Indonesia: Jaji Mkuu akamatwa kwa rushwa

Indonesia: Jaji Mkuu akamatwa kwa rushwa

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,477
Reaction score
21,025
KWENU HAYA YANAFANYIKA? JAJI MWENYE WADHIFA MKUU KAMA HUYU ANAWEZA KUKAMATWA KWA MADAI YA RUSHWA

131003075954_indonesia_akil_mochtar_304x171_afp_nocredit.jpg

Jaji mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Indonesia amekamatwa kwa madai ya rushwa. Akil Mochtar alikamatwa na maafisa wa kupambana na rushwa kwa madai ya kupokea dola laki mbili na nusu kama rushwa nchini humo

Kwa mujibu wa maafisa hao, kukamatwa kwa Mochtar ni tukio la kwanza la hivi karibuni kukamatwa kwa afisaa mkuu wa umma kuhusiana na rushwa aliyopokea akisikiliza kesi kuhusu uchaguzi.

Mahakama ya kikatiba ya Indonesia husikiliza kesi zote kuhusiana na uchaguzi.

Bwana Mochtar alichaguliwa mwaka huu kwa muhula wa miaka mitano kwa wadhifa huo katika mahakama ya kikatiba.

Alikamatwa kwake nyumbani mjini Jakarta baada ya mfanyabiashara ambaye pia ni mbunge kumkabidhi pesa, kwa mujibu wa msemaji wa tume ya kupambana na rushwa nchini humo.

Kesi hiyo ilihusishwa na utata ulioibuka katika uchaguzi uliofanyika kisiwani Borneo.

Watu wengine wawili wamekamatwa baada ya kuhusishwa na kesi hiyo.

Mwezi jana mahakama ya kupambana na rushwa ilimpata na hatia generali wa polisi Djoko Susilo kwa kosa la kutengeza pesa haramu.

Susilo alihukumiwa jela kifungo cha miaka 10 na kutozwa faini


CHANZO: Jaji mkuu akamatwa kwa rushwa Indonesia - BBC Swahili - Habari
 
OOH MY GOD!nilishtuka nikadhani ni Tz
 
Kwa Tz ni vigumu rushwa kubwa za aina hiyo kukamatwa - watendaji wakuu vyombo vya dola wamekuwa wakihusishwa katika migao hiyo. Virushwa vidogo dogo vinavyowahusisha walala hoi ndio vimekuwa vikifuatiliwa na kuripotiwa- Rushwa kubwa zinazoyumbisha uchumi wa nchi zinalindwa kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom