Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Umeshawahi kujiuliza, hivi ukikamatwa na polisi, ukafunguliwa kesi, ukakaa mahabusu mwaka mzima kupisha uchunguzi ukamilike, baadaye ukaachiwa kwakuonekana hukuwa na hatia, nani anayekufidia hasara ya muda, maumivu na haiba yako inayotokana na kadhia hii?
Jambo hili ndio msingi wa masharti ya Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Tanzania. Kifungu hiki kinasema "Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo"
Natambua kazi kubwa inayofanywa na law enforcement agencies pamoja na mahakama kama chombo cha utoaji haki katika jitihada za kudumusha utawala wa sheria. Hata hivyo utashi kwamba 'maadam tunaisha' kwa namna moja au nyingine, siku moja twaweza kujikuta ni wateja wa hivi vyombo, hivyo basi tunao wajibu na kwakweli hatuna budi kufanya tathmini ya mwenendo wa haki jinai hapa nchini kwetu.
Kimsingi mtuhumiwa sio muhalifu, hili ni takwa la katiba yetu. Lakini ni ukweli ulio wazi kuwa hili linatekelezeka kwa makosa yanayodhaminika tu. Inapotokea ukatuhumia kutenda makosa yasiyodhaminika kama uhaini, ugaidi, mauaji n.k; utekelezaji wa dhana ya mtuhumiwa sio muhalifu huwa ni changamoto. Uzoefu wa mashtaka ya aina hii, ni kuwa mara baada ya kutuhumiwa, utakamatwa na kuwekwa gerezani kipindi chote cha upelelezi na kipindi chote cha kusikilizwa kesi yako, haya yote yakiwa hakijulikani yatachukua muda gani kumalizika.
Mwanya huu wa makosa yasiyodhaminika, ni uchochoro unaoweza kutumika vibaya kumkomoa mtu yoyote yule kwa misingi ya chuki binafsi au hata ushindani wa kisiasa. Kwakifupi unaweza kupewa tuhuma za kufanya mipango ya ugaidi, wenye nchi yao wakakusweka lupango, huku wakiendelea na upelelezi mpaka watakaporidhika wamekukomesha vya kutosha, mwisho DPP anaiambia mahakama hana nia yakuendelea na kesi au mahakama inakuachia kwa kukosekana kwa ushadi. Hebu fikiri hasara ya muda uliopotezewa, maumivu uliyoyapata na fedheha ya kukaa jela bila hatia, ni nani atakufidia?
Haya mambo ni mambo makubwa na pengine hatuyazungumzii sana kwasababu tunahisi hayatuhusu. Lakini ni vyema tukadai mageuzi ya mifumo kandamizi kama hii. Tunaweza kukubaliana, na bunge likatunga sheria, kuwa ukitaka kumshtaki mtu kwa kosa lisilodhaminika, sharti upelelezi uwe umekamilika na uwe na ushahidi tayari. Hii itatusaidia sana kuendeleza na kudumisha utawala wa sheria na utunzaji wa haki za binadamu.