Ingelikuwa hivi tungefika mbali

luckyperc

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
495
46
Wanajamvi habari za kwenu:

Poleni kwa majukumu ya kulijenga Taifa ambalo limejaa wajanja ambao wanauwezo wa kuzichezea akili za Raia jinsi wanavyoweza.

Hivi mwakilishi wetu(mbunge au diwani) akienda kuuliza mradi wowote uliotakiwa kufanyika katika jimbo au kata yake kwenye mamlaka husika ili kesho na keshokutwa akisimama kwa wananchi ajue la kuwajibu.

Lakini ninachoona nitofauti, hivi ukiuliza je ya madarasa,vyoo,barabara,maji safi yaliyotakiwa kutekelezwa yamefikia wapi? siwatakupa majibu! wakati mwakilishi wetu ni mmoja wa wanakamati wa mradi huo anakuwa anaelewa yalitakiwa kumalizika kwa kipindi fulani. Akiona hajaridhika akiwafuata wananchi(NGUVU YA UMMA) na kuwaeleza waende kudai haki yao itakuwaje? kuliko kupoteza nguvu kuita umati mkubwa nakuanza kutoa lawama, nafikiri ni bora diwani akiwaita wananchi wake kwenda kwa mtendaji wadai haki wakiona vipi wa apply njia mbadala ya kumtia adabu!

Inauma sana kuona tunafanya mikutano mingi kuimarisha chama ili hali maendeleo hakuna!
Je Tundu Lissu akimwambia Dr slaa/kikwete kuna visima vilitakiwa kujengwa lakini havijatekelezwa wakienda kwa mkurugenzi wa wilaya kudai, wasiporizika wakaleta NGUVU YA UMMA MLANGONI KWAKE KAMA WANAVYOFANYA KWENYE MIKUTANO itakuwaje? Z.KABWE, IDDI AZZAN, ZUNGU, H. MDEE, NYAMBARI, KAFULILA, MAHANGA, MALECELA, TYSON woooote hawa wakifanya hivi tutafika MBALI kweli.


Hawa watendaji bila kuwapelekesha hawatekelezi majukumu, tukikaa kwenye mkutano tu halafu ukamtaja tu HAZITASAIDIA atajulikana tu bila kuwajibishwa.

chondechonde tubadilike tuanze kuwamaliza hawa sisimizi kabla ya kwenda kwa siafu!

NAWASILISHA!
MTAZAMO TU.
 
Ndugu yangu luckyperc utakaa sana na mawazo chukua hatua njema 2015 kama utakuwa umetimiza miaka 18 tafuta na wenzoko kama 200 muingie cdm ndiyo dawa kuliko kuchanganya hayo majina hapo juu.....
 
Back
Top Bottom