Ingelikuwa wewe utafanyaje!!!!

Nianze mapema kwa maana nihame ofisini, nimchunie au nimkatalie? Je nikimkatalia itakuwaje si unafahamu ofisini tunafanya kazi kwa ushirikiano akiwa adui yako atakupa ushirikiano kweli? Nikimchunia pia ataona nimedharau na hivyo atanisumbua kuniulizia kila mara jambo silitaki.

Kwahiyo mwanamke yeyote atakeyevutiwa nawe hapo ofisini...........akija hutamkatalia ili ushirikiano wa kazi uwepo?

Acha sababu za ajabu..................halafu wewe unaonekana kumtamani tangu siku nyingi..............acha kutafuta matatizo,mwambie hapana!
 
Nimesoma shauri zote hapo juu. na kinacho nishangaza unapinga kwa njia moja au nyengine. so we vulia maji nguo yakoge2 ajali kazini 'inzi kufia kidondani ni hakiyake' mungu ka2leta duniani 2ongezane. ila kiukweli mimba ikikaa jua jukumu la kulea unalo hiyo nigia ya kukupata. laiti kungekuwa na vidonge kwa wanaume vya kuzuia mimba ningekwambia 2mie ili ufaidi urembo unao utolea mimacho na udenda. ila chondechonde kupima ukimwi lazima usije ukampelekea mwenzio gonjwa. maisha matamu bila maradhi

Mawazo mengine nimeyakataa na mengine nimeyakubali. Wazo nalokubaliana nalo ni la kuachana naye kabisa ila vipi nimuambie ndio kizuizi . Mjadala wangu ni vp nimuambie akanielewa yakaishia kama ni pepo mbaya amepita baina yetu.
 
Kwahiyo mwanamke yeyote atakeyevutiwa nawe hapo ofisini...........akija hutamkatalia ili ushirikiano wa kazi uwepo?

Acha sababu za ajabu..................halafu wewe unaonekana kumtamani tangu siku nyingi..............acha kutafuta matatizo,mwambie hapana!

Ballerina,

Kuniambia kuwa nisimsifu mwanamke alivyo ni ngumu kama mwanaume yeyote rijali mwanamke mzuri akipita mbele yake atavutiwa naye tu. Mbona akina mama nyie humsifu mwanaume anayepita mbele yenu sisi kwanini tusimsifu mwanamke? Cha msingi ni kushinda majaribu na unaposema namtamani sio kweli najitahidi sana kusema na moyo wangu na kumshinda shetani asinipoteze.
 
Asubuhi ya leo nimefika ofisini na kukaa chini kuanza kazi.

Kama kawaida ya siku za kawaida baada ya kupata kifungua kinywa katika mgawaha katikati ya jiji la Dar nikaona leo ni siku ya kuchapa kazi kwa nguvu zote. Ilipotimu mida ya saa nne asubuhi ameingia mfanyakazi mwenzangu wa kike na tumekuwa tukifahamiana kwa muda mrefu hapa kijiweni (kazini). Dada huyu mzuri na amejaaliwa kimaumbile na ni msomi tulisoma wote pale kwenye mlima wa dar. Kwa bahati mbaya au nzuri amekuwa katika mahusiano ya muda mrefu bila ya mafanikio ya kupata mtu aliyeserious katika maisha yake. Kwa bahati mbaya au nzuri mie sio katika hao waliobahatika kumpata ijapokuwa nilivutiwa naye sana chuoni.

Imepita miaka tumekutana ofisini na kufanya kazi pamoja na tumekuwa marafiki wa karibu sana. Mie binafsi nimepata mwenza na tunafurahia ndoa yetu kwa muda mrefu nashukuru mungu. Karibuni, kwa kipindi cha mwezi nyuma dada yangu huyu alinifuata kwa ushauri kuhusu mpenzi wake anayeishi naye muda mrefu ila hana shukrani na anamsaliti ijapokuwa anampenda sana. Binafsi nilichomshauri ni kwamba mimi siwezi kumshauri kuhusu jambo lililokuwa moyoni mwake isipokuwa ingelikuwa mie binafsi sitapendelea kuwa mtumwa wa kupenda kwasababu mapenzi ni sharing responsibility. Isitoshe, mwanaume au mwanamke anayemsaliti mkewe au mumewe hafai kuwa mumeo au mkeo. Ikiwa utaruhusu mtu akutawale kifikra utakuwa mtumwa wa mapenzi na inaweza kukuathiri kimaendeleo, kifikra na kiafya pia.

Nikasikia ofisini ameachana na mchumba wake (ijapokuwa hakunifuata kunitaarifu mwenyewe) na anatafuta mchumba wa kuishi nae maisha. Leo ndio amenifuata ofisini na kuniomba kitu sijapata kusikia maishani. Amenitaka radhi sana nisije kumuona muhuni ila ameniomba nizae nae tu halafu majukumu ya mtoto yeye atayamudu mwenyewe pasina kunisumbua. Kali ya yote ameniambia sina haja ya kufanya naye tendo la ndoa ila naweza kumpatia maji yangu ya uzazi kuna kliniki South Africa ataenda kuziweka katika mfuko wake wa uzazi.

Nikaona wacha nifikiri kwanza maana hii kali!!!!
a. Nikizaa naye atanihakikishia vp hatonisumbua katika malezi ya mtoto hata kama maisha yakibadilika baadae?

b. Mke wangu akisikia nimezaa nje ya ndoa (wanawake wa kiafrika na fikra zao tunawajua wenyewe) si itakuwa kasheshe la nguvu?

c. Je nikimkatalia urafiki wetu utaendelea au ndio utageuka kuwa uadui?

d. Je mtoto akitaka kumjua baba yake au baba akiwa anataka kumufahamu mtoto itakuwaje?

