Indian Soldier...oh sorry.....US Soldier

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
capt.65889e93cf2540d0ad760eecf915412f-65889e93cf2540d0ad760eecf915412f-0.jpg

U.S. Army Capt. Tejdeep Singh Rattan speaks to journalists a U.S. Army officer basic training graduation ceremony at Fort Sam Houston in San Antonio on Monday, March 22, 2010. Capt. Rattan is the first Sikh allowed to complete officer basic training while wearing the traditional turban and full beard since the Army altered the dress code, which had made exceptions for Sikh soldiers, in 1984

http://news.yahoo.com/nphotos/Most-...blicid_ap_org65889e93cf2540d0ad760eecf915412f
 
Mamluki kama hawa safi wakichoshwa mara wanakurupuka na kurembea risasi ovyo,hivi kuna Watanzania wenye asili ya kihindi katika jeshi la polisi au JWTZ, Tanzania?
 
Ooops! Na mimi nimeuliza swali hili.
 
Walikuwepo zamani. Nadhani walihama baada ya Azimio la Arusha.
Hapa napata swali la kujiuliza, hivi ni kweli haya tunayoambiwa kuwa viongozi wanaoitwa "waaasisi wa misingi" ya taifa la Tanzania,(mm siijuwi ipi hiyo misingi), walifanya kazi kubwa kuondoa mambo ya ubaguzi wa kidini,ukabila, rangi n.k kama ni kweli...mbona hakuna uwakilishi walau wa kupishana katika sekta za ajira za kiserikali,hasa katika maeneo kama hayo ya jeshi,polisi..nk,?
Na kama kweli vitu kama ubaguzi wa asili ya mtu anapotoka havizingatiwi katika mambo hayo..kwanini watanzania wengine wanaitwa kuwa ni wenye asili ya pahala fulani,mfano utasikia "mtanzania mwenye asili ya kiasia" huu si ubaguzi au...?
 
Hoja ya kijinga. Mfumo wa ajira wa serikalini unafahamika. Mwombaji ndiye mwenye maamuzi ya kuomba au kutokuomba. Sasa unataka usawa utoke wapi?

Upuuzi tu!
 
Mamluki kama hawa safi wakichoshwa mara wanakurupuka na kurembea risasi ovyo,hivi kuna Watanzania wenye asili ya kihindi katika jeshi la polisi au JWTZ, Tanzania?
Hmna jeshini ukiwa na asili hiyo wanakuchuja kwa sababu nyingine yoyote,tangu kikao cha ulinzi na usalama cha wilaya
 
Mamluki kama hawa safi wakichoshwa mara wanakurupuka na kurembea risasi ovyo,hivi kuna Watanzania wenye asili ya kihindi katika jeshi la polisi au JWTZ, Tanzania?
Enzi za Mwalimu hata wazungu walikuwemo jeshini, kumbuka vita vya Idd Amin. Sasa hivi wahindi wote ni matajiri na tumewapa sisi wenyewe.
 
Walikuwepo zamani. Nadhani walihama baada ya Azimio la Arusha.

nasikia wahindi na waarabu wapo ... ila wako zaidi kama informers na undercovers ... kuna mmoja nilionyeshwa maeneo ya mnazi mmoja ... zamani uswazi tulikuwa tunawaita waarabu/wahindi pori ... yaani waarabu/wahindi lkn wanajua mambo yote ya kiswahili (tofautisha na wamanga koko)
 
Walikuwepo maofisa wa jeshi kama canal mitta wa airforce alistaafu alikuwa mhindi sasa kusema wanachujwa si kweli hawataki tu.Walden mzungu Hans pope mgiriki akina katles na wengineo wengi tu zama hizo
 
Hoja ya kijinga. Mfumo wa ajira wa serikalini unafahamika. Mwombaji ndiye mwenye maamuzi ya kuomba au kutokuomba. Sasa unataka usawa utoke wapi?

