Ingekuaje kama mtu angeijua siku yake ya kufa?

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,236
14,205
Salaam,

Linapotajwa neno "KIFO" watu huwa ni waoga sana kutokana na usiri wake.

Tafiti zinasema katika mambo ambayo yanamuogopesha binadamu zaidi, jambo la kwanza ni kifo.

Sasa nikawaza na kujiuliza sana hili swali. Hivi ingekuwaje watu wote wangejua siku yao ya mwisho ya kuishi hapa duniani?

Yaani mtu anapozaliwa tu tayari anajua kama ataishi miaka 50.

Ingekuwaje?

Mambo mengi yakaanza kuja kichwani kama ifuatavyo:

1. Mtu asingekuwa na uoga wa kifo kabisa, mpaka siku zinapokaribia.

2. Kwenye misikiti na makanisa tungekuwa tukiwaona hasa wazee na baadhi ya vijana waliobarikiwa umri mfupi.

Hapo mpaka mtu akaribie siku yake ya kifo, miaka 5 kabla ndio ataanza kurejea kwa mungu wake.

3. Starehe na uchafu ndio vitazidi kuongezeka..

4. Uhalifu wa kila namna.

5. Hakuna kusaidiana wala kuhurumiana, japo itabaki kwa wachache sana.

Ni mambo mengi mno yangebadilika tofauti kabisa na maisha ya kawaida.

Hivi mmewahi kulifikiria hili?

Tupia mawazo yako kuhusu hili!
 
Siku husika ikifika ningekimbia Kama jehu situlii sehemu moja Yani ni mbio tu mpk kifo chenyewe kiwe kinaniambia "we fala ntakupata tu" huku kikihema!
Duh! Muda wote utakuwa bado hujajiandaa tu kisaikolojia?
 
Yani kuna watu pamoja na kujua siku fulani ndio anasepa duniani, lakini bado atajisahau tu.. Anaendelea kula ujana.

Mpaka siku inamfikia hajui!
 
Back
Top Bottom