Naona ninapata masuali mengi kuliko majibu nawaulizeni nyie Je ingelikuwa wewe ungelifanyaje kwasababu ameumbika huyu dada na angelikuwa anataka za chap chap ningelimpa ila hili la mtoto mh?
hapo kwenye red-watoto wanakujaga kuleta shida sana pindi wanapohitaji kuwajuwa wazazi/mzazi wao-wanaweza kumsumbua huyo mama mtu hadi ajute kwa maamuzi aliyoyafanya-cha kufanya-as long umeoa-ni bora kuachana nae
 
Mawazo mengine nimeyakataa na mengine nimeyakubali. Wazo nalokubaliana nalo ni la kuachana naye kabisa ila vipi nimuambie ndio kizuizi . Mjadala wangu ni vp nimuambie akanielewa yakaishia kama ni pepo mbaya amepita baina yetu.
Ohk hapo nimekupata kiukweli ninakupa hongera kwa uwamuzi huo. njia pekee ya kumkwepa ni lazima umuhusishe mungu so funga siku3 then katika kila siku unapo fungua mwambie mungu akuepushe nae naimani utafanikiwa kwani ww dini gani? kama muslim. soma ikhlas 3 then mwambie kwauwezo wake mungu atakuelewa unacho mwambia na hatokuwa na chuki na wewe
 
Kaka mimi naona usithubutu kumsaliti mkeo maana cku akijua unalo na c kweli hatokuja kukugasi cku za usoni na it seems anatafuta mahala popote regardless of what will hapen next so the best thing u must tell her frankly you wont do that
 
Naona kama huwezi kum-face na kumwambia hutaki. Kama kweli unaipenda ndoa yako, tafuta cheti feki cha HIV+ ukishakipata, mwambie ungependa kuwa naye lakini ndo hivyo tena hauko salama, akitaka ushahidi mwonyeshe!
 
Ballerina,

Kuniambia kuwa nisimsifu mwanamke alivyo ni ngumu kama mwanaume yeyote rijali mwanamke mzuri akipita mbele yake atavutiwa naye tu. Mbona akina mama nyie humsifu mwanaume anayepita mbele yenu sisi kwanini tusimsifu mwanamke? Cha msingi ni kushinda majaribu na unaposema namtamani sio kweli najitahidi sana kusema na moyo wangu na kumshinda shetani asinipoteze.

Sasa kinachosababisha ushindwe kusema ni kipi?.....................................................
Mwambie umejadili na mkeo kwa kuwa mbegu ulizonazo ni za familia (zako na mkeo)...................lakini mkeo kakataa........na kama mkeo angekuwa radhi..............we usingekuwa na pingamizi.

Na umuulize..............yeye angekuwa na mume.............................angekubali kutendwa hayo?..............................
Mbona hao wanaomcheat kawakimbia.................si angeomba mbegu kwao.................kama shida ni mbegu tu????

Utaingia mtegoni muda si mrefu............................chukua tahadhari.
 
Mkuu jambo hili lilinitokea mimi na liliniletea madhara makubwa utaipata hapahapa MMU thread yake kwa jina la Jambo limezua jambo,naomba uisome kwanza kabla ya kuamua utafanya nini.
 
huko sa hakuna sperm bank kwenye hyo hosptl? Mpaka atake zako?

Hili nalo neno lakini mie sijui sababu zake za kutaka sperms zangu na wala sitaki kujua kwani nakaribisha mjadala nisioutaka bora nisifahamu kabisa.
 
Sasa kinachosababisha ushindwe kusema ni kipi?.....................................................
Mwambie umejadili na mkeo kwa kuwa mbegu ulizonazo ni za familia (zako na mkeo)...................lakini mkeo kakataa........na kama mkeo angekuwa radhi..............we usingekuwa na pingamizi.

Na umuulize..............yeye angekuwa na mume.............................angekubali kutendwa hayo?..............................
Mbona hao wanaomcheat kawakimbia.................si angeomba mbegu kwao.................kama shida ni mbegu tu????

Utaingia mtegoni muda si mrefu............................chukua tahadhari.

Ballerina,

Usijali ndugu yangu nishaandika barua pepe kumjibu itashindikana hilo ombi lake nasubiri kesho akiingia ofisini atakutana nayo au pengine usiku huu ameshaisoma. Nasubiria reaction yake itakuwaje kuanzia kesho.
 
Mkuu jambo hili lilinitokea mimi na liliniletea madhara makubwa utaipata hapahapa MMU thread yake kwa jina la Jambo limezua jambo,naomba uisome kwanza kabla ya kuamua utafanya nini.

Mkuu,

Nishafanya maamuzi ya kutuma barua pepe kukataa ombi lake, ila nitasoma kupata maujuzi zaidi. Nawashukuruni sana kwa ushauri wenu. Alamsiki!
 
sasa wewe unataka uambiweje?yaani nikuonavyo mimi unataka uambiwe kuwa mkubalie ndo utafurahi! unaonekana maadili huna kwa nini unaogopa kumkatalia kisa teamwork,hapo hapo eti unampenda mkeo ahghaa.... kwani hiyo mimba anayotaka ina uhusiano gani na kazi?mkienda kula mwambie ukweli sitaki mpango wako wa mbegu zangu coz ni za mke wangu hahahaha ....... then mwambie lakini teamwork iko palepale la sivyo ntakutangaza kwa wafanyakazi wote,utaona atakuwa dada yako kabisaaa.....ila kama ulikuwa unataka JF ikupe go ahead umkubalie... mi sijui tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom