Ingekuwa inaisha kama penseli angeshabaki na kifutio

Billion Dolar

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
1,260
2,865
Mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy alimbaka msichana mmoja kisha akamwambia "ni sawa, nimefanya ngono na wanawake 10,000", mahakama imeambiwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka 24 wakati huo, kwenye jumba lake la kifahari la pauni milioni 4 huko Mottram St Andrew, Cheshire, Oktoba 2020.

Pia anatuhumiwa kwa jaribio la kumbaka mwanamke mwingine, mwenye umri wa miaka 29 wakati huo, ambaye alisema pia alimshambulia nyumbani kwake miaka miwili kabla.

Mwanasoka huyo amekanusha mashtaka yote mawili.

Anakabiliwa na kesi katika mahakama ya Chester.

Jopo la wazee lenye wanawake sita na wanaume sita limeambiwa na Jaji Stephen Everett, Msajili wa Chester, kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipatikana hana hatia ya makosa ya kingono yanayodaiwa na wanawake wengine baada ya kesi iliyomalizika Januari mwaka huu.

Aliwaambia wazee hao mara ya mwisho hawakuweza kufikia uamuzi juu ya mashtaka mawili wanayosikiliza, ya ubakaji na kujaribu kubaka, hivyo basi kusikilizwa tena kwa mashtaka hayo mawili.

Jaji aliwaonya kutotafuta maelezo ya kesi iliyopita au kufuata habari kwenye vyombo vya habari, na kuamua tu kesi kuhusu ushahidi uliosikilizwa mahakamani katika kesi ya sasa.

Alikuwa akifanya karamu na mikusanyiko ya kijamii nyumbani kwake, The Spinney, huko Mottram St Andrew, Cheshire.

"Alikuwa na wageni wa kiume na wa kike kwenye mikusanyiko yake ya kijamii.

"Ni wakati huo ambapo mara mbili Bw Mendy alitumia fursa ya wagenin hao wawili wa kike.

"Wakati mmoja alijaribu kufanya mapenzi ya lazima na mgeni wa kike, mwanamke A.

"Katika tukio lingine alimbaka mgeni wa kike katika moja ya vyumba vyake vya kulala, mwanamke B."

Bw Aina alisema Bw Mendy alikutana kwa mara ya kwanza na mwanamke A, mwanafunzi wa Uingereza, akiwa katika klabu ya usiku huko Barcelona mwishoni mwa 2017 na akawa na urafiki wa karibu na mmoja wa marafiki zake.

Waliendelea kuwasiliana na mwaka mmoja baadaye alipanga kwenda kumtembelea rafiki wa mshtakiwa kwenye nyumba ya mwanasoka huyo, ambapo walikaa baada ya wote kwenda na wasichana wengine kwa mapumziko ya usiku.

Asubuhi iliyofuata, alipoingia bafu ya chumba cha kulała kuoga, Bw Mendy alionekana bila kualikwa, akiwa amevalia kaptura tu na "alisisimka", mahakama iliambiwa.

Mwanasoka huyo ndipo anadaiwa kumshika mwanamke huyo na kujaribu kumbaka kitandani alipokuwa akijitahidi kumsukuma, licha ya kumwambia mara kwa mara aache.

Miaka miwili baadaye, mwanamke B alikuwa ametoka na marafiki zake kwenye baa moja huko Alderley Edge, Cheshire, karibu na nyumbani kwa Bw Mendy, walipoalikwa kwa nyumba ya mwanasoka huyo.

Anadai mshtakiwa alimnyang'anya simu yake, iliyokuwa na picha za "ndani", kisha kumpeleka kwenye chumba chake cha kulala kilichofungwa, huku akiomba arudishiwe simu yake.

Bw Aina alisema Bw Mendy alimwambia "Nataka tu kukutazama" na kumwambia avue nguo zake.

Mwanamke B alitii, akiiacha nguo yake ya ndani, kisha Mr Mendy akaitupa simu yake kitandani.

Alipokuwa akienda kuichukua, mwanasoka huyo anadaiwa kumshika kwa nyuma na kumbaka licha ya kumwambia hataki kufanya ngono.

Bw Aina aliambia baraza la wazee: "Katika hatua hii Bw Mendy alirudi nyuma na kusema 'una haya sana'.

"Bwana Mendy alisema, 'Ni sawa. Nimefanya mapenzi na wanawake 10,000'."

Mchezaji huyo aliwaambia polisi katika hafla zote mbili mawasiliano yoyote ya ngono yalikuwa ya makubaliano na anakanusha makosa yoyote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom