Mpigamsuli
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 3,885
- 575
wana jf ninaomba msaada wa hili hivi ni kwa nin infixation ni very rare kutokea kweny lugha? kama izo lugha zpo ntajien!
Ninakupeni tahadhari wachangiaji. Mleta uzi anataka makini ielekezwe katika kumuelewesha habari za viambishi-kati katika huo mchakato wa uambishaji. Dotworld umejaribu kufafanua suala la uambishaji kwa ujumla na hata ulipojaribu kutoa mifano miwili hivi, umetumia maneno changamano na ambayo ni mukhari kuuchora mstari kuonesha mzizi hasa ni upi. Mchango wa hukumundo unaweza kuwa jalabati (nikiri mimi si mjuzi wa kiarabu) hasa ikiwa -ktb- kweli ni mzizi wa neno. Tatizo kubwa ninalolibaini katika neno hilo na kutilia mashaka uwezekeno wa kuitwa mzizi ni kukoseakana kwa kiambishi kingine chochote. Lakini kwa kuwa tabia ya lugha hiyo ya kiarabu siijui, mashaka yangu yanabaki kuelea hasa alivoendelea kutengeneza maneno k-a-t-a-b-a na k-i-t-a-b katika kuhalalisha viambishi-kati vilivyojitokeza katikati ya mzizi. Lugha ya Kihaya kwa mfano ina neno 'bon-a' lenye mzizi bon- lakini linaweza kubadilika kuwa 'boin-e' na hivo kusababisha mzizi wetu wa awali 'bon-' uruhusu kiambishi kingine kiingie na kuufanya mzizi huo kuonekana 'bo-i-n-' jambo ambalo ni nadra sana miongoni mwa lugha nyingi. Hata hivo niseme tu kwamba mchakato wa uambishaji ni moja ya njia zinazosaidia kuzalisha msamiati wa lugha; na kwa lugha za kibantu ambazo zinaitwa lugha ambishi-bainishi (Kiswahili kikiwemo mchakato huu hufanyika zaidi katika aina za maneno ziitwazo Nomino na Vitenzi.
Wakuu, ninawasilisha!