India yasimamia sera yake huru ya biashara: Afisa wa cheo cha juu kutojiunga na Jukwaa muhimu la biashara ya IPEF

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Los Angeles
Afisa mwandamizi wa serikali alisema kwamba India inasimamia sera yake huru ya biashara na kuongeza kuwa kabla ya kwenda kujiunga na jukwaa hilo la biashara la pamoja la India na Pacific (IPEF), New Delhi itazingatia faida na hasara za ahadi hizo.

Akizungumzia kuhusu India kutojiunga na Jukwaa la biashara ya IPEF, afisa huyu mwandamizi aliiambia ANI, “Kuna baadhi ya masharti ya lazima ambazo zimewekwa na Marekani na hivyo India inatakikwa kuwa waangalifu,” afisa huyo aliongeza, “India inasimama kwa miguu yake, sisi. tuwe na sera yetu huru,” afisa huyo alisisitiza.

“Tutakuwa tunazingatia faida na hasara za ahadi za lazima na kisha tutachukua tahadhari wakati maelezo ya vifungu vya kisheria vinavyotuhusisha sisi katika miezi ijayo.”

Mapema , katika mkutano wa kwanza wa mawaziri huko Los Angeles,mwakilishi wa biashara wa Marek Katherine Tai alithibitisha kwamba India itajiunga na jukwaa hilo la biashara ikiwa ni moja ya majukwaa manne yanayounda mfumo wa uchumi wa Indo-Pacific(IPEF)

“India sasa haiko katika Jukwaa la biashara ya IPEF, Waziri wa Biashara wa Muungano Piyush Goyal na Mimi tumekuwa kizungumza sana,Tuna muundo wetu wa nchi mbili Jukwaa la Sera ya Biashara, ambalo linatarajia kukutana tena mwishoni mwa mwaka huu na tuliangazia maswala yanayofanana katika mkondo huo wa nchi mbili na mawaziri tunawasiliana kwa karibu sana,” Tai alisema.

Waziri wa Muungano wa Biashara na Viwanda Piyush Goyal alisema Ijumaa iliyopita kwamba Mfumo thabiti wa Uchumi wa India na Pacific kwa Maendeleo (IPEF) unapendekezwa kuwasilishwa hivi karibuni Bungeni, na India itachukua maamuzi yake juu ya nyanja tofauti kulingana na masilahi yakitaifa.

Goyal alisema kuwa India ni mzalishaji mkubwa wa huduma za teknolojia kwa kampuni za Marekani na Makubaliano haya yanayopendekezwa yatawasilishwa Bungeni hivi karibuni.

“India inatazamia kuwa na sheria za zinaendana na wakati na za kisasa katika ulimwengu wa kidijitali huku ikidumisha viwango vya juu vya faragha ya taarifa (data),” aliongeza.

Alisema kuwa ndani ya Mkataba huo wa makubaliano, "tunaweza kuanza kushirikiana kati ya nchi wanachama katika maeneo tofauti yenye kugusa maslahi ya pande zote. India itachukua maamuzi yake juu ya vipengele tofauti vya Mkataba wa IPEF kwa kuzingatia maslahi yetu ya kitaifa.

Tulikuwa na ushirikiano wenye manufaa kati ya nchi wanachama wa Mkataba wa Uchumi na maendeleo wa India na Pasifiki. Maafisa wamefanya kazi kuandaa mazingira ya mahusiano yenye manufaa baina ya mawaziri.Kufikia kesho tunatarajia kuunda Mwongozo thabiti,” Goyal alisema.

Waziri wa Muungano Piyush Goyal yuko katika ziara ya siku sita huko San Francisco na Los Angeles kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa Jukwaa la Uchumi wa Indo-Pacific (IPEF). Goyal alikutana na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Katherine Tai kabla ya mkutano huo.

“Pia nimepata fursa ya kuwa na majadiliano baina ya nchi mbili na Mwakilishi wa Marekani wa biashara Balozi Tai na Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo. Wote wawili walifurahishwa sana na kazi nzuri inayofanyika kati ya India na Marekani,” Goyal alisema.

“Walifurahishwa sana kupanua uhusiano katika biashara na uwekezaji ikijumuisha maeneo ya Teknolojia ya hali ya juu. Pia walikuwa wanataka kuimarisha minyororo ya usambazaji kati ya India na Marekani,” aliongeza.

Mwakilishi wa Marekani wa biashara Katherine Tai Alhamisi hii alisema kuwa Makubaliano ya India na Nchi za Pacific juu ya Uchumi na Maendeleo yanatoa fursa ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama na pia itawezesha kukabiliana na changamoto kwa pamoja.
Alisema kuwa IPEF pia inaruhusu kufanya kazi pamoja kujenga jukwaa la kushughulikia changamoto za siku zijazo na kuleta ukuaji endelevu na wenye usawa katika eneo la India-Pasifiki.

Makubaliano ya Uchumi wa nchi za Indo-Pasifiki(IPEF) ulizinduliwa kwa pamoja na Marekani na nchi nyingine washirika wa eneo la Indo-Pasifiki mnamo tarehe 23, Mei 2022, mjini Tokyo.

India ilijiunga na IPEF na Waziri Mkuu wake Narendra Modi alihudhuria hafla ya uzinduzi pamoja na Rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio na viongozi wengine kutoka nchi washirika.

Hapo awali,Mikutano ya Mitandaoni ya Mawaziri ilifanyika mara tu baada ya uzinduzi wa tarehe 23 Mei na baadaye kuanzia tarehe 26-27 Julai, 2022.

India imejidhatiti kufanya makubaliano ya kikanda ya Indo-Pasifiki yanakuwa huria, wazi na jumuishi na ingejitahidi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya washirika kwa ukuaji na ustawi wa eneo hilo.

Makubaliano haya ni jumuishi na yanaruhusu marekebisho kwa nchi washirika kuchagua vipengele na maeneo kulingana na vipaumbele vyao husika, Wizara ya Biashara na Viwanda ilisema katika taarifa.

IPEF ni kundi la nchi 13, ni Mkataba/Makubaliano ya kiuchumi unao husisha nchi zaidi ya mbili. Katika siku za hivi karibuni, India inaonekana kuangazia mikataba ya biashara huria baina ya nchi mbili badala ya ile ya kimataifa.
ANI-20220909180511.jpg
 
Back
Top Bottom