mmeamua kubaki kwenye campaign mode na kuvaa miwani za mbao ambapo kamwe hamtaki kumkosoa.

Magufuli hawezi kufanikiwa katika ndoto zake za "kuikomboa Tanzania" endapo ataendelea kuwekeza katika siasa za chuki. Kukandandamiza haki za wapinzani na media kunaweza kumfanya atawale kwa amani lakini moja ya athari za wazi ni kwamba itamuwia vigumu kufahamu madudu ya watendaji wake (hasa ikizingatiwa kuwa kitengo ni kimeo: kina uhaba wa skills za intelligence na kinakabiliwa na tatizo hatari la uzalishaji taarifa feki).

Way forward, ninyi wapambe mnapaswa kuanza kukemea makosa/mapungufu sambamba na kushauri. Pia mnapaswa kupigia kelele umuhimu wa umoja wa kitaifa badala ya hizi siasa za chuki ambazo kwa vyovyote vile haziwezi kuwa na matokeo mazuri kwa sababu chuki huzaa chuki.

Samahani kwa mchango mrefu.

I stand to be corrected

Sent using Jamii Forums mobile app
Mdogo wangu Chahali acha jazba kabla ya kujenga hoja.Hata wewe ukiwa Rais hakuna jinsi ndugu zako na rafiki zako wakatosheleza kuwa wasaidizi wako.Hakuna mapambano bila changamoto,ukisoma hoja ya Ndugu Mwanakijiji kwa makini utaelewa,rudia kusoma.Hivi Ile hela uliyoahidiwa na Kinana ulishalipwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nina uhakika Rais Magufuli halali vizuri na akilala hulala kwa kushtukashtuka. Na kama huwa anaota ndoto basi ndoto zake zimejaa maluweluwe. Zinatisha; zinashtua; zinaumiza. Ni zile ndoto ambazo mtu akishtuka anajikuta amelowa jasho hadi kwenye ndevu na anatamani bilauri la maji baridi kuzimulia. Ni zile ndoto mtu ambazo huogopa hata kuzisimulia.

Ukimsikiliza Rais Magufuli mara kwa mara akinung'unika na kuhuzunika kuhusu mambo aliyoyakuta ndani ya serikali utakubaliana na mimi kuwa kuna hatari ya kuwa maji yamezidi shingo. Sipendi tena sitaki kusikia Rais Magufuli anaanza kuzama. Inapofika mahali hadi Rais anaenda kufanya mwenyewe ukaguzi wa miradi midogo kama ya kupaka rangi ndege basi bila ya shaka farasi wake wamegoma kunywa maji.

Nilipokuwa kijana mdogo kule Matimila Songea babu yangu alinisimulia kisa kimoja ambacho kilikukuwa ni cha kunifundisha maadili ya kufanya kazi kwa kujituma badala ya kusubiri mtu anifuate kila baada ya dakika kuniuliza kama nimefanya nilichotakiwa au la. Kilikuwa ni kisa ambacho baadaye ukubwani nilikuja kusikia hata kwenye nchi nyingine (kimefanana). Simulizi la jamaa mmoja aliyekuwa na farasi wake wengi ambao alikuwa anawatumia kwa shughuli zake mbalimbali za nyumbani na kwa usafiri. Alikuwa anawalisha farasi wale vizuri na kuwatunza vizuri. Aliwajengea banda zuri ambamo walikuwa wanalala na zizi lao lilikuwa ni mojawapo ya mazizi bora kabisa ya farasi.

Alikuwa pia anawatumikisha kweli kweli. Farasi - alisema mzee yule - walikuwa ni wanyama wa kazi. Aliwatumia kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalibali na pia aliwatumia kwa kufanya kazi za kilimo cha maksai. Wakati mwingine mzee alikuwa anajikuta anachanganyiwa katika shughuli zake - labda sababu ya uchovu au mambo mengi kichwani - na kujikuta akiweka mkokoteni mbele ya farasi badala ya nyuma yake na farasi wakashindwa kwenda hadi mtu amshtue kuwa ameuweka mkokoteni vibaya!

Wakati mwingine hata hivyo Mzee yule alipata shida ilipokuja zamu ya kuwapa maji farasi wake. Kuna siku moja - alinisimulia babu yangu - mzee alipata shida kuwapa farasi maji ya kunywa. Baada ya safari ndefu poleni, mzee alihisi kuwa farasi wana kiu na aliamua kuwapeleka kwenye kijito cha maji. Farasi walikwenda vizuri tu hadi kwenye kijito kile lakini hawakutaka kunywa maji yale. Mzee aliwavuta kwa kutumia rijamu na kuwachapa mijeledi viumbe wale wa Mungu lakini farasi waligoma katakata kunywa maji ya kijito kile. Mzee hadi presha ilianza kumpanda na hakuelewa kwanini hawakutaka kunywa maji yale.

Hakutaka kuendelea na safari bila farasi kunywa maji! Alipita bi kizee mmoja pale na kumkuta anahangaika kuwalazimisha kunywa maji yale. Yule bi kizee kumbe alikuwa anamuangalia kwa muda mzee wa watu anavyohangaika kuwanywesha "maji" farasi wake. Bi kizee baada ya masabahiano alimuambia mzee yule "unajua unaweza kuwapeleka farasi kwenye maji lakini huwezi kuwalazimisha kunywa maji!" Alimaanisha tu kuwa farasi wakiwa kweli na kiu hawatahitaji kulazimishwa kunywa maji. Wanachohitaji ni kujua maji yapo na wao wakiwa na kiu watakunywa! Mzee alimsikiliza ajuza yule na kuamua kuendelea na safari; na kweli farasi walifika salama alikokuwa wanakwenda na aliwawekea maji bandani na baada ya muda akakuta farasi wamekunywa maji yote ya kwenye ndoo!

Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kama hili. Anajitahidi sana kuwafanya 'farasi' wake wanywe maji lakini inaonekana kama kuna mgomo fulani hivi. Hivi ni viongozi gani hawaelewi matarajio ya Rais ni nini? Kwanini Rais azungumzie mapato ya uwanja wa taifa na mgawanyo wake; kwanini Rais ndio afikirie kutoa msaada kwa watu kama kina Peter Tino na watu wengine wengi ambao tunaona anawasaidia? Inakuwaje Rais ndiyo aende Magomeni kukagua ujenzi wa nyumba na kugundua kuna tatizo? Yaani, inafika mahali Rais anaonekana ni 'micro manager' wa aina fulani hivi.

Inawezekana watendaji wake hawajui wanatakiwa kufanya nini? Fikiria kwa mfano mojawapo ya mambo yanayotia aibu sana na kudhalilisha jeshi la polisi ni kuwa hawana uwezo, weledi na mbinu za kutoa ulinzi kwenye kijimkutano kidoto cha ACT-Wazalendo! Yaani, miaka karibu 60 ya Uhuru bado hatuna chombo kinachoweza kusema "Zitto, mna haki ya kufanya mkutano wenu, tumesikia kuna watu wanataka kufanya vurugu na sisi tupo kuhakikisha mnafanya mkutano wenu salama!" Yaani ikibidi hata kuleta 'batalioni' nzima ya FFU kuwapa ulinzi; badala yake farasi wamegoma! Wanatafuta njia ya mkato - futa mkutano!

Labda farasi hawa wanafikiria wanamfurahisha Magufuli. Upande mmoja unaweza kuona ni kama utani lakini inawezakana ni kweli. Kuna wanaokumbuka wiki chache tu nyuma Rais Magufuli - maskini wa Mungu - alijikuta analalamikia utekwaji wa Mohammed Dewji; alinyoshea jeshi la polisi jinsi gani lilishindwa hata kutoa maelezo nini kimefuatia. Sasa tukifuata mantiki inawezekana kweli jeshi letu siyo tu halina uwezo wa kulinda "vimikutano" kama vya kina Zitto bali halina weledi wa kufuatilia tukio zito kama la kutwa kwa MO! Hili hata mimi lingenikosesha usingizi!

Swali kubwa ni Magufuli afanye nini? Kama farasi wake wanamgomea hivi kiasi kwamba inamlazimu yeye mwenyewe, makamu wake au waziri mkuu kwenda kufuatilia? Inanikumbusha kisa kingine - nilichowahi kukisimulia hapa huko nyuma - cha jamaa waliokuwa wamelazimika kulisikuma gari kulitoa kwenye matope. Baada ya gari lao zuri kukwama kwenye matope licha ya kuwa ni 4 x 4 walijikuta wanahitaji kulipa nguvu ya ziada ili litoke. Baada ya jitihada zao zote walifanikiwa kulikwamua kwenye matope. Gari lilikuwa limechafuka nyeng'enyeng'e na harufu ya moshi ilikuwa pande zote. Cha kushangaza baada ya kulisafisha dereva akawaambia waendelee kulisikuma! Gari lilikuwa linawaka na mifumo yake mbalimbali ilikuwa inaweza kufanya kazi; lakini dereva kwa sababu hakutaka likwame tena akaamua abiria wake walisukume!

Rais Magufuli asije akajikuta anakosa usingizi na kukabiliwa na matatizo ya moyo au msongo wa mawazo kwa sababu anawaza sana juu ya kulisukuma gari hili la Tanzania. Labda umefika wakati - sijui kwa uhakika - anapaswa kuangalia ni nini kinaweza kufanya gari hili liende bila kupewa maelekezo toka "juu". Kwamba kila mtu anajua wajibu wake chini ya Katiba na akautekeleza bila kuhofia kutumbuliwa, kuudhi mtu au kuonekana haendani na "juhudi".

Ngoja niwaulize kitu; wote tushasahau mambo ya 'madawati' kwa vile Rais 'kasahau'! Wote wamesahau masuala ya usafi kwa vile tu Rais hafanyi tena usafi; wote wamesahau mambo mengi ambayo Rais aliyaanzisha na sasa wanasubiria kudakia tu atakachosema Rais. Halafu akija kuwatumbua watasema Rais Mkali sana! Fikiria hili la kupaka ndege rangi; yaani wapo watu kabisa wanafikiria wanaweza kufanya hili na hadi taarifa zinamuendea Rais Ikulu na yeye apige mkwara! Katibu Mkuu wa Wizara yuko wapi?

Mwisho wa siku tusije kuwa kama yule mama ambaye alimdekeza sana mtoto wake kiasi kwamba wakati wa harusi yake alijikuta amejikojolea... mama akataka kuwahi kwenda kumtafutia 'nepi'... eh hili nalo nilisimuliwa na babu yangu kule Matimila, Songea. Kisa cha siku nyingine.
Mtizamo wako,uheshimiwe,ngoja waje tulinganie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom