GE2025 INEC, NIDA wamkana Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sio kwamba wewe umeshindwa kuelewa kinachofanyika ?
Ngoja nikuulize swali... Unajua kitu kinaitwa daftari la wapiga kura ?

Ukinijibu ...nitakupa mwanga...
 
Chawa wanalinda ugali wao, kizuri mtu aliyekuwa kwenye mfumo ndiye aliyevujisha siri and whatever his motives are we don't give a damn.
 
Tulitarajia wakane au kunyamaza kimya na kumpotezea Polepole. Wamechagua kukana na hata wasipopewa maelekezo toka juu ilikuwa ni obvious kuwa wangekana.
Eniweis, sisi wananchi tumemwelewa polepole vizuri tu.
 
Duh!
 
Polepole kachoma kichaka wadudu lazima watoke.
Kule Dom vijijini kina Agwe wakishapiga ugimbi pori huwa wanachoma nyika ekari kama mia mbili, ardhi inawaka moto panya wote wanaungua huko chini wanatoka mbio kwenye mashimo yao na kukimbilia ndani kwenye nyumba za tembe za wakazi nao wanapata kitoweo bila shida wala kusumbuana just wanakamata panya na kubanika tu, sasa msimu wa mvua ukifika wanatafutana, miti hakuna na mvua hakuna!!

Vichaka ni vingi bongo!! Digidigi kalewa cha Arusha anafyeka vichaka kwa hatua! Kaanza na mchakato, sasa mifumo!
 

Jambazi hata likifumaniwa wazi wazi linaweza kukiri?



Kabla ya hapo ninkutupigia kelele tu!

Zaidi sana:

Kuingilia mifumo ya uchaguzi ni Uhaini. Lissu anashtakiwa kwa niaba yetu kwa kufanya Uhaini na tunaopaswa kuwashitaki kwa Uhaini!
 
Sio kwamba wewe umeshindwa kuelewa kinachofanyika ?
Ngoja nikuulize swali... Unajua kitu kinaitwa daftari la wapiga kura ?

Ukinijibu ...nitakupa mwanga...
Daftari la kudumu la wapiga kura, ni nakala inahifadhi orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura eneo fulani, ikiwa pamoja na baadhi ya taarifa zao muhimu.
 
Aliyetoa tuhuma ndiye mwenye jukumu la kuthibitisha hayo madai.Ukipenda kusikia kile unachopenda kukisikia bila kutumia akili zako kutafakari kuna uwezekano mkubwa ukalishwa na kuamini jambo ambalo pia sio sahihi.Ukiwa na akili timamu huwezi kua binadamu wakuamini maongezi ya mtu bila prove kwavile tu wanasemwa usiowapenda.Polepole atupatie uthibitisho ili tupime uongo wa hao waliokanusha.
 
ati sisi ni TUME HURU? Mpala mtu anakuwa jaji hajui maana ya uhuru?
huna pesa, huna watumishi huo uhuru unaupata wapi
 
Wajinga ni wengi,reasoning yetu ni kidogo sana.
 
wengi wanachangia mada kwa mihemko.Hawana akili yakuwaza kama wewe ndo maana huyo polepole nawenzake wanajua akili zetu ndo maana wanajiongelea tu wakijua kuna ambbao wanaamini maneno matupu.
 
Siku jambazi ukiona anakiri na kusema ni kweli nilikuwa jambazi, ni siku ambayo jambazi huyo ameamua kutoendelea kuwa jambazi.

NIDA na INEC ni taasisi za kijambazi kwaajili ya kuhalalisha ujambazi wa CCM. Mkiona siku moja hizi taasisi zinakiri zilivyohusika katika kuhalalisha ujambazi wa CCM, irakuwa ni siku ambayo watakuwa wameamua kuachana na huo uovu. Maadam wanaendelea na uovu, kamwe hawataukiri uovu wao.

Wangekuwa wanasema ukweli, wangeitikia wito wa Pole Pole wa kuwa tayari kuwakaribisha wataalam wa IT wakathibitishe ukweli au uwongo wa maneno ya PolePole. Kwa sababu ni waongo, kamwe hilo hawatafanya.
 
Huyo Mwambegele kachaguliwa na nani kukaa hapo? Kifupi hana jipya.

Juzi nilihudhuria mkutano na Tume huru na Waandishi wa Habari aliambiwa ukweli kuwa Tume haikubaliwi na haitakiwi na Wananchi...huyu Jaji aliwaka utadhani mwehu.
Wanahangaika kubeba hizi laana zote wakidhani zitasaidia familia zao kuja kuishi maisha ya kifalme baadae na ndo maana wanakubali kuwachambisha watu kwa ndimi zao wenyewe ..hawa ni sawa na ma maamuma
 
Daftari la kudumu la wapiga kura, ni nakala inahifadhi orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura eneo fulani, ikiwa pamoja na baadhi ya taarifa zao muhimu.
Sasa ...nikwamba ...Kuna uhuni unafanyika...

Kuna watu walikwenda kujiandikisha kweli kwenye daftari...na kuna watu hata hawakupata muda wa kujiandikisha...

Kinachofanyika ni wale ambao hawajajiandikisha Kuna sehemu majina yao yapo katika daftari ...kwa kufanya copy and paste kutoka NIDA., na ndio maana Kuna sehemu watu walikuta majina ya marehemu..mtu hayupo Duniani miaka 4 ila jina linasomeka...

Sasa daftari linakuwa na idadi kubwa ya watu..ile mbeleni isaidie kuongeza kura ...yaani Kuna watu watakuwa nyumbani ila watapigishwa kura bila kujijua...na hapo ndio kura feki zinawekwa kwenye mabox ya kuhesabia...

Najua utauliza wakala wanakuwa wapi...Hilo siwezi kukueleza...maana mawakala huwa wanapata Cha mtema Kuni vituoni...hata simu hawaruhusiwi kuwa nazo ili wasirekodi vituko... Nimejitahidi kukupa mwanga
..
 
Je wanaruhusu wakaguliwe ? Maana pole pole ka advice kama wanabisha wakaguliwe na mkaguzi huru
 
Pole pole amewaomba radhi watanzania kwa kushiriki huo uovu, mimi binafsi nimemsamehe na kama itampendeza aendelee kutoa misumali mingine kwa sababu pamba zinazotumika ni zile za kutokia Igunga ambazo hazina quality kama pamba za shinyanga
 
Ulitegemea wakiri huo uhuni? Hawana guts hizo ila Watanzania Wenye akili hatimaye wameelewa kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…