Ingelikuwa wewe utafanyaje!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ingelikuwa wewe utafanyaje!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mdondoaji, Jul 14, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asubuhi ya leo nimefika ofisini na kukaa chini kuanza kazi.

  Kama kawaida ya siku za kawaida baada ya kupata kifungua kinywa katika mgawaha katikati ya jiji la Dar nikaona leo ni siku ya kuchapa kazi kwa nguvu zote. Ilipotimu mida ya saa nne asubuhi ameingia mfanyakazi mwenzangu wa kike na tumekuwa tukifahamiana kwa muda mrefu hapa kijiweni (kazini). Dada huyu mzuri na amejaaliwa kimaumbile na ni msomi tulisoma wote pale kwenye mlima wa dar. Kwa bahati mbaya au nzuri amekuwa katika mahusiano ya muda mrefu bila ya mafanikio ya kupata mtu aliyeserious katika maisha yake. Kwa bahati mbaya au nzuri mie sio katika hao waliobahatika kumpata ijapokuwa nilivutiwa naye sana chuoni.

  Imepita miaka tumekutana ofisini na kufanya kazi pamoja na tumekuwa marafiki wa karibu sana. Mie binafsi nimepata mwenza na tunafurahia ndoa yetu kwa muda mrefu nashukuru mungu. Karibuni, kwa kipindi cha mwezi nyuma dada yangu huyu alinifuata kwa ushauri kuhusu mpenzi wake anayeishi naye muda mrefu ila hana shukrani na anamsaliti ijapokuwa anampenda sana. Binafsi nilichomshauri ni kwamba mimi siwezi kumshauri kuhusu jambo lililokuwa moyoni mwake isipokuwa ingelikuwa mie binafsi sitapendelea kuwa mtumwa wa kupenda kwasababu mapenzi ni sharing responsibility. Isitoshe, mwanaume au mwanamke anayemsaliti mkewe au mumewe hafai kuwa mumeo au mkeo. Ikiwa utaruhusu mtu akutawale kifikra utakuwa mtumwa wa mapenzi na inaweza kukuathiri kimaendeleo, kifikra na kiafya pia.

  Nikasikia ofisini ameachana na mchumba wake (ijapokuwa hakunifuata kunitaarifu mwenyewe) na anatafuta mchumba wa kuishi nae maisha. Leo ndio amenifuata ofisini na kuniomba kitu sijapata kusikia maishani. Amenitaka radhi sana nisije kumuona muhuni ila ameniomba nizae nae tu halafu majukumu ya mtoto yeye atayamudu mwenyewe pasina kunisumbua. Kali ya yote ameniambia sina haja ya kufanya naye tendo la ndoa ila naweza kumpatia maji yangu ya uzazi kuna kliniki South Africa ataenda kuziweka katika mfuko wake wa uzazi.

  Nikaona wacha nifikiri kwanza maana hii kali!!!!
  a. Nikizaa naye atanihakikishia vp hatonisumbua katika malezi ya mtoto hata kama maisha yakibadilika baadae?

  b. Mke wangu akisikia nimezaa nje ya ndoa (wanawake wa kiafrika na fikra zao tunawajua wenyewe) si itakuwa kasheshe la nguvu?

  c. Je nikimkatalia urafiki wetu utaendelea au ndio utageuka kuwa uadui?

  d. Je mtoto akitaka kumjua baba yake au baba akiwa anataka kumufahamu mtoto itakuwaje?


  Naona ninapata masuali mengi kuliko majibu nawaulizeni nyie Je ingelikuwa wewe ungelifanyaje kwasababu ameumbika huyu dada na angelikuwa anataka za chap chap ningelimpa ila hili la mtoto mh?
   
 2. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  umeleta maneno mengi na kumbe unataka watu wakuambie ule au usile, kwanini ulianza ana mwili mzuri sijui mara ningelipiga chapu chapu na huku unasema mtu akienda nje ya ndoa si wa kuishi nae wewe unataka kufanya nini?

  anza mapema jee na mkeo akimkumbuka aliyekuwa akimkosesha usingizi nae vipi?
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Ndugu epuka hilo balaa bado mapema!Hana maana huyo!
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Sina haja ya kutembea wala shida ya kutembea naye ila katika wanawake walioumbika ofisini hapa huyu nafikiri ndio mrembo wetu. Tatizo ni kwamba anapenda wanaume wenye kipato kushinda yeye. Isitoshe namuheshimu sana mke wangu na nilijiwekea nikishaoa sitamsaliti hivyo naiheshimu sana ndoa mkuu na watoto wetu. Kuumbika ni sifa yake huyu mrembo wetu na analijua hilo mwenyewe.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nianze mapema kwa maana nihame ofisini, nimchunie au nimkatalie? Je nikimkatalia itakuwaje si unafahamu ofisini tunafanya kazi kwa ushirikiano akiwa adui yako atakupa ushirikiano kweli? Nikimchunia pia ataona nimedharau na hivyo atanisumbua kuniulizia kila mara jambo silitaki.
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hii scrpt ungepelekea kanumba_ingekua poooooooooa!....anyway inafikirisha na kuchangamsha akili
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mmmh!! Hii stori inavutia sana.............inatufundisha tujiweke mbali na hatari!!!!
   
 8. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kaka mkimbie kaka huyo hakufai
   
 9. charger

  charger JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Acha urongo mkuu we unamezea mate huo mzigo,na yeye anakutega tu yani hayo maji unayoyasema anajua kabisa huwezi kusimama kwenye daladala wakati seat zipo.
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo kamanda nitamkimbiaje wakati nakutana naye kila siku ofisini? Kama sijamuona nikiingia asubuhi ofisini nitakutakana naye lunch, au corridor za ofisi au mlangoni. Kuacha kazi itakuwa ngumu maana ndio mlo wa familia unatokea hapo. Ndio kwasababu nakosa majibu ya wapi nitokee ametibua plan zangu za leo acha tu!
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kummezea mate mkuu sio mimi ni sote hapa ofisini. Kuna siku alikuja ofisini kuniletea mafile na nilikuwa na wenzangu wanaume alivaa suruali ilimpendeza mmoja wao alikuwa alikuwa na kikombe akapaliwa kidogo amwage chai. Alipotoka gumzo likawa yeye binafsi sio siri namuheshimu sana mke wangu na I am not going against my plan kumsaliti. Kumgaia maji ya uzazi naweza kumpa mkuu shida ni mtoto!!!!

  Nilikuwa nafikiria kuandika mkataba wa adoption ila roho inanisuta mfano mama yake akifariki na ndugu zake wakamdhulumu na mimi baba yake nipo hai je nitamsaidiaje wakati nimemkana kwenye mkataba?
   
 12. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  we mdondoaji inaoneka umekwisha ndio maana uko tayari hata kupiga punyeto ili umridhishe huyo dada. Jaribu ndo utajua, pengine hata hizo mbegu zako hazihitaji zaidi ya kutaka kukudharirisha tu. Utakufa wewe shauri yako.
   
 13. G

  Gathii Senior Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  hizi stori za kutunga huwa zinalenga nini hasa?niwe mkweli sielewi lengo huwa ni nini?.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  So your advise mkuu nimkatalie point blank? Laiti ungelifahamu kazi za maofisini zinavyohitaji teamwork ungelifahamu kwanini napata shida kumkatalia straightforward.
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Unajua kuna mtu aliwahi kusema kwamba ni vizuri wakati mwingine mtu ukae kimya kuliko kuongea au kuandika. Mpaka hapa wewe unaonyesha kabisa unaelekea kuanzisha nae uhusiano na pengine mmeshakubaliana sema tu hapa unajishaua
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Kwanini umefikiria ya kutunga usifikirie ni kweli? Jukwaa hili sijawahi kuanzisha thread hii ndio ya kwanza ujue how serious I am.
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  mkatalie au ndi mara yako ya kwanza kukutana na mwanamke mrembo nini? Angalia isje ukaanza kuona mkeo anafanana na sokwe mtu!!!!!!!!
   
 18. k

  kisukari JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  usije ukakubali,ukaona ni easy.fikiria baadae,huyo dada ana frustration zake,anaona njia ya mkato ni hiyo.muheshimu kama mwenyewe unavyosema.na umueleze ukweli kuwa hicho kitu hakiwezekani.huruma huruma,saa nyengine huponza.kuhusu sperm hata kwenye internet zinauzwa.unachagua mwenyewe kama unataka mchina,muhindi,muarabu,mzungu au mtu muafrica.ni hela yako tu. wanaume wa kukupa ujauzito na kusema,wamejaa tele,kama mwenyewe yupo tayari kulea mwenyewe.lakini kama wewe una mke wako,mpe heshima mke wako,usije ukajuta,mtoto ni for life
   
 19. k

  kisukari JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  sorry nimekusudia wanaume wa kukupa ujauzito na kusepa wamejaa tele
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nitakujibu kwa mfano ndyoko,

  Ukiwa mwanasheria hasa wa makampuni kuna wanasheria magwiji (Associate Lawyers), Wanasheria wa chini (sometimes unaweza kuwaita kuruta). Kila associate anaweza kuwa na team ya watu kama 11 anaofanya nao kazi. Kila timu ina connection na network wanazozifahamu wao. Inapotokea kesi ya pamoja wanashirikiana kutokana na kuaminiana na ushirikiano wa kazi na harmony iliyopo baina ya associate lawyers.

  Ikitokea Associate Lawyers hawaelewani kesi inakuwa ngumu na kazi inakuwa ndefu kwasababu unaweza kumtafuta mtu kumbe mwenzio wanafahamiana vizuri na kusababisha kesi yako ichukue muda kukamilika.

  Sasa kwa mfano huo tufanye mimi na huyu dada ni associate lawyers na tumegombana kwa jambo dogo kama hili huoni tunaweza kuharibu kazi zetu?
   
Loading...