Ingependeza zaidi kama Maalim Seif Sharif Hamad angejiuzulu CUF kama hawezi kufanya kazi na Profesa Lipumba kwa maslahi ya chama cha CUF

Bwana Kheri

Member
Oct 31, 2018
26
49
Kama kichwa cha habari kinavyosadifu hapo juu. Kwakuwa mzozo wa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba mwenyekiti wa CUF Taifa aliyejiuzulu na kurejea kwenye nafasi yake hiyo bado ni mkubwa katika kambi mbili yani upande wa Lipumba na ule wa Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad. Na kwakuwa Maalim Seif ameapa hawezi kufanya kazi na Lipumba? Na kwakuwa Maalim Seif uwezo wa kumtoa Lipumba hana ndani ya CUF Taifa!

Na kwakuwa walioshindwa kufanya naye kazi wote wakiwamo baadhi ya wabunge na madiwani walijiuzulu na kuhamia CCM, akiwamo Mtolea na wengineo! Kwa maslahi ya CUF Taifa Bara na Visiwani, Maalim Seif haoni kuna haja ya kuachia ngazi ili nafasi yake ijazwe na mwana CUF mwingine mwenye ndoto za kuiongoza CUF?

Nasema hivi kwa sababu uwezo wa kumuondoa Lipumba ofisini hana, amekosa nguvu upande wa Bara na hata visiwani si kama Maalim Seif tunayemjua ngangari kinooma.

Ikiwa kujiuzulu CUF hataki, haoni anapaswa kukaa chini na watu wake pamoja na Lipumba ili kumaliza mzozo huu. Ama ndio Maalim Seif anataka CUF ife ili wakose wote akiamini Chadema itambeba Zanzibar 2020?

Kama anaamini hayo anajidanganya kwa sababu Wazanzibar kuamini Chadema ni ngumu zaidi kuliko kumbeba nguruwe kwenye chai maharage zao.
 
Back
Top Bottom