Upuuzi tu!

True kaka,hoja nyingine zitolewe baada ya mtu ku think critically,

Majeshini kazi hutangazwa mfano JWTZ,POLISI,MAGEREZA,UHAMIAJI,nk,watu wanaomba kwa vigezo vilivyoainishwa kisha huitwa ktk usaili,labda ndg yetu alitaka waitwe watu wote hata ambao hawajaomba?

Ila anapaswa afahamu na asibishane na ukweli,hao waTZ wanoitwa wenye asili ya kiasia wengi hawataki kabisa kazi za kuajiriwa hususan Serikalini,wanaoajiriwa ni wale waoajiriana ktk kampuni za ndg zao,mjomba,shangazi nk,the rest wanaishia ktk Biashara.

Mwisho,kuna msomi alipata kunena kua

KAMA HUJAFANYA UCHUNGUZI,HUNA RUHUSA YA KUSEMA.

All the Best.
 
Enzi za Mwalimu hata wazungu walikuwemo jeshini, kumbuka vita vya Idd Amin. Sasa hivi wahindi wote ni matajiri na tumewapa sisi wenyewe.

or may be they worked hard while we were sleeping ?
 
Ni suala la ubora wa mazingira ya kazi ikilinganishwa na fursa kadhaa zilizopo. Kwa kifupi ni kuwa mazingira ya kazi za umma kwa ujumla yamekuwa yakishuka viwango kwa kasi kiasi kwamba jamaa zetu wengi wenye asili ya kiasia walianza kujiondoa taratibu kuanzia mwishoni mwa miaka ya 70 hadi kutoweka kabisa mwanzoni mwa 1980s. Ukifuatilia historia ya nchi utagundua kuwa Watanzania wa kiasia walikuwepo karibu katika fani nyingi za sekta ya umma. Uliweza kukuta walimu wa kiasia katika shule za msingi na sekondari za serikali; katika mawizara, polisi, n.k.

Naweza kuthubutu kusema kwamba nilivyoona ni kuwa watu wenye asili ya kiasia wana hulka kubwa ya ushindani kiuchumi; si rahisi kuwakuta waking'ang'ania mahali panapodorora. Kwa nini iwe hivyo? Nawaachia wenye ujuzi kuchambua.
 
Hoja ya kijinga. Mfumo wa ajira wa serikalini unafahamika. Mwombaji ndiye mwenye maamuzi ya kuomba au kutokuomba. Sasa unataka usawa utoke wapi?

Upuuzi tu!
Sawa nakubali ujinga wangu...ndo maana nauliza nipate kujuwa...nikielewa ntakuwa si mjinga au vp...bw. Mwerevu...?
Haya ww mwerevu twambie ss wajinga,huo mfumo wa serikali unaoeleweka ndo upi mpaka tunakosa watu wa asili tofauti katika vyombo vya ulinzi vya dola tofauti na wenzetu walioainishwa hapo juu?
 
Hawa wataki tu wenyewe kwani kazi za wako kimaslahi zaidi wako radhi wafanye biashara hata ndogo lakini sio kuwa chini ya mtu hasa mbongo pure.

Swali jingine la kujiuliza mbona hawa hawako vijijini?
 
Ushatembelea vijiji vyote vya Jamhuri ya Tanzania?
 
Sawa nakubali ujinga wangu...ndo maana nauliza nipate kujuwa...nikielewa ntakuwa si mjinga au vp...bw. Mwerevu...?
Haya ww mwerevu twambie ss wajinga,huo mfumo wa serikali unaoeleweka ndo upi mpaka tunakosa watu wa asili tofauti katika vyombo vya ulinzi vya dola tofauti na wenzetu walioainishwa hapo juu?

Sasa unataka nikujibu nini hapa? Unadhani ujinga unaeza kufutika bila kuzingatia kwa makini 'werevu' wamekujibu nini? Mwe!